Siku ya Shahidi… Jenerali Abdelmoniem Riad

Siku ya Shahidi… Jenerali Abdelmoniem Riad

Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled  

Imeandikwa na/ profesa Khairat Drgham 

Mnamo tarehe 9, mwezi wa Machi katika kila mwaka ilitangazwa Maadhimisho ya Siku ya Shahidi huko nchini Misri mnamo mwaka  1969, ambapo wakati huo ulitangazwa na Jamuhuri ya Kiarabu ya Misri ili kuadhimisha kumbukumbu ya kufariki kiongozi mkubwa Jenerali Mkuu wa kijeshi Luteni Jenerali Abdulmoniem Riad, na pia alipewa cheo cha Luteni nusu pamoja na nyota ya heshima

 Na inakumbukwa kuwa Luteni Jenerali Mohamed Abdulmoniem Mohamed  Riad, alizaliwa mnamo mwaka 1919 na alifariki Machi 9, 1969, ambapo alikuwa na cheo cha kiongozi wa opereseheni za vikosi vyenye silaha mnano mwaka 1964, na aliteuliwa kama mwenyekiti wa uongozi wa pamoja wa kiarabu, na pia katika Vita vya 1967 alichaguliwa kuwa kiongozi wa upande wa Jordani pamoja na ushiriki wake katika Vita vya Pili vya Dunia, Vita vya Palastina, Ukaidi wa Marekani , uingereza na Ufaransa dhidi ya Misri pamoja na Vita vya Kumwagilia Damu.

 Na pia aliusimamia mpango wa Misri wa kupomoa safu ya Bar Lev ، na mnamo  Machi, 3 asubuhi Luteni jenerali Abdulmoniem Riad aliamua kwenda ukandani ili kuangalia kwa ukaribu yanayotukia, na ghafla moto na makombora yalirushwa katika eneo la kuwepo kwake na kufariki kati ya askari wake na kuwa mfano wa kuigwa kwa vikosi vya kijeshi vya Misri, kiasi kwamba hakukaa ofisini mwake huko kairo lakini alitaka kuwa pamoja na wanajeshi wake ili kuwa mfano wao wa kuigwa na kuwapa amri za juu za kupambana na adui.
 Na mwenyezi Mungu amrehemu shahidi huyo , na alipewa heshima na Rais mwenda zake Gamal AbdelNasser, na siku hiyo ya  Machi 9  ilizingatiwa kuwa Siku ya Shahidi, na ili kumpa heshima zaidi uwanja mbalimbali, shule na mitaa mikuu ilibeba jina lake.

Mwenyezi Mungu awarehemu wale wanaotoa mhanga kwa ajili ya kulinda taifa letu.
 
 “ Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.”  [Al Omran : 16 ]


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy