Siku ya Televisheni Duniani... Kumbukumbu ya mataifa na nguvu zao laini
Imetafsiriwa na/ Amr Ashraf
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Siku ya Televisheni Duniani haikuwa sherehe ya chombo kama vile ni sherehe ya falsafa iliyooneshwa na chombo hicho, kwani televisheni imekuwa ishara ya mawasiliano na utandawazi kwenye ulimwengu wa kisasa, na nguvu inayodhibiti tabia na maadili ya jamii, na ufahamu wa vijana, utamaduni, mwelekeo wa kisiasa na ushirika wa kiakili, na inaweza kuathiri sana ujuzi wa watoto vibaya na chanya.
Siku ya Televisheni Duniani huadhimishwa mnamo tarehe Novemba 21 kila mwaka, kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa la 51/205 la mwaka 1996, katika kumbukumbu ya Mkutano wa kwanza wa Televisheni Duniani, ambapo viongozi waandamizi wa vyombo vya habari walikutana chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, na kuhimiza ubadilishanaji wa vipindi vya televisheni na maudhui yenye maana ya vyombo vya habari kati ya nchi za dunia, kutoa kipaumbele katika kukuza kubadilishana utamaduni, kukuza ufahamu wa masuala ya amani na usalama, na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Katika tukio hili, ni lazima ieleweke kwamba televisheni ya Misri «Maspero» ni mojawapo ya taasisi kongwe za televisheni ulimwenguni, na hutumika kama shahidi wa enzi, kama ilivyo karibu miaka sitini na moja, baada ya Misri ilikuwa mfano katika uwanja wa redio, ambapo vituo vya redio vya kibinafsi vya Misri vilianzishwa mnamo mwaka 1925, na matangazo ya kwanza rasmi ya redio ya serikali ilizinduliwa na sauti ya redio Ahmed Salem, mmiliki wa maneno maarufu "Hapa Kairo", iliyozinduliwa kupitia kituo cha kwanza cha redio «Radio Heliopolis» mnamo mwaka 1934.
Mnamo mwaka 1959, Kurugenzi Kuu ya Televisheni ilianzishwa na uamuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Utangazaji Na. 2 ya 1959, na mwaka mmoja baadaye, Misri ilisaini mkataba na Shirika la Utangazaji la Amerika (RCA).
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy