Kikao cha Mazungumzo (Marekebisho ya Kiuchumi, Ujumuishaji wa Fedha na jukumu la Benki Kuu ya Misri)
Kikao cha mazungumzo kiliandaliwa katika hitimisho la shughuli za siku ya saba ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwa kauli mbiu " Marekebisho ya Kiuchumi, Ujumuishaji wa Fedha na jukumu la Benki Kuu ya Misri", kwa mahudhurio ya Khaled Bassiouni, Mkurugenzi Mkuu wa Ujumuishaji wa Fedha kwenye Benki Kuu ya Misri.
Khaled Bassiouni alianza kuelezea ufafanuzi wa ujumuisho wa fedha ambao ni kutoa bidhaa na huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya makundi yote ya jamii ili kurahisisha maisha, akiashiria hali ya maisha ambayo inakumba kila mtu wakati mfumo huo unapoporomoka,ambapo watu hawakuweza kukidhi mahitaji ya familia zao, lililoshawishi kuibuka kwa Istilahi ya ujumuishaji wa kifedha, na sio tu kwa mfumo wa benki, lakini pia ilijumuisha ofisi za posta na rehan za ujenzi.
Katika hotuba yake, Bassiouni alionesha maendeleo ya kiwango cha ujumuishaji wa kifedha nchini Misri, ambapo mnamo 2010 kilikuwa %10 , mnamo 2014 kiasi cha ujumuishaji nchini Misri kilifikia 14% na kisha kimeongezeka mwaka 2017 hadi 33% mpaka Kiwango cha ujumuishaji wa kifedha nchini Misri mnamo 2020 kilifikia 53.6%, Alisisitiza kuwa mafanikio hayo yamefikiwa kwa kufanyia kazi vipengele kadhaa vilivyoainishwa kwa uwazi, baada ya kufanya tafiti kamili za makundi mbalimbali yanayowakilisha jamii ya kimisri na zimeshatoa matokeo yaliyowakilisha mahitaji inayohitajika kwa makundi mbalimbali ili kufanyiwa kazi moja kwa moja na kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya walengwa.
Bassiouni katika hotuba yake aliongeza kwamba Benki Kuu ya Misri kupitia kazi zake, inalenga makundi mengi, wakati ambapo wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wazee wanazingatia miongoni mwa wa muhimu zaidi na hiyo kupitia kufanyia kazi vipengele vinne vinavyowakilisha vipengele vya kazi za Benki Kuu ya Misri, navyo ni: kuelimisha , maelewano ya kifedha, ulinzi wa watumiaji, na utofauti wa Huduma za kifedha ili kukidhi mahitaji ya jamii, teknolojia na utegemezi wa huduma za kielektroniki kama njia ya kulipa, na majengo madogo, ya kati na majidogo, akiashiria kwamba huduma nne za kifedha ambazo wananchi wanazihitaji, nazo ni kuweka akiba, kukopesha, malipo na bima.vilevile , alionesha baadhi ya mifano ya miradi ambayo Benki Kuu inaifanyia kazi kwa ajili ya kuwapatia walengwa haswa ile miradi inayohusika na wanawake na vijana iliyokuja baada ya utafiti na masomo ya mahitaji ambayo makundi hayo wanaihitaji .
Washiriki wa Udhamini waliuliza maswali kadhaa kwa Khaled Bassiouni baada ya kumaliza kikao cha mazungumzo ,kisha washiriki wakapiga picha za kumbukumbu wakati wa hali ya kusherehekea na furaha kutoka wote kutokana na kikao muhimu na taarifa zenye thamani wamezipata kutoka kikao hicho cha mazungumzo.