Siku ya Wakulima nchini Tanzania

Siku ya Wakulima nchini Tanzania

 

Imefasiriwa na / Aya Nabil

"Siku ya Wakulima" ni tukio maalum kwa wakulima na wafugaji nchini Tanzania, na ni likizo rasmi ya kitaifa  inayoadhimishwa kila mwaka mnamo Agosti 8. Kabla ya hapo, ilikuwa ikiadhimishwa mnamo  Julai 7, iliyojulikana kama "Saba Saba", lakini katikati ya miaka ya 90 serikali iliamua  kuwa Siku ya Wakulima iadhimishwe mnamo Agosti 8 kila mwaka, na kuacha Julai 7 (Saba Saba) kama siku ya wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni, kwa hivyo, Agosti 8 iliwekwa kwa ajili ya kuadhimisha wakulima na wafugaji kama tukio maalum kwao pekee.

Siku ya wakulima iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977; kwa lengo la kukuza sera ya serikali kwa kauli mbiu ya "Sera ndiyo kilimo", na kwa miaka mingi sera hiyo ilibadilishwa kuwa "Sera ya kilimo", kwa sababu maadhimisho hayo yakawa ya kisiasa zaidi, na ya kibiashara kuliko malengo yake ya awali, na Tukio hilo ni fursa muhimu ya kuonesha teknolojia na maendeleo mapya katika kilimo kwa kuonesha mazoea bora, tangu kuanza kwa maonesho ya kilimo mnamo Agosti mosi, ambayo huwapa wakulima, taasisi na wadau wa kilimo kote nchini fursa ya kuonesha bidhaa zao na mafanikio yao katika kilimo.

Maadhimisho ya "Siku ya Wakulima" pia yaashiria Maonesho ya Kilimo, ni maonesho ya wiki moja ambayo hufanyika kila mwaka katika maeneo tofauti ya Tanzania.Katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima, wakulima na wadau wa kilimo (kama vyuo vikuu, taasisi za utafiti, wasambazaji wa pembejeo, au viwanda vya kuzalisha mbolea) huonesha teknolojia na mawazo mapya, tena uvumbuzi na suluhu mbadala zinazohusiana na sekta ya kilimo, ambapo serikali na makampuni binafsi hutoa huduma na shughuli zao kwa umma.

Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu ya Tanzania itashiriki katika maonesho ya kitaifa yanayopangwa kufanyikwa katika viwanja vya "John Mwakangale", Mkoa wa "Mbeya", kuanzia Agosti mosi hadi 8, 2023,pia Taasisi hiyo itakuwepo katika maeneo mbalimbali ya maonesho hayo.

Mnamo Agosti mosi, 2023 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango alifungua maonesho ya kitaifa yanayofanyikwa katika viwanja vya "John Mwakangale" Mkoani mwa "Mbeya".

Kwa kumalizia, siku hiyo  inakuja kama shukrani na heshima kwa wakulima na mchango wao muhimu katika uchumi wa kitaifa wa Tanzania.

Vyanzo