Lazima tugeukie siku zijazo ili kulinda Utaifa wetu

Lazima tugeukie siku zijazo ili kulinda Utaifa wetu

Imefasiriwa na / Osama Mostafa

Ndugu zangu:

Nilisema baada ya tukio la mwisho na shambulio la mwisho lililotokea Gaza kwamba sitazungumza tena, baada ya kumuwekea Amiri Jeshi Mkuu jukumu hilo, lakini kwa tukio hilo ningependa kuwaambia: Hatutasahau kamwe... Hatutasahau njama zilizopangwa ili kuondoa utaifa wa Waarabu huko Palestina.. Hatutasahau. Na kama nyinyi watu wa Palestina mliona kuwa ni maneno yenu; Sisi, watu wa Misri, tunaona kuwa imeelekezwa kwetu pia.

Lazima tugeukie siku zijazo ili kulinda Utaifa wetu; Utaifa wetu, ambao waliweza kuupenya ndani na kuuondoa humo utaifa wa Waarabu na utaifa wa Kiarabu, na kuubadilisha katika sehemu ya ardhi pendwa ya Waarabu yenye utaifa wa ajabu, lugha ya ajabu na rangi za ajabu. Njama hizo hazijaisha, lakini bado zinafanya kazi kama zimekuwa zikifanya kazi kwa miongo kadhaa, na sisi huko Misri tumesimama kuziangalia. Ninachokuomba tu ni kuwa na subira na kufanya kazi, na ninachoomba kwa taifa la Kiarabu ni kuchukua mfano kutoka kwa Mayahudi na kuchukua mafunzo kutoka kwa Mayahudi, sio kuzungumza sana, na kufanya kazi na kuungana ili kuhifadhi Utaifa wetu.

Hayo ndiyo ningependa kuwaambia, na Mwenyezi Mungu awatunze na kuwalinda.

Assalamu Alaikum warahmat Allah.

ـــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــ
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Ukanda wa Gaza wakati wa ziara yake  ghafla huko mnamo Machi 29, 1955.