Vijana wa Udhamini wa Nasser wako kwenye matembezi ya kiutalii huko eneo la Piramidi za Giza na Saqara
Shughuli za siku ya 4 ya Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa " zilianza kwa kupanga matembezi ya kiutalii katika eneo la piramidi za Giza na Saqara, kwa wajumbe Vijana walioshiriki katika Udhamini huo , ambapo walitazama Piramidi ili wajue zaidi kuhusu Ustaarabu wa kifarao wa kale.
Vilevile , Mkurugenzi Mkuu wa eneo la mabaki ya kale ya ya Saqara , Dkt. Sabri Farag alikuwa wa kwanza wa kuwapokea washiriki wa Udhamini huo, akiambatana nao matembezi yao ya ziara ya kutazama maeneo ya kale katika eneo hilo na Piramidi tatu.
Washiriki wa Udhamini walisikiliza maelezo ya kina kuhusu historia ya mahali palipovutia Dunia nzima, Piramidi na jinsi zilivyojengwa, na kuhusu kipindi kile cha historia ya kifarao ya Misri , pia washiriki walifikia eneo la Panorama ambapo walipiga picha kadhaa za kumbukumbu na walinunua vipande vya kale pamoja na zawadi za kumbukumbu.