Mbio za Marathon za michezo kwenye mji wa Michezo huko Mji Mkuu mpya wa Utawala
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, akiwakilisha Rais wa Jamhuri alianzisha Mbio za Marathon katika mji wa Michezo huko Mji Mkuu Mpya wa Utawala, ikiwa ni mojawapo ya shughuli za siku ya 13 ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa Gamal Abd El Nasser katika toleo lake la pili kwa wajumbe Vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo .
Marathon iliyoandaliwa ilijumuisha Baiskeli, pikipiki, na Marathon kwa Mbio kuzunguka na ndani ya mji wa Michezo huko Mji Mkuu mpya wa utawala, vilevile mwishoni mwa Marathon hiyo washiriki walipiga picha za kumbukumbu kwa hali ya furaha tele ya watu wote wakielezea Shukrani zao kwa Wizara ya Vijana na Michezo; kuipanga Marathon ambayo ni miongoni mwa shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa .