Tuna Uhakika Kwamba Misri Ina Imani Kwamba Yaweza Kutoa Mchango Bora Zaidi kwa Ustawi na Furaha ya dunia

Tuna Uhakika Kwamba Misri Ina Imani Kwamba Yaweza Kutoa Mchango Bora Zaidi kwa Ustawi na Furaha ya dunia

Imetafsiriwa na/ Naira Abdelaziz 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled

 Mtu mwenye nafasi nzuri:

Nimepokea barua yako iliyoandikwa mnamo Septemba 7, 1956, kuhusu mahojiano yaliyofanyika kati yetu na kamati uliyoiongoza uliendesha,ambayo inawakilisha serikali 18 zilizoshiriki katika Mkutano wa London juu ya Mfereji wa Suez, na kamati yako inaweza kusemeka kwamba nilitoa maoni wakati wa majadiliano juu ya mambo kadhaa ya kimsingi.

Ulionesha kuwa nchi 18 zinawakilisha 90% ya nchi zinazotumia mfereji, na bila kujali kama asilimia makadirio haya yametiwa chumvi, tunachoelewa  kwa kauli  "zinazotumia mfereji" inamaanisha kujumuisha nchi hizo, hata kama hazina meli zinazovuka mfereji , zinategemea mwisho kwa kupitisha  sehemu kubwa ya biashara zao za nje,  kama mfano wa nchi hizi ni  Australia, Siam, Indonesia, India, Pakistan, Iran, Iraq, Saudi Arabia, Abyssinia, na Sudan.

Isitoshe, tatizo la mfereji lina mahusiano yenye nguvu  na kanuni za mamlaka, haki ya kumiliki mali, na heshima ya nchi, inaweza kuonekana kuwa mgogoro wa sasa ulitokea  mnamo Julai 26, 1956, wakati serikali ya Misri ilipotumia mamlaka yake kutaifisha kampuni iliyokuwa ikijulikana kama “Kampuni ya Kimataifa ya Bahari ya Mfereji wa Suez,” na hakuna Shaka kuhusu haki kamili ya serikali ya Misri kutaifisha kampuni hiyo ya Misri.

Serikali ilipotaifisha kampuni hiyo, ilitangaza kwa uwazi kwamba  imefungwa na mkataba wa 1888 unaohakikisha uhuru wa kusafiri kwenye Mfereji wa Suez, na maandalizi  yake ya kuwalipa wanahisa fidia kwa haki.

Mnamo Tarehe Agosti 12, serikali ya Misri ilitangaza utayarifu wake wa kuzialika nchi zilizotia saini Mkataba wa Constantinople mnamo mwaka 1888 hadi washiriki katika mkutano ambao serikali ambazo meli zao zilivuka Mfereji wa Suez hushiriki, Ili kuhakiki upya Mkataba wa Constantinople, na kufikiria kuhitimisha makubaliano kati ya nchi hizo  yanayothibitisha na kudhamini uhuru wa urambazaji kwenye Mfereji wa Suez.

Wakati uleule, serikali ya Misri haiwezi kulaumiwa kwa kukiuka, wakati wowote au tukio, wajibu yake yoyote ya kimataifa kuhusu Mfereji wa Suez. Wakati uleule, urambazaji katika Mfereji wa Suez umeendelea kwa utaratibu na ufanisi katika siku 50 zilizopita, hayo yote ilihali matatizo  yaliyojengwa na serikali za Ufaransa na Uingereza, na baadhi ya wadau/watu wenye mslahi kutoka kampuni ya zamani ya mifereji.

Kwa hivyo, mgogoro huu na kile wanachokiita "hali ya hatari" si chochote ila ni uzushi  unaofanywa na wahusika waliotajwa hapo juu, hii inathibitishwa na yafuatayo:

1- Taarifa zenye vitisho vya kutumia nguvu.

2- Uhamasishaji wa Ufaransa na Uingereza wa vikosi vyao na harakati wanazofanya kwa vikosi hivi.

3- Uchochezi wa wafanyikazi na waelekezi wanaofanya kazi katika Mfereji wa Suez kukosa kazi yao ghafla na Ufaransa, Uingereza, na baadhi ya wafanyikazi rasmi wa Kampuni ya Suez Canal.

4- Hatua  za kiuchumi zilizochukuliwa dhidi ya Misri.

Licha ya haya yote, mara nyingi tulisikia marejeleo ya "Suluhisho la Amani" na "Majadiliano ya Bure" ili kufikia suluhisho linalotarajiwa, Je, kuna haja ya kuthibitisha mgogoro huu kati ya ukweli ulio wazi na kusudi linalodaiwa?

Iwapo kuna vitendo vinavyotokana na ukiukaji wa wazi na kudharau barua ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ni jaribio la kutishia, kutoa shinikizo la kiuchumi, na kuchochea kuharibu kazi ya urambazaji.

Mbali na serikali ya Misri ilitangaza maandalizi kamili wa kufanya majadiliano . Kutakia lengo lake la kufikia suluhisho la Amani kwa mujibu wa malengo ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kanuni ambazo msingi wake ni, na lengo hili inafika kuwa ndilo ambalo sera ya serikali ya Misri inataka kufikia na malengo inayotaka kufikia.

Tumechunguza kwa umakini  mapendekezo yaliyowasilishwa katika Mkutano wa London na nje yake kuhusu tatizo hili, ikiwa ni pamoja na mapendekezo yaliyowasilishwa na nchi 18,  zinazowakilishwa na Kamati. Tunakubaliana na nchi 18 kwa kusema kwamba suluhisho lazima:

1- Kutumikia haki za Uhuru wa kimisri.

2- Kuhakikisha uhuru wa urambazaji katika Mfereji wa Suez kwa mujibu wa Makubaliano ya Oktoba 29, 1888.

3- Kutumikia umiliki wa kimisri wa mfereji.

4- Kuhakikisha usimamizi mzuri na wa kuaminika wa mfereji, na pia kuhakikisha matengenezo na kazi ya upanuzi.

Lakini tunapochunguza njia zinazopendekezwa na kamati kufikia malengo haya, tunagundua kuwa njia hizi zinaharibu malengo wanayokusudia, na inaishia kuwa kinyume na kile inacholenga kufikia. Mfumo mahususi uliopendekezwa na kamati kwa hakika unamaanisha kukamata kile ambacho serikali zilizoandaa mkutano huu kiliwasilisha kwa serikali zilizoalikwa kabla ya kuanza kwa mkutano huo, na ndicho kilichopitishwa katika kipindi chote hiki.

Ambalo ni  jambo lisiloepukika kwamba wananchi wa Misri watauchukulia mfumo unaopendekezwa kama mfumo unaoegemezwa kwenye uchokozi na ukiukaji wa haki na mamlaka yao ya kujitawala, Matokeo yake, ushirikiano ukawa hauwezekani. Mtu anaweza pia kuuliza kama ni Kampuni ya Mfereji ilikuwa inahakikisha uhuru wa kusafiri kwenye Mfereji huo.Je, si kweli serikali ya Misri iliyokuwa na bado ikihakikisha  uhuru wa kusafiri kwenye Mfereji huo?Je, inawezekana kivitendo kuhakikisha uhuru huu kupitia Kamati inayopendekezwa ya Mfereji wa Suez? Je, haitarajiwi kwamba kamati hii itakuwa chanzo cha sintofahamu na matatizo badala ya kuwa chanzo cha misaada na suluhisho?

Tunaiweka mbele ya macho yetu iliyo muhimu wa ushirikiano wa kweli wa kimataifa, ambao ni tofauti na udhibiti wa nchi yoyote; Iwapo udhibiti huo unafanana na ule  Misri iliondoa hivi majuzi, au udhibiti wa pamoja, hatuna chaguo ila kuuzingatia kuwa umewakilishwa katika mfumo uliopendekezwa na kamati.

Jaribio lolote la kulazimisha mfumo kama huo kwa kweli lingekuwa kielelezo cha mzozo usiotarajiwa, na lingesukuma Mfereji wa Suez katikati ya siasa badala ya kuuweka mbali nao, kama kamati inavyotaka. Vyovyote vile mfumo wa usimamizi wa kituo utakuwa katika siku zijazo; Itategemea ushirikiano wa nguvu na kamili wa watu wa Misri,  mfereji unaoendesha ardhi yao. Ni wazi kwamba ushirikiano huo - ambao ni wa lazima - hauwezi kufikiwa ikiwa wananchi watauchukulia utawala huu kuwa chuki kwao na dhidi ya mamlaka yao, haki na utu wao.

Inashangaza kweli kwamba wale wanaounga mkono kuweka Mfereji wa Suez nje ya siasa ndio hao hao waliofanya vitendo vilivyopingana kabisa na lengo hili walilotangaza. 

Nini maana ya kufanya mfereji hiyo kuwa ya kimataifa na kufanya mkutano wa London, kwa uteuzi wa wanachama walioalikwa kulingana na mpango ulioandaliwa, kisha kutuma kamati ya watu watano, vitisho vya harakati za jeshi na kuchukua hatua za kiuchumi? Haya yote ni nini ikiwa sio siasa katika maana zake zote?

Imetajwa kuwa wajumbe wa nchi yoyote iliyowakilishwa katika Kamati inayopendekezwa ya Mfereji wa Suez hawapaswi kuwa na wajibu wowote wa kufuata maelekezo ya kisiasa; Wajumbe hawa, vyovyote itakavyokuwa, watakuwa watiifu kwa nchi zao na watakuwa wafuasi wa serikali zao, na hakuna uwezekano mkubwa kwamba hawataathiriwa na mazingatio haya, na mifano uliyotaja katika hotuba yako kuhusu Benki ya Dunia na Mahakama ya Kimataifa ya Haki haiwezi kuwa halali au kushawishi.

Tunaamini kwamba kuondolewa kwa kweli kwa mfereji kutoka kwa sera kunaweza kuhakikisha kwamba hatua za kimataifa zimefungwa. Inakuja ama kwa njia ya uthibitisho au upyaji wa makubaliano ya 1888, na masuluhisho haya yote mawili yanakubalika kwetu, kama tulivyotangaza wakati wa nyuma.

Kumekuwa na madai kuwa serikali ya kimisri inalenga kutegemea upande mmoja wa nchi inazoziwakilisha, ambayo ni Uingereza, na kwamba serikali ya kimisri inaona kuwa mojawapo ya  malengo yake ya kuleta mkanganyiko katika uchumi wa Uingereza, na kuvuruga harakati za biashara na vifaa vinavyohitajika kwa Uingereza kupitia Mfereji wa Suez.

Jambo lilio wazi kwamba madai haya  mbali na ukweli, kwani hakuna mtu binafsi anayeweza kutoa sababu yoyote kwa Misri kufuata siasa kama hiyo.

Umetaja pia suala la uaminifu wa kimataifa, na nilielekeza maoni yako Mheshimiwa kuhusu suala hilo kwa ukweli kwamba uaminifu una sehemu mbili: Ingawa umuhimu wa uaminifu katika nchi nyingine haujakataliwa, imani ya wamisri ni muhimu kwa usawa katika eneo hilo, na haiwezekani kupata uaminifu  ikiwa walilazimika,Kama matokeo ya baadhi  ya vitendo na siasa. kutilia shaka na kupoteza Imani juu ya kuwepo kwa haki ya kimataifa au katika uanzishwaji wa Utawala wa sheria katika mahusiano ya kimataifa.

Ikiwa lengo la kweli  ni kuhakikisha uhuru wa kupita katika Mfereji wa Suez; Jibu ni wazi: 
 kupitia mfereji kilikuwa na bado kinaendelea na uhuru umehakikishwa. Hatari pekee inayoukabili uhuru huu inatokana na vitisho, uhamasishaji wa vikosi vya kijeshi, uchochezi wa wafanyikazi kwa kuzuia maendeleo ya kazi katika mfereji huo, na hatua za kiuchumi zilizochukuliwa dhidi ya Misri.

Lakini ikiwa lengo, kama inayokuwa wazi, ni kuchukua sehemu kubwa ya ardhi ya Misri, na ikiwa lengo ni kuwanyima Misri sehemu iliyo muhimu ya ardhi yake; Ni muhimu kutangaza hili kwetu.

Ni wazi kabisa sasa kwamba Misri - kwa asili ya mambo - ina nia ya dhati ya kudumisha Amani na Usalama sio tu katika eneo la Mfereji; Lakini katika eneo lote hupatikana, na hata katika sehemu zote duniani kote.

Ni lazima pia kuwa wazi kwamba Misri ina nia kamili - hata ikiwa tu kwa manufaa yake binafsi - katika uhuru wa kupitia mfereji na katika umuhimu wa kuendelea na usimamizi wake wa ufanisi, ujuzi na maendeleo, bila ubaguzi wowote au unyonyaji wa aina wa mtu yeyote.

Napenda kutaja - suala la mwisho - kwamba nimeieleza Kamati kwa uwazi  Serikali ya Misri iko tayari kuingia makubaliano yoyote muhimu kuhusu kutoza ushuru wa haki na ushuru wa bidhaa.

Kuhusu miradi ya uboreshaji wa mifereji uliyorejelea; Napenda kusisitiza kuwa serikali ya kimisri imedhamiria kufanya kila iwezalo katika nyanja hiyo, ndiyo ilitangaza awali nia yake ya kutekeleza mradi wa uboreshaji wa mfereji ulioandaliwa na kampuni ya zamani, na miradi mingine ambayo inalenga malengo makubwa na ya muda mrefu.

Tumetangaza kwamba sera yetu ni kwa Mamlaka ya Suez kubakia kuwa chombo huru chenye bajeti inayojitegemea, na kwamba imepewa mamlaka yote yanayohitajika bila ya kufungwa na taratibu au kanuni za kiserikali. Pia tulitangaza nia yetu ya kutenga asilimia ya kutosha ya mapato ya kituo ili kutekeleza miradi yake ya baadaye, na kutoelekeza sehemu yoyote ya mapato yanayohitajika katika miradi hii kwa malengo mengine yoyote. Serikali ya Misri  imeonesha mara nyingi nia yake ya kufaidika kutokana na uzoefu na kubadilika kwa wataalam wenye uwezo kutoka duniani kote ili kuboresha mfereji na usimamizi wake.

Kwa maoni yetu, jambo lililo muhimu katika msimamo wa sasa ni kwamba mradi uliopendekezwa yenyewe, na kile kinachoweza kutokea kutokana na hilo, unalenga kuhakikisha kuwa usimamizi wa mfereji huo ni mdogo kwa kundi maalumu la nchi zinazotumia mfereji huo. Hii inafanywa kwa kudhibiti usimamizi wake.

Waraka ambao ulisambazwa kwa nchi zilizoalikwa kwenye mkutano wa London muda mfupi kabla ya kufanyika, na hadi sasa unaonekana kuwa mwongozo kwa nchi hizi katika malengo ambayo bado wanayazingatia, unasema: “Pendekezo la kuanzisha chombo cha kimataifa kusimamia Mfereji wa Suez."

Kwanza: Ufaransa, Uingereza, na Marekani zilikubaliana kwamba wakati wa mkutano huo, rasimu ya pendekezo la kuanzisha chombo cha kimataifa cha kusimamia mfereji huo itajumuishwa kwa mujibu wa kanuni zifuatazo:

Pili: Kwamba malengo na kazi ya mamlaka hii ya kimataifa iwe kama ifuatavyo:

1- Kusimamia mfereji. 

2- Kuhakikisha kuwa mfereji unatekeleza dhamira yake ipasavyo, kama njia ya maji ya kimataifa ya bure, iliyo wazi na salama kwa mujibu wa kanuni za Mkataba wa Constantinople wa 1888.

3- Kuandalia malipo ya fidia ya haki kwa Kampuni ya Mfereji wa Suez.

4- Kuihakikishia Misri fidia ya haki kwa kuzingatia haki zote za Misri na maslahi halali.

Katika tukio la kushindwa kukubaliana na kampuni au na Misri juu ya moja ya mambo mawili  haya ya  mwisho; Suala hilo linaweza kupelekwa kwa kamati ya usuluhishi yenye wajumbe watatu walioteuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

Tatu: Vyombo vinavyounda mamlaka ya kimataifa ni:

1- Bodi ya wakurugenzi  wanaochama  huteua nchi zinazotumia sana mfereji katika urambazaji wao na biashara ya baharini.

2- Miili muhimu ya kiufundi katika suala la kazi na utawala.

Nne: Mamlaka ya kimataifa inajumuisha  hasa yafuatayo:

1- Kufanya kazi zote zilizo muhimu.

2- Kuamua ada, mrabaha na ushuru mwingine kwa misingi ya haki.

3- Masuala yote ya kifedha.
4- Uwezo wa usimamizi na udhibiti kwa ujumla.

Tunaamini kuwa utafiti wowote wa barua hii hauachi chochote katika akili ya msomaji ila lengo ni kuunyakua mfereji kutoka mikononi mwa Misri na kuuweka kwenye mikono mingine,  vigumu kwa mtu kufikiria jambo la uchochezi zaidi kwa watu wa Misri kuliko hili, na kitendo kama hicho kinabeba ndani yake kile kinachosababisha kushindwa kwake, na ni chanzo cha ukiritimba, kutokuelewana na migogoro inayoendelea. Kwa maneno mengine, inaweza kuwa mwanzo wa msukosuko badala ya mwisho wake.

Kwa upande mwingine, ningependa kusisitiza kwamba siasa ya serikali yangu inaendelea kuhakikisha:

1- Uhuru wa kuvukia Mfereji wa Suez, na kuhakikisha matumizi yake bila ya ubaguzi.

2- Kuboresha Mfereji wa Suez ili kukidhi mahitaji ya urambazaji ya siku zijazo.

3- Kuweka ada za haki na ushuru wa bidhaa.

4- Kusimamia Mfereji wa Suez kwa njia inayozingatia ufanisi wa kiufundi.

Tunatumai kuwa Mfereji wa Suez kwa hivyo utatengwa na siasa, na kwa mara nyingine tena utakuwa kiungo cha ushirikiano, manufaa ya pande zote, na maelewano ya karibu kati ya nchi za dunia, badala ya kuwa chanzo cha migogoro.

Pia tuna imani kwamba Misri ina uhakika kwamba inaweza kutoa mchango bora zaidi kwa ustawi na furaha ya dunia, na pia inachangia ustawi na furaha yake yenyewe kwa kupitisha sera hii na kupanua nia yake njema katika kila upande.

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwa Robert Menzies.

Mnamo Tarehe ya Septemba 9, 1956.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy