Liao Liqiang... Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China mjini Kairo

Liao Liqiang... Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China mjini Kairo

 

‏Imefasiriwa na / Alaa Zaki


Bw. Liao Liqiang alizaliwa mnamo Julai, mwaka wa 1964 katika mji wa Li-ling, Mkoa wa Hu-nan.

Shahada za Kielimu: 

Ana shahada ya Uzamili katika Usimamizi mkuu.

Uzoefu wa kazi :

Alifanya kazi kama mfanyakazi katika ofisi ya utafsiri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China mwaka wa 1986.

Mfanyakazi na mshikaji wa kidiplomasia katika Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China katika Jamhuri ya Senegal kuanzia (1986-1991).

Mshikaji wa Kidiplomasia katika Idara ya Masuala ya Ulaya Magharibi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China, mwaka 1991.

Katibu wa Tatu, Katibu wa Pili katika Ofisi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China mnamo kipindi cha (1991-1995).

Katibu wa Pili, Katibu wa Kwanza, Mshauri katika Ofisi ya Mambo ya Nje ya Baraza la Jimbo la China na Kundi linaloongoza la Mambo ya Nje la Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China mnamo kipindi cha (1995-1999).

Mshauri katika Idara Kuu ya Masuala ya Vyombo vya Habari ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China mnamo kipindi cha (1999-2002).

Meya Msaidizi wa mji wa Mian Yang, Mkoa wa Si-chuan, mnamo miaka ya 2002 na 2003.

Mshauri katika Ofisi Kuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China mnamo kipindi cha (2003-2008).

Kada katika ngazi ya Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Ofisi Kuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China mnamo wa miaka ya 2008 na 2010.

Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China katika Ufalme wa Ubelgiji mnamo kipindi cha (2010-2014).

Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Idara ya Mambo ya Nje ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China mnamo kipindi cha (2014-2019).

Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na mjumbe wa Jamhuri ya Watu wa China kwenye Umoja wa Nchi za Kiarabu tangu mwaka wa 2019.

Vyanzo

Tovuti ya Ubalozi wa China mjini Kairo.