Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wajadili "Hafla na Itifaki" miongoni mwa shughuli za siku ya nane ya Udhamini

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wajadili "Hafla na Itifaki" miongoni mwa shughuli za siku ya nane ya Udhamini
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wajadili "Hafla na Itifaki" miongoni mwa shughuli za siku ya nane ya Udhamini
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wajadili "Hafla na Itifaki" miongoni mwa shughuli za siku ya nane ya Udhamini
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wajadili "Hafla na Itifaki" miongoni mwa shughuli za siku ya nane ya Udhamini

Shughuli za siku ya nane ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaoandaliwa na Wizara wa Vijana na Michezo kwa Ufadhili wa Rais wa Jamhuri Abd El Fatah El-Sisi, zimemaliza kwabkikao cha majadiliano kiitwacho "Hafla na Itifaki" kwa kuwepo kwa Mkuu wa mahusiano makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani "Kanali Tarek Elshamy", Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa "Hassan Ghazali" na viongozi wengi wa Wizara ya Vijana na Michezo.

Kanali Tarek Elshamy, Mkuu wa Mahusiano Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia mazungumzo yake wakati wa kikao cha mwisho cha matukio ya siku ya nane ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kiitwacho "Hafla na Itifaki", alionesha kuwa hafla hizo zinazingatiwa ndani ya mambo muhimu ambayo yangeweza kusababisha migogoro ya kidiplomasia ikiwa wageni hawakaribishwa kama ipasavyo na mwenyeji haswa kama hafla hizo ni rasmi ambazo Marais wa nchi na wakuu wa ujumbe wanahudhuria, aliongeza kwamba kuna sheria kuu nyingi ambazo watu wanazijitolea katika Hafla na Itifaki na miongoni mwao ni hafla za mapokezi, jinsi ya kuketi kwa washiriki wa matokeo, jinsi ya kuziweka  bendera wakati wa hafla hizo, jinsi ya kupokea uwakilishi wa kidiplomasia kwa watu husika, sheria za kupeana mkono haswa baina ya wanawake na wanaume, jinsi ya kuwapa zawadi kwa watu walioshiriki katika matukio na sheria za heshima.

Mkuu wa Mahusiano Makuu ya Wizara wa mambo ya Ndani wakati wa maneno yake mwishoni mwa siku ya nane ya matukio ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa aliweka wazi, kwamba kuna tofauti katika Hafla na Itifaki wakati wa uandaaji wa matukio ya kiraia na matukio ya kijeshi, pia matukio ya asubuhi na yale ya jioni, hivyo kuna tofauti nyingi na kati zao; tofauti za rangi, za nguo ambazo zinatofautiana kiangazi na majira ya baridi, akasisitiza umuhimu wa kuwepo kwa timu ya kazi kwa ajili ya uaandaaji na utayarishaji mzuri unaofaa wa tukio lolote ambapo timu hiyo inachangia kikubwa katika kuyafanikisha matukio yanayoandaliwa ikiwa yaliandaliwa ipasavyo kuhusiana na aina na umuhimu wa tukio hilo, pia kwa mujibu wa sheria zilizowekwa,  zinazojulikana na zinazofuatiliwa katika mambo hayo na ambazo lazima zifae sheria za Hafla na Itifaki, alionesha, kupitia kikao hicho, Video ya ziara ya Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wa chuo cha Polisi kisha alionesha Video nyingine ya mafunzo wa wanawake wa chuo cha Polisi.

Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walimwuliza Kanali Tarek Elshamy maswali mengi baada ya kwisha kwa kikao cha majadiliano ya matukio ya siku ya nane ya Udhamini kuhusu masuala mengi kama vile uratibu wa mikutano mikuu, jinsi ya kuwapokea Marais wa nchi au wanaowawakilisha, wimbo wa kitaifa, jinsi ya kukabiliana na kushindwa kwa nyakati zilizowekwa, adabu za kula chakula, jinsi ya kuandaa meza rasmi, namna kupata taarifa tofauti juu ya hafla Itifaki, na adabu za kula chakula, halafu washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walipiga picha za kukumbuka wakati wa mwingiliano, furaha kubwa ya wote waliohudhuria kikao hiki cha kipekee na taarifa muhimu za Hafla na Itifaki walizozipata.

Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Hassan Ghazaly, alionesha kwamba Udhamini huo uliitwa kulingana na Kiongozi Marehemu Gamal Abd El Nasser kwa kuwa mmoja ya viongozi muhimu zaidi wa wananchi wa nchi zinazoendelea (Afrika, Asia, Amerika Kusini) na miongoni mwa mifano ya kipekee ya Uongozi, kwa hiyo akawa akiitwa "Baba wa Afrika", vilevile Rais Gamal Abd El Nasser ni mfano wa kisiasa na kihistoria kwa dhana ya uongozi kwani alipokuwa kiongozi alitaka kuziimarisha harakati za ukombozi za kimataifa hata nchi zikawa huru, pia alichangia kwa umakini kuanzisha taasisi zilijumuisha raia ya mabara matatu; Asia, Afrika na Amerika Kusini kama vile Shirika la Mshikamano wa Raia wa Afrika na Asia, Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote, Shirika la Umoja wa Afrika na Shirkia la Ushirikiano wa Kiislamu.

Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa alionesha kuwa Udhamini huo unalenga kuhamisha uzoefu wa Kimisri wa kale kuimarisha na kujenga taasisi za kitaifa, kuunda kizazi kipya cha viongozi vijana wenye maoni yanayoendana na ushiriki wa Kusini_Kusini, kushikamana viongozi vijana walioathiri zaidi, ngazi ya mabara matatu (Afrika, Asia, Amerika kusini), mafunzo, ustadi unaohitajika na maoni ya kimkakati kupitia kuwalenga watu wengi kama waamuzi wa sekta ya umma, wahitimu wa programu ya Wajitolea wa Umoja wa Afrika, viongozi wa sekta binafsi waliotekeleza, wanaharakati wa mashirika ya kiraia, wakuu wa halmashauri za kitaifa ya vijana, wanachama wa bodi za mitaa, Wanachuoni, watafiti wa vituo vya Tafiti wa kimkakati na mawazo, wanachama wa vyama vya wafanyakazi, wafanyakazi wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na wajasiriamali wa kijamii.

Ikumbukwe kuwa shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kwa toleo lake la pili, ukiandaliwa na Wizara wa Vijana na Michezo, ikiongozwa na  Dkt. Ashraf Sobhy pamoja na Chuo cha kitaifa kwa mafunzo, Wizara wa Mambo ya Nje ya kimisri na Taasisi nyingi za kitaifa kwa Ufadhili wa Rais wa Jamhuri Abd El Fatah El-Sisi zinafanyika hadi nusu ya Juni hii kwa  kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini Kusini" kwa ushiriki wa viongozi vijana wengi wa kipekee wa mabara ya Asia, Afrika na Amerika Kusini.