Wanafunzi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi watembelea Klabu ya Sinema ya Kiafrika

Wanafunzi wa Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi watembelea Klabu ya Sinema ya Kiafrika


Miongoni mwa shughuli za siku ya tano kwa Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kiafrika  , zinazoandaliwa na Ofisi ya Vijana wa Afrika na Idara kuu ya Bunge na Elimu ya Kiraia, pamoja na usimamizi wa Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, wakati wa kipindi cha 8 hadi 22 Juni, kwa kushirikiana na Umoja wa Vijana wa Afrika.

Vijana walioshiriki walitembelea ukumbi wa Sinema wa Hanager ambapo Filamu mbili zilioneshwa (Sambine) na (Photo Copy) Sherehe hiyo iliyooneshwa  na msanii Mohamed Galal, Mkurugenzi wa Ofisi ya tamasha la   Luxor  la   semina ya kiafrika , ilianza kwa maneno kuhusu sinema za Kiafrika na  shughuli za klabu, kisha mkosoaji wa filamu Farouk Abdel Khalek, Mkuu  wa  taasisi ya  Vijana wasanii , alitoa hotuba    ya kuwakaribisha vijana wa Kiafrika.

Alielezea furaha yake kubwa kwa kusheherekea mkurugenzi wa Senegal Othman Sembene katika kumbukumbu yake, kisha  mtungaji Ahmed Halba, mratibu mkuu wa tamasha hilo, alizungumzia shughuli za klabu na umuhimu wake katika kutoa filamu za Afrika zilizoshinda tuzo kutoka kwa tamasha la Luxor na kuenezwa kwa shughuli zake katika mikoa ya Misri mbalimbali . vilevile ,Msanii Yasmine El Hawary  alizungumza kwa niaba ya mkurugenzi Azza Al Husseini., Mkurugenzi wa Tamasha, juu ya kuadhimisha kumbukumbu ya marehemu mkurugenzi wa Senegal Ousmane Sembene; Maadhimisho haya yanafanyika katika nchi 38 za Afrika mnamo wakati mmoja kupitia mradi wa "Sambine kupitia Afrika".

Hassan Ghazali, Makamu wa Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Afrika, pia alizungumza alitoa hotuba kuhusu Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika  na alimaliza hotuba yake  kabla ya kuoneshwa kwa filamu hizo mbili, mwandishi wa filamu Sayed Fouad, msimamizi wa Tamasha la Filamu la Afrika la Luxor anayesimamia  klabu kwa kushirikiana na taasisi ya  Maendeleo ya Utamaduni unaoongozwa na Dkt. Fathi Abdel Wahab, ambamo aliwakaribisha vijana wa Kiafrika nchini Misri  katika mfumo wa Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika, na pia alizungumzia Tamasha la Filamu la Kiafrika na nafasi yake katika kujua  tamaduni za Kiafrika na jukumu la sinema katika kuwaunganisha watu pamoja .

Filamu ya   "Smbene"  kwa wakurugenzi wawili " Samba Jadjigo " na " Jason Silverman "  ilioneeshwa kwa maadhimisho ya kumbukumbu ya mkurugenzi marehemu wa Senegal Osaman Sembene ambaye anaitwa mwanzilishi wa sinema ya kiafrika  na  Filamu hiyo inahusu maisha ya Sembene, ambaye  alikuwa alizaliwa mwaka wa 1923 na alifariki  mnamo  2007.

Kisha filamu ya Kimisri “Photocopy” ikatangazwa, iliyoongozwa na Tamer Ashry na kuandikwa na Haitham Dabour, ikiigizwa na Mahmoud Hamida, Sherine Reda, Farah Youssef, Bayoumi Fouad, Ali Al-Tayeb, Youssef Othman na Ahmed Dash, iliyotungwa na Haitham Dabour, iliyoongozwa na Tamer Ashry, na kutayarishwa na "Red Star". vilevile , Filamu hii inazungumzia Mahmoud, mwanamume mwenye umri wa karibu miaka hamsini ambaye anamiliki duka la vitabu kwa ajili ya kupiga chapa katika mtaa wa Abdo Pasha wakati ambapo anapoulizwa kuchapisha karatasi za utafiti kuhusu kutoweka kwa dinosaurs, jambo hili lilimfanya kupandwa na  wasiwasi tena anahisi kwamba hii itaeleza suala la  kuzorota kwa hali yake ya kifedha na idadi ya wateja wake, ambayo inapungua siku baada ya siku.