Ujasiri wa Nasser na Hekima ya Nkrumah: Kurudi kwa Mizizi 

Ujasiri wa Nasser na Hekima ya Nkrumah: Kurudi kwa Mizizi 

Hakika, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abi Ahmed na wenzake hawajui  ukweli wa jukumu la kimisri katika Harakati ya Muungano wa kiafrika, ambapo mji mkuu wa nchi yake unashuhudia jambo hilo. 

Pengine  tunamsamehe na tunatafutia sababu kwake, kwani yeye ni miongoni mwa vizazi walivyopatikana kwenye kukandamiza na vurugu za kiserikali za kijeshi katika nchi yake.

 Lakini, haikubaliki kamwe mtu aliye na Uzamivu na Tuzo ya Nobel , kujaribu kuhoji kitambulisho cha Kiafrika kwa Misri. Na anaongoza Harakati yenye athari za zamani inayounganisha  rangi nyeusi na wazo la Kiafrika kama sehemu ya mchakato wa  Usaliti wa kisiasa , kwa ajili ya kupata msaada wa ndugu zetu waafrika wasio waarabu katika suala la Bwawa la El Nahda.

Inawezekana kwake  kurudi tena  rekodi za jumba lake la utawala au Kumbukumbu ya makao makuu ya Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa nchi yake; kujua jinsi Gamal Abd El Nasser, alipokewa akiambatana na Ahmed bin Bella katika ndege moja kuelekea Adis Ababa kuhudhuria Mkutano wa kilele cha kiafrika mnamo 1963. 

Nasser alikuwa akielezea mwelekeo wa kipekee katika Harakati ya Muungano wa kiafrika, naye aliyeitwa na Ali Mazroui kama "Afrabia" kupata nguvu ya mahusiano ya kihistoria na kiustaarabu kati ya Waarabu na Afrika.Na ubalozi wetu huko Adis Ababa uliitwa ubalozi wa kiarabu, na huko Nasser alikutana na viongozi wa Harakati ya Ukombozi wa Afrika, waliokaribishwa kupitia Waziri Mohamed Faik kwani anawajua vizuri. 

Na miongoni mwa maamuzi ya kilele ni kuunda kamati ya kusaidia harakati za ukombozi wa kitaifa, na bila shaka wanachama wake wa kwanza walikuwa na Misri na Algeria. 

Je! Damu za Mashahidi wamisri hazikuchanganyika na damu za ndugu zao kutoka Algeria katika kutetea ardhi , Heshima, na kumfukuzwa mkoloni?  Na Pengine Kurudi kwa fuvu la Shahidi mmisri kutoka Ufaransa kwenda Algeria kunatukumbusha Muungano wa kina uliotetewa kutoka kwa kizazi cha kwanza cha waanzilishi.

Wakati wa utawala wa Rais Thabo Mbeki, aliyesambaza Mpango wa Maendeleo mapya barani Afrika unaojulikana kama NEPAD, nilialikwa kwa semina ya kujadili suala hilo kwa mahudhurio ya Rais mwenyewe. 

Wakati nilipotoa hotuba yangu, mmoja wa hadh