Ozoni kwa ajili ya maisha... Chini ya kauli mbiu hii, Umoja wa Mataifa wadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni
Imetafsiriwa na/ Gerges Nagy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Leo, Septemba 16, Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni, na Mkutano Mkuu umeteua siku hii mnamo mwaka 1994, kusherehekea tarehe ya kusaini Itifaki ya Montreal kuhusu vitu vinavyopunguza Tabaka la Ozoni mnamo mwaka 1987, na itifaki hii ilianzishwa chini ya Mkataba wa Vienna uliopitishwa na serikali za ulimwengu mnamo mwaka 1985 kama jibu la uamuzi kwa ulinzi wa tabaka la ozoni.
Madhumuni ya msingi ya Itifaki ya Montreal, ambayo zaidi ya Mataifa ya 190 ni saini, ni kuchukua hatua za kudhibiti uzalishaji wa kimataifa na matumizi ya jumla ya vitu vya ozoni, wakati wa kutafuta kuondoa vitu hivi kupitia maendeleo ya maarifa mbadala ya kisayansi na teknolojia.
Ratiba ya awamu ya HCFCs mnamo mwaka 1992 iliwasilishwa kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea kwa lengo la kufungia kabisa mzunguko wa HCFCs mnamo mwaka 2015 na awamu ya mwisho kufikia mwaka 2030 katika nchi zilizoendelea na kufikia mwaka 2040 katika nchi zinazoendelea. Kwa kweli, kulikuwa na maendeleo makubwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Montreal katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea, na ratiba zote zilikuwa zimezingatiwa na wakati mwingine hata kabla ya ratiba.
Tabaka la ozoni ni ngao tete ya gesi inayoilinda dunia dhidi ya sehemu hatari ya miale ya jua, na kusaidia kuendeleza maisha katika sayari
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy