Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Mkutano wa kilele cha kiafrika mjini Addis Ababa huko Ethiopia
Mheshimiwa Mfalme mkuu, Mheshimiwa Rais, enyi marafiki wapendwa:
Kutoka ukaribu na chimbuko la Mto Nile, ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu ulikuja hapa, ukifuatia mkondo wa mto mvutaji huo, unaofikia chimbuko mojawapo la machimbuko yake muhimu hapa katika nchi hii kubwa.
Ikiwa kuna miongoni mwenu - marafiki wapendwa - ambaye ameelezea kuvutiwa kwake kwenye ukumbi huu kwa ukarimu wa watu hawa wakubwa wa Ethiopia ambao walikuwa wenyeji wa mkutano huo nyumbani mwao na utaratibu makini wake , na kwa taifa lililofanya juu chini ili kuwezesha mkutano kufikisha jukumu lake kwa urahisi basi tayari tumeshajua tangu miaka mingi iliyopita , ambayo ni zamani kama vile historia ya binadamu , ukarimu wa nchi hii na umakini wa mfumo wake; Mafuriko hutujia kila mwaka na mwendo mzuri Mto Nile , na daima hutujia kwa wakati wake hauukosea wala kuchelewa . Kwa hivyo, Ethiopia, ardhi yake, watu wake na mfalme wake, ambaye alitoa mkutano huo wa uangalizi na juhudi yake ile ambayo sisi sote tunaiona na kuithamini na tunayokabiliana kwa Shukrani na tathmini kubwa.
Enyi Wapendwa:
Natarajia mniruhusu kufupisha hadithi hii kadiri iwezekanavyo. Ni wazi kwangu kutokana na yale niliyoyasikia hadi sasa kwamba mawazo yetu yote yanafahamiana na yanafanana upeo mmoja, na maoni yetu yanaambatana kwa maslahi yale yale. na hilo linaonekana katika makubaliano ya haraka yaliyofanywa na mawaziri wa mambo ya nje ambao wameshatutangulia kuja hapa na walifanya juhudi inastahili kuheshimika , waliweza kupitia juhudi hiyo kufikia mradi wa orodha ya ya kazi unaojumuisha masuala mengi ambayo yanavuta uzingatio wetu na kushughulikia akili yetu , kutokana na hayo mitazamo yetu imeambatana kwenye vikao hivi.
kutoka hapa , tunahisi sasa kuwa ni wakati wa kugeuza yote tunayofikiria na tunatarajia kufanya mpango wa utekelezaji, nami mtazamo wangu kwa shughuli inayohitaji juhudi zetu , unaenda kama ifuatavyo :-
Kwanza: Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu inaona kuwa hivi karibuni Bara la Afrika linakabiliana na awamu hatari zaidi za mapambano yake, na tukisema kwamba bendera za uhuru zilizopandishwa huko ardhi za Bara hilo mnamo miaka ya hivi karibuni ni shahidi kwamba mwanzo wa uhuru umeshatekelezwa. kwani mwanzo peke yake, hata kwa muujiza wake wa kushangaza , hautoshi; kwa sababu , Uhuru lazima ukue, inapaswa ukuaji wake uwe sahihi na kamili, na wenye uwezo wa kukabiliana na majukumu ya maisha mnamo kipindi chake.
Kwa hivyo, baada ya muujiza wa kuwepo, bara sasa linakabiliwa - kwa maoni yetu - changamoto za maisha, na ni lazima - wakati wa hali ngumu - kuthibitisha uwezekano wake wa kuendelea na kukua, na zaidi ya hayo, uwezo wake wa kufanyia upya maisha yenyewe kuiendeleza.
Sidhani kwamba nahitaji kuelezea kwa undani hali ngumu hizo , na labda inatosha kwangu kuziashiria, kati zake na yale yanazizungusha nje ya bara na kati zake na yale yaliyoko kwenye ardhi ya bara lenyewe.
Kutoka nje ya bara hili,bado kuna ukoloni, usioondolewa kabisa na kikamilifu katika sehemu zote za bara, pia bado uko na Ukali wake katika baadhi ya sehemu hizo, na kwa upande mwingine unajaribu kujificha nyuma ya maski ya uongo. Kuna mateso ya rangi na ubaguzi zinazolazimishwa kwenye baadhi ya sehemu za bara na wale ambao wanaiba mali yake na kuiba kazi yake, lakini hawasiti kamwe kusagasaga hadhi yake katika maonesho yake ya kwanza ya kibinadamu. Kuna kuficha nyuma ya miungano ya kijeshi ili kutumia ardhi za watu kama msingi wa kuwatishia. Kuna majaribio ya kutengeneza njia mpya na za kiubunifu za ukoloni, ambazo zinaingia kinyemela hata nyuma ya bendera za Umoja wa Mataifa zilizofanyika chini yao nchini Congo - wakati wa mgogoro wake mkali - janga la kutisha ambalo lilimuua mwanamapinduzi na shahidi mwafrika " Patrice Lumumba". Hata kwa kujifanya kwa kutoa misaada kwa watu wa bara hilo, majaribio ya kupenyeza yalitokea, na kuna msisitizo wa kugeuza bara hili kuwa ghala la malighafi kwa bei ambazo hazitoshi kukidhi njaa ya watu wake wakati ambapo faida zote zinakwenda kwa nchi zinazoagiza, zinazojaribu kufanya maendeleo yao ya viwandani na kisayansi kuwa kama ukoloni wa aina mpya kupitia kutumia vibaya utajiri wa wengine bila ushiriki kwa uadilifu .
vilevile , kuna kuchukua ardhi za watu wa bara hilo kama uwanja wa majaribio ya atomiki bila ya kibali cha watu hawa na kinyume chake matarajio yao ya Amani , na kuwa tishio la moja kwa moja kwao hata kwa hewa wanayoipumua kwenye ardhi yao ya kitaifa. pia Kuna michakato ya kunyakua ardhi za watu na kuwanyima wamiliki wake halali na kuwaruhusu walowezi waliokuja kutoka mbali na walikataa kukaribishwa kama wageni na wakaanza - kiburi na vitisho - kuweka dhuluma ya bwana. Kuna michakato ya upotoshaji kwa kauli mbiu, hata haki na hata Amani zilikusudiwa kukubali dharura za hali ilivyo, na haiwezekani kuwepo amani bila haki; kwani Kuikubali hali iliyo hiyo inamaanisha kuridhika kwa kujisalimisha, na hilo ndilo mbali zaidi na dhana ya Amani.
kwenye Bara lenyewe lina hali ngumu nyingine na ikiwa ardhi ya Afrika ni ya haki na haibebi wajibu wake, basi ina wajibu wa kuitafutia ufumbuzi bora bila kuzingatia mgawanyo wa majukumu. Kwa mfano, kuna tatizo la maendeleo duni ya kutisha, ambapo watu wengi wa bara hilo wanaishi, na hii inaleta tofauti ya kutisha kati ya viwango vya maisha katika ardhi yake na viwango vya mabara mengine yaliyoishinda kimaendeleo. Hili ni tatizo linaloathiri si tu hadhi na haki halali za bara hilo; bali lenye matokeo ya hatari kwa amani ya ulimwengu.” Amani inawezaje kuenezwa kati ya utajiri uliopita kiasi na umaskini mkali katika ulimwengu ambao umbali imeondolewa? Na tatizo la utafauti wa Kiwango cha kijamii liko ndani ya nchi yenyewe, jambo linalopaswa lijirekebishe kwa kutumia vigezo vya uadilifu zaidi vinavyowapa raia ndani ya nchi moja fursa sawasawa ya maisha. Kuna matatizo ya kimaendeleo ili kukabiliana na madhara ya ukosefu wa maendeleo na kukabiliana na mahitaji ya haki ya kijamii, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kupanga na kutoa misaada ya fedha na utaalamu na ndani ya nyanja hizo zote , bara linahitaji misaada mingi.
Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu ina mtazamo kuhusu suala la misaada ya nje, ambayo inaona kuwa ni haki ya watu walio nyuma nyuma juu ya wale waliowashinda kimaendeleo. ni haki inayotegemea mshikamano wa kibinadamu na kuimarisha Amani, hakika kwamba Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu inaona msaada huo kuwa ni wajibu wa lazima unaopaswa kulipwa na nchi kubwa za historia ya ukoloni - kabla ya nyingine - kwa fidia ya unyakuzi ambao uliwakumba ambapo bado wanaukumba raia wengi katika Afrika na Asia ambao utajiri wao ulinyakuwa ili ustawi uwe ukiritimba kwa wengine, na kinachobaki kwao ni ukiritimba wa umaskini.
Na ikiwa yuko mtu anatuuliza tusamehe yaliyopita, basi tuko tayari moyoni mwetu kusamehe, lakini hatuko tayari kusahau, tunasamehe lakini hatusahau, tunafunga ukurasa wa zamani kwa Uvumilivu , lakini tutafanya makosa tukiugeuza kwa ujinga.
Kuna matatizo ya mipaka kati ya nchi kadhaa za Afrika, nasi sote tunajua jinsi ilivyochorwa mara nyingi na jinsi ilivyopangwa.
Kuna yaliyobaki zamani yaliyoacha doa nyingi ndani ya dhamiri ya bara letu, na ambayo sasa yanahitaji juhudi kubwa katika nyanja za malezi , elimu na utamaduni ili kumkomboa Mwafrika kutoka kwa minyororo yote isiyoonekana ambayo inamfunga na kuzuia Ubunifu wake.
Hata makabiliano yetu kwa hali ngumu hizo kutoka nje ya bara na ardhi yake hufanyika katika mazingira ambayo huongeza ugomvi na hatari ya mapambano dhidi yao. Tunaendelea mapambano yetu kwa ajili ya maendeleo ya maisha ya kukabiliana makundi ya ukatili ; Kuna makundi ambayo yana maslahi ya kutuwekea ujinga , na hayasiti hata kufikia hatua ya kuwachochea ndugu dhidi ya ndugu yake , kwa kupatikana shaka ili kutuachia mavuno ya chuki.
Na kuna makundi ya Vita Baridi na mvuto wake. Kisha tunaishi katika ulimwengu ambao umbali uliondolewa kwa sababu ya maendeleo makubwa ya kisayansi, haswa katika vyombo vya usafiri, lililoleta vita vya Baridi kwenye nyumba zetu na ndani ya mioyo na akili za watu ndani ya nyumba. miongoni mwa matokeo, tunaishi katika ulimwengu ambao uko wazi kwa uwezekano, ulimwengu ambao mahitaji ya kweli na halali ya mwanadamu yameongezeka bila ya ongezeko kwa ufanisi na lenye Athari la uwezo unaoruhusu kupatikana kwa mahitaji hayo ya kweli na halali. na haiwezekani kutekeleza ahadi ya kufikia matarajio makubwa ya wanadamu isipokuwa kwa kazi mtaratibu inayohitaji ukubwa na dhamira ya kitaifa ambayo italetwa kwa utashi wa raia wa demokrasia na iwawajibishe - kwa ridhaa na ufahamu - kujitolea kwa dharura kabla ya awamu ya uzinduzi, hayo yote chini ya masharti na hatari ya Vita Baridi.
Pili: Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu inaona kwamba hatua hii ya mapambano ya kiafrika ambayo ilionekana mbele yenu, kadiri niwezavyo kwa usawa , haielekei kukata tamaa, na wala haijiachii kwenye matumaini inayotarajia ishara za njia zake tofauti zinazoihitaji kwanza kuwepo ya utashi wa moja ya kiafrika, kwa hivyo uamuzi wa kufanya mkutano huu - halipungui umuhimu kuliko maamuzi yoyote yaliyotolewa nayo.
Onyesho hili tunaloliona pembezoni mwetu katika mji mkuu huu mzuri, Addis Ababa, ni tukio la kihistoria lisiloweza kusahaulika, na bara litakaendelea kutarajia mkutano huu kwa vizazi wajao, kwa kuzingatia hatua madhubuti ya mabadiliko katika kuendeleza kazi ya kibinadamu.
endapo mkutano huo hufanyika ni ushahidi, kama nilivyosema, wa kuwepo kwa utashi huru na mmoja wa kiafrika.sisi Hatukufika hapa kwa bahati , wala hatukufika haraka, bali tulikuja kutoka njia kadhaa, na ujio wetu ulichukua majaribio ambayo hatimaye yaliweza kujifanikisha; Kwa sababu inatolewa kutokana na wito wa umoja ambao hatuwezi kuupinga, na hakuna mtu mwingine aliyeweza kutuzuia kwake .Hilo linathibitisha kwamba mashirika au makundi yote ambayo yalifanyika katika bara ili kukabiliana na hatua za awali za maendeleo ya kazi ya Afrika - katika hali na mazingira yake mbalimbali - wametambua kwamba wakati unaofaa wa kuungana pamoja umeshafika na bila kusita, kwa ajili ya utashi wa Afrika mmoja na huru kutekelezwa kutokana na mkutano wao ,Hili linathibitisha kwamba migawanyiko yote ambayo ukoloni ulijaribu kuliweka katika bara hili na kuligawanya kwa sehemu ya kaskazini mwa Sahara na kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa Afrika nyeupe, nyeusi na kahawia, na kwa mashariki na magharibi hadi Afrika inayozungumza Kifaransa na Kiingereza. zote ziliporomoka na kutupiliwa mbali na ukweli wa asili wa Kiafrika, na hakuwepo kitu chochote juu ya ardhi ya Afrika isipokuwa lugha Moja ni lugha ya hatima ya pamoja, kwa mbinu tofauti zozote za kujielezea.
Tatu: nafikia baada ya hivyo kipengele cha tatu na cha mwisho.. mwanzoni Nilisema kwamba bara hili linakumba awamu hatari zaidi za mapambano yake, na kwamba bara hilo baada ya muujiza wa kuwepo linakabiliwa na jukumu la maisha, ukuaji na kuishi kwa nguvu. pili ,nilisema endapo mkutano unafanyika ni kama ushahidi wa kuwepo utashi wa Afrika huru na mmoja, kwa mara ya tatu nasema kuwa utashi huru na mmoja huo unahitaji akili yenye busara na nguvu ya kusonga mbele ili Kuweza kuhimili machangamoto yanayoukabili, pamoja na kuweza kusonga mbele ipasavyo kwa matarajio makubwa ya Afrika, na hilo ndilo jukumu linalosubiriwa kutoka kwa mkutano huo na juhudi zake.
Ni hatua muhimu ya kutambua kwamba mipaka ya majukumu yetu na hatua muhimu zaidi kwa Utashi wetu mmoja kukutana na majukumu hayo, lakini hatua ya kweli na ya mwisho ni kuweka utashi mmoja huo kama mashine ya kuzalisha nishati ya ubunifu na kuisukuma kwa nguvu pamoja na mishipa nyeti ili kutumia mabadiliko makubwa ambayo tunayataka kuendeleza maisha katika ardhi yetu ya Afrika. Halitoshi kuona matatizo yetu, na halitoshi sisi sote kukusanyika mbele yake tu .Bali, lililo muhimu ni kufanya mazoezi ya mapambano yetu katika ngazi zake zote na kulingana na hali ilivyo. Ukoloni hautaondoka sehemu za bara letu la Afrika ambalo bado unazimiliki, kwa sababu tu tunaupigia kelele ndani ya nchi yetu kwa miaka 70 tukitarajia kwamba msimamo wa kujadiliana utamkanaisha kwa kuondoka , jambo ambalo lilitulazimisha kubeba silahana tulishangaa baada ya Kufukuzwa kwake kwa miezi tu kutoka ardhi yetu - kwa mara ya kwanza - mnamo mwezi wa Juni, na hilo baada ya ulirudi kwetu tena kwa uvamizi kamili mnamo tarehe Oktoba 29, ukikusanya majeshi ya nchi tatu kwa kujifanya kwamba urejeshaji wetu wa Mfereji wa Suez na kuondoa ukiritimba huo uliobaki kwenye ardhi yetu katika karne ya kumi na tisa ni uchokozi dhidi ya sheria za kimataifa na utakatifu wa mikataba, na tulipaswa kubeba silaha tena , licha ya kulazimishwa kubeba silaha katika mvutano, ushindi wa Suez ulikuwa ushindi kwa uhuru katika Afrika na kila mahali, na ishara ya kuokoa. ilitoa ishara ya matumaini kwa raia wa bara kadha wanaopambana.
Sisemi kwamba lazima tuwe na sera pengine katika kila sehemu ambapo ukoloni umejisambaza lakini nasema: Nia yetu njema pekee haitoshi hata ikiwa inaungwa mkono na dhamiri ya ulimwengu ambayo nguvu zake zinaongezeka siku baada ya nyingine. kwa hivyo , majukumu yetu yanatulazimisha kujiandaa kwa uwezekano wowote , inapaswa kuandaa kwa akili yenye busara na mawazo ya kusonga mbele.
Ubaguzi wa rangi na mateso hazitatosha kuziondoa, kwani ni tusi kubwa kwa wanadamu wote katika zama hizi na katika kila zama, bali upinzani hodari unahitajika kwa njia na mbinu zote mpaka kufikia silaha ya kukataa kabisa na kubadilisha jambo hilo, pia kuwageuza wale waliotaka kujitenga watu wa Afrika, wawe mbali na Ulimwengu wa kimataifa, wakifukuzwa sana kwa Ubinadamu, pia Upinzani kali unahitajika kutoka kwa akili timamu na mawazo ya kusonga mbele.
Matatizo mengine yanayotukabili kutoka nje ya bara hili yanahitaji jambo hilo hilo,Ushirikiano wa kijeshi hautaanguka moja kwa moja kama majani ya vuli, kuiba malighafi hausitishwi wala hautafikii hatua ya kushiba, na walowezi hawatakubali kupata haki ya mgeni kama kibali cha kuacha kiburi cha bwana, lakini Afrika inakumba mvutano katika kila tatizo kutoka matatizo haya ambao unahitaji akili yenye busara na mawazo ya kusonga mbele. Vilevile, matatizo yetu Barani; Matatizo ya ukosefu wa maendeleo katika nchi zote za kiafrika, matatizo ya utafauti wa usawa wa kijamii ndani ya kila taifa la Afrika, kisha matatizo ya maendeleo, mipaka na elimu yote yanahitaji jambo hilo hilo ... akili yenye busara na mishipa nyeti ikiwa sote tuyaone na mtazamo huo huo, na tunaamini kwa dharura ya kutafuta suluhisho kwake. Kwa kigezo hicho hicho , majukumu ya Afrika kwa Amani ya Ulimwengu , na hii haimaanishi hata kidogo kwamba Afrika itageuka kuwa jumuiya ya kimataifa au kwamba kazi ya Afrika itatengwa na harakati ya maendeleo ya binadamu nzima .Hilo ndilo la mwisho tunalofikiri au kuliomba . bali sisi tunazingatia kufikia kiasi hicho ni ubaguzi ambao hatuwezi kuvumilia matokeo yake.
Ni bahati nzuri kwamba mkutano wetu katika ukumbi wa Umoja wa Mataifa huu daima unatukumbusha kwa lile tunalitamani ambalo ni upanuzi wa matumaini ya mataifa uliyayoanzisha na kuyalinda mbele ya kila tishio linalolitishia . jambo ambalo tunataka kuliweka wazi ,kama nilivyosema ni akili timamu ya kiafrika na mishipa ya kiafrika ya kusonga mbele inayowezesha utashi wa kiafrika wa uhuru na mmoja kupambana na matatizo na changamoto zinazolikabili bara hilo na kupunguza uwezo wake wa kujiendeleza maisha yake bara hili na kupunguza uwezo wake na hivyo inapunguza michango yake katika harakati za maendeleo ya binadamu.
kazi hiyo ndiyo inayongojea mkutano huu, na kwa kadiri ya kuifanikisha, itakuwa kadiri ya unavyotekeleza majukumu yake ya kihistoria kwa Afrika na kwa ubinadamu, akili na nguvu kwa ajili ya utashi huru na mmoja wa Kiafrika.. akili yenye hekima na ujasiri pamoja , anayepigana kama mjenzi na anayejenga kama mpiganaji, anayepigana kwa uwezo wa kujenga na uvumilivu wake , anajenga kwa hamasa ya mpiganaji na kujitolewa kwake , na mishipa yenye ujasiri na ubunifu , anakabiliana na hatari na ana uwezo wa kuboresha mitazamo yake ili kuona upeo mpana na mpya kwa njia za maendeleo ya ubunifu.
haya ni - kabla ya mengine - majukumu yetu hapa.. Shida zetu hazihitaji ufafanuzi mpya , Sote tunaziona. utashi wetu mmoja hauhitaji ushahidi wa uwepo wake. Sote kwenye ukumbi huu. Tunachohitaji ni machine ya kuzalisha nishati kutoka kwa matumaini yetu makubwa, kutoka kwa uwezo wetu usio na kikomo, na kuuelekeza na hapa ndio hitaji letu la akili yenye busara na mishipa ya kusonga, kwa ajili iwe chuo kikuu cha Kiafrika, iwe makubaliano kwa Afrika yote, iwe mikutano ya endelevu kwa marais wote wa nchi za Kiafrika na wawakilishi wake maarufu, iwe chochote.. Jambo moja ambalo Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu hailitaki.. ni tuondoke kutoka hapa kwa maneno ya shauku au mipango isiyo na faida na kwa hali hii tunajidanganya na kutowadanganya wengine, na kwa hali hii tunaichukiza Afrika na Amani, bali kwa hali hii tumepoteza kile tulicho nacho, ambacho ni maoni ya matatizo yetu na mshikamano wa utashi wetu.
Enyi Marafiki Wapendwa:
Kiwe Chuo Kikuu cha Kiafrika.. Hili lililokiriwa na Mkataba wa kazi ambalo lililodhinishwa na Kongamano la Kitaifa lililochaguliwa kidemokrasia katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, ambalo lilipitishwa mnamo Juni mwaka jana; kwa ajili ya uwe mkataba kwa Afrika zima.. ili Kuwepo mikutano katika ngazi zote rasmi na kitaifa kama tulivyosikia hapa kutoka kwa marafiki kadhaa, iwe chochote, basi lazima kiwe kitu cha kweli. Tuandalia mipango tunaitaka , tuweke muda maalum ili kukomesha ukoloni,tuanzishe miradi ya ushirikiano wa kiutamaduni na kitaaluma na tuanze kupanga ushirikiano wa kiuchumi wetu kuelekea soko la Afrika la pamoja.
Haya yote - na mengine - yanangoja juhudi zetu, lakini yote yanahitaji akili yenye busara na nguvu ya kusonga mbele na tukumbuke daima kwamba mpango wowote tutakayoanzisha liwe ubongo na mishipa ya kusonga kwa utashi wangu wa kiafrika halitajenga Mshikamano wa kiafrika kwa siku moja. lakini daima itatiwa moyo na matamanio yake, na itachora mipango ya kuyafanikisha kwa uwezo unacho kuwa , na inafuata kuutekeleza kwa uangalifu mkubwa, kwa hali hiyo hauonyeshi umoja wake tu, bali pia huongeza undani wa hisia yake kwa umoja. ; kwa maana inatolewa kutokana na matumaini ya umoja na huongeza ufanisi wake moja kwa moja kupitia mazoezi ya kujaribu tajriba katika hali halisi.
Marafiki Wapendwa:
Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu ilikuja hapa kwa moyo wazi, nia iliyo wazi, na kulithamini jukumu lililojawa na nia ya dhati, nalo liko tayari kuvumilia kiasi chochote cha majukumu yake ya kihistoria kwa bara letu la Afrika. Tulikuja hapa bila ubinafsi, hata tatizo ambalo tunalizingatia kuwa mojawapo ya matatizo yetu makubwa zaidi, ambayo ni tatizo la Israel, ambayo kwa hakika iliona kwetu nchi za kundi la Casablanca kuwa ni njia miongoni mwa njia za uingiaji wa wakoloni ndani ya bara, msingi mojawapo wa misingi yake ya ukatili ambayo hatutajadili katika mkutano huu, tukiamini kwamba maendeleo ya kazi ya Huru ya Kiafrika itaonesha ukweli siku baada ya nyingine kupitia uzoefu na kuuondolea uwongo wote mbele ya dhamiri ya Waafrika.
Kama hivyo , tulikuja hapa bila ya kukataa , bila matakwa.Tunaamini kwamba kazi ya pamoja itajibu uhitaji wetu la kupinga, na tunaamini kuwa mafanikio ya kazi ya pamoja hii yatakidhi matakwa yetu yote.
Enyi Marafiki Wapendwa:
Katika mkutano huu ambao ukifanyika utazingatiwa kuwepo utashi huru na moja wa kiafrika, basi ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu uko tayari ili kufanya juu chini kwa uaminifu na bidii ya hali ya juu ili kufikia mfumo unaofanya utashi wa kiafrika wa uhuru na moja ni akili yenye busara na mishipa ya kusonga mbele . Kwa njia hii, itatekelezwa matumaini yote ya Afrika ya uhuru na hadhi , bali itatekelezwa kwa Afrika matumaini yote ya utu katika Amani inayotegemea Haki.
Haya kwaherini, Amani za Mungu ziwe nanyi , juhudi zenu zibarikiwe.