Waziri wa Michezo ashuhudia mikutano ya kwanza ya Shirikisho la kimataifa la Wachezaji wa Olimpiki wa Afrika nchini Misri

Waziri wa Michezo ashuhudia mikutano ya kwanza ya Shirikisho la kimataifa la Wachezaji wa Olimpiki wa Afrika nchini Misri

 Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy amehudhuria mikutano ya Shirikisho la kimataifa la Wachezaji wa Michezo ya Olimpiki wa Afrika kwa Mahudhurio ya nchi wanachama 25 kutoka bara la Afrika katika Shirikisho hilo linalojumuisha nchi 150 Duniani kote, na yanayofanyika ili kujadili mipango inayotekelezwa katika nchi za Afrika kwa ajili ya kuwahudumia wachezaji wa michezo ya Olimpiki na mipango inayopendekezwa na baadhi ya nchi kwa wachezaji wa michezo ya Olimpiki mnamo kipindi kijacho.

Matukio hayo yamejiri kwa kuhudhuria kwa Bwana Jowal Bozo, Mwenyekiti wa Shirikisho la wachezaji wa michezo ya Olimpiki Duniani, Dkt. Hassan Mostafa, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, Mustafa Biraf, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA), Mhandisi Hisham Hatab, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, Mhandisi Sherif El-Erian, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kisasa la Pentathlon la Misri (UIPM) na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, Dkt. Ehab Amin, Mwenyekiti wa Shirikisho la Sarakasi la Misri, Mamdouh El Sheshtawy, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, na kundi la wachezaji wa Olimpiki wa Wamisri na Waafrika.

Katika hotuba yake, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliwakaribisha waliohudhuria, akielezea furaha yake ya kuwepo kwake katika mkutano huo mkubwa wa kuwahudumia wachezaji wa michezo ya Olimpiki Barani Afrika, akionesha nia yake ya kuimarisha Ushirikiano kati ya nchi zote za bara hilo ili kuendeleza michezo ya Kiafrika kwa kuzingatia mwelekeo wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kuimarisha Ushirikiano na uratibu endelevu pamoja na nchi za bara la Afrika katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na Michezo na Vijana.

Waziri huyo aliashiria kuwa kufanyika kwa Kongamano hilo kwa mara ya kwanza Barani Afrika haswa nchini Misri na kuhudhuria kwa riadha kwa kipekee kwa wawakilishi 50 wa nchi zinazoshiriki tukio hilo kwa sababu ya uandaaji wa Misri wa matukio mbalimbali ya michezo, matukio na mashindano, na msisitizo juu ya jukumu kuu la Misri katika michezo katika kipindi cha sasa, kinachoshuhudia uandaaji wa Misri na mwenyeji wake wa mashindano na mikutano mingi ya kimataifa ya michezo.

Shirikisho la Kimataifa la Wachezaji wa Olimpiki wa Afrika limewatunuku Waziri wa Vijana na Michezo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, mwenyekiti wa ANOCA, viongozi wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, na wachezaji wa michezo ya Olimpiki ya Wamisri na Waafrika. pia Shirikisho hilo lilimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri kwa kile mchezo wa Misri ulichokishuhudia kwa utofauti, maendeleo na kiwango cha hali ya juu, aliyeishuhudia mwenyewe wakati akiwa nchini Misri hivi karibuni.