Miaka 103 tangu Uhuru wa Afghanistan

Miaka 103 tangu Uhuru wa Afghanistan

Imetafsiriwa na/ Husna Mohammed 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Leo, pamoja na maadhimisho ya miaka 103 ya watu wa Afghanistan, nashuhudia mapambano ya watu wa Afghanistan kwa ajili ya uhuru, kama Afghanistan ilipata uhuru wake kutoka Uingereza mnamo Agosti 19, 1919, chini ya uongozi wa Mfalme Amanullah Khan, tunatoa rambirambi zetu za kina kwa familia za waathirika, na kutangaza mshikamano wetu mkubwa na watu wa Afghanistan wenye kiburi, ili kuondokana na hali hii ngumu ambayo Afghanistan inapitia.

Afghanistan ina umuhimu wa kijiografia kwa sababu ya eneo lake linalounganisha Magharibi, Mashariki, Kusini na Asia ya Kati, na hakuna shaka kwamba hali ya sasa, ikiwa haijadhibitiwa, inaleta tishio kwa usalama wa kitaifa na utulivu wa kimataifa, kwani machafuko haya ya kisiasa yanawakilisha tishio la kikanda na kimataifa, na inaweza kuacha machafuko katika Mashariki ya Kati, hasa baada ya kujiondoa kwa Umoja wa Mataifa wa wafanyakazi wake na raia kutoka ndani, kwa hivyo inahitaji juhudi zaidi kutoka kwa jumuiya nzima ya kimataifa ambayo itapunguza vurugu huko, katika Jaribio la kufikia suluhisho zinazokidhi pande zote, kulinda maisha ya watu wasio na hatia na kuhifadhi haki zao.

Mshikamano wa Harakati ya Nasser kwa Vijana na watu wa Afghanistan leo unakuja kwa ubinadamu kwanza, na kulingana na kiwango cha mahusiano ya kihistoria kati ya Misri na Afghanistan, ambapo msimamo wa kisiasa wa pamoja wa nchi hizo mbili kuelekea masuala ya kikanda, tangu miaka ya sitini ya karne iliyopita, hasa wakati Misri ilivunja mahusiano yake na baadhi ya nchi, Afghanistan ilikuwa nchi inayofadhili maslahi ya Misri, na kwa kupita kwa mahusiano ya Misri na Afghanistan katika hatua kadhaa, hadi na baada ya matukio ya 2001 na uhamishaji wa madaraka kwa mara ya kwanza katika historia ya Afghanistan, na kuingia kwa mahusiano ya nchi mbili katika zama mpya. Misri ilikuwa na nia ya kutoa njia zote za msaada kwa watu wa Afghanistan na serikali, kwa njia inayochangia kuhifadhi uhuru wa Afghanistan, na kufanya kazi ili kuboresha kiwango cha maisha ya watu wa Afghanistan katika nyanja zote, tunayotumaini itarudi tena na Afghanistan itafurahia uhuru wake tena, na kwamba usalama na amani itaimarishwa kwenye eneo lake.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy