Siku ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano kati ya nchi za Kusini-Kusini

Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa ilipitisha azimio (58/220) mnamo Desemba 2003, ikizingatia tarehe 19 ya Desemba kama Siku ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano kati ya nchi za Kusini, na mnamo tarehe 22 Desemba 2011, kwa mujibu wa azimio lake (550/66) Jumuiya kuu iliamua kwamba, kuanzia mwaka 2012, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirikiano kati ya nchi za Kusini yatabadilika kutoka Desemba 19 ikawa Septemba 12,kama kuadhimisha kumbukumbu ya Kupitishwa kwa Mpango wa Utendaji wa Buenos Aires kwa kuhimiza na kutekeleza wa Ushirikiano wa kiufundi kati ya Nchi Zinazoendelea mnamo 1978.
Na Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini Kusini ni Moja ya marejeleo muhimu zaidi ambayo Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unategemea.
Ushirikiano wa Kusini-Kusini unamaanisha Ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi zinazokuwepo kusini mwa Dunia katika nyanja za kisiasa au kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kimazingira au kiufundi, pamoja na kubadilishana maarifa , uzoefu, ujuzi, masuluhisho tofauti na teknolojia, kuunda fursa za kazi, Miundombinu na kuimarisha biashara Katika nchi za Kusini, na hiyo ni mojawapo ya sura za mshikamano kati ya raia na nchi za Kusini, linalochangia kutekeleza ustawi wao wa kitaifa , na kujitegemea kitaifa na kikundi .Ushirikiano huo umechangia ongezeko la kiwango cha biashara, mtiririko zaidi wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, na hatua za kukwenda kwa ushikamano wa kikanda kati ya nchi za Kusini. inawezekana pia Ushirikiano huo uwe kati ya nchi mbili au kikanda au baina ya kanda tofauti, na unaweza kujumuisha nchi mbili au zaidi kutoka kwa nchi zinazoendelea.
Pia kuna ushirikiano wa pande tatu, na ushirikiano huo ambapo nchi zilizoendelea na mashirika ya kimataifa hurahisisha mipango kati ya nchi za Kusini, kwa kutoa Ufadhili, mafunzo, idara na mifumo ya teknolojia, pamoja na aina nyingine za misaada . Ushirikiano wa pande tatu hujumuisha nchi mbili au zaidi kutoka nchi zinazoendelea kwa ushirikiano na upande wa tatu, kwa kawaida huwa ama nchi iliyoendelea au shirika la kimataifa, ambalo huchangia katika kubadilishana ujuzi na rasilimali zake.
Malengo makuu ya Ushirikiano kati ya nchi za Kusini yanafupishwa kama ifuatavyo
Kwanza: Kuhimiza nchi zinazoendelea kwa kujitegemea kupitia kuimarisha uwezo wa kibunifu wao wa kupata masuluhisho kwa matatizo yao ya kimaendeleo, kulingana na matarajio na mahitaji yao na uwezo pia.
Pili : kuhamasisha na kukuza kujitegemea wengi ndani ya nchi zinazoendelea kupitia kubadilishana Uzoefu, na kupata faida kutoka kwa Vyanzo vyake vya kiufundi kikamilifu, pia kuimarisha uwezo wake; uwe usaidizi mkuu.
Tatu: Kuimarisha uwezo wa nchi hizo zinazoendelea wa kuainisha na kuchambua kwa pamoja masuala makubwa, kutilia mkazo kwa kuziendeleza na kuunda mikakati muhimu ya kuendesha, kuwezesha na kuunga mkono mahusiano yao ya kiuchumi ya kimataifa .na hivyo inatekelezwa kupitia kukusanya maelezo yanayopatikana katika nchi hizo na taasisi husika zinazokuwepo ziangalie masomo ya pamoja kwa lengo la kuanzisha mfumo mpya wa kiuchumi wa kimataifa.
Nne: Kuongeza Ushirikiano wa kimataifa kwa upande wa Kiwango,kuuimarisha kwa upande wa Ubora, na kuboresha ufanisi wa Vyanzo husika kwa ajili ya Ushirikiano wa kina wa kiufundi, na hivyo kwa kuunganisha uwezo.
Tano: Kuimarisha uwezo wa kiteknolojia uliopo sasa hivi katika nchi zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na sekta ya kijadi, kuboresha ufanisi wa kutumia uwezo huo na kuunda uwezo mpya, na kutilia maanani katika upande huo, kwa kuhimiza uwasilishaji wa teknolojia na ujuzi unaosambamba na kile kilichopatikana katika nchi zinazoendelea kutoka rasilimali na nguvu za kimaendeleo kwa namna inavyopeleka kuimarisha uwezo wao wa kujitegemea binafsi na wa pamoja.
Sita: Kuongeza na kuboresha mawasiliano kati ya nchi zinazoendelea, linalosababisha kuunda maelewano zaidi kwa matatizo ya pamoja na kuongeza fursa za kupata maarifa na uzoefu unaopatikana, pamoja na kuunda ujuzi mpya kwa lile linalohusiana na kutatua matatizo ya maendeleo.
Saba: Kuboresha uwezo wa nchi zinazoendelea wa kupokea na kuwezesha teknolojia na uzoefu ili kukidhi mahitaji maalum ya maendeleo yao;
Kujua matatizo na mahitaji ya nchi za maendeleo ya chini zaidi , nchi zisizo na Ufukwe, visiwa vinavyoendelea na nchi zilizoathirika zaidi.
Hatimaye, kuziwezesha nchi zinazoendelea kufikia kiwango kikubwa cha kushiriki katika shughuli za kimataifa za kiuchumi, na kupanua Ushirikiano kati ya nchi.