Waziri wa Umwagiliaji wa Misri na mwenzake wa Sudan Kusini wahudhuria kutimiza kozi ya " Taasisi ya kitaifa kwa Tafiti za Maji "

Waziri wa Umwagiliaji wa Misri na mwenzake wa Sudan Kusini wahudhuria kutimiza kozi ya " Taasisi ya kitaifa kwa Tafiti za Maji "
Waziri wa Umwagiliaji wa Misri na mwenzake wa Sudan Kusini wahudhuria kutimiza kozi ya " Taasisi ya kitaifa kwa Tafiti za Maji "
Waziri wa Umwagiliaji wa Misri na mwenzake wa Sudan Kusini wahudhuria kutimiza kozi ya " Taasisi ya kitaifa kwa Tafiti za Maji "

Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji iliandaa mafunzo yaliyopewa jina la “Maendeleo Endelevu.. Uhusiano kati ya Maji, Chakula na Nishati”katika Kituo cha kitaifa cha tafiti za Maji, Kwa ushiriki wa wanafunzi 30 kutoka nchi 18 za Afrika.

Ijumaa, Wizara ya Umwagiliaji  katika taarifa  ilisema kwamba washiriki walioshiriki mafunzo hayo wanatoka (Sudan - Sudan Kusini - Tanzania - Rwanda - Congo ya Kidemokrasia- Mali - Malawi - Ghana - Burkina Faso - Sierra Leone - Camerun. - Nigeria - Comoro - Chad - Mauritius - Djibouti - Zambia - Liberia).

Kozi hiyo ya mafunzo inalenga kuelimisha watafiti na wataalamu kutoka bara la Afrika umuhimu wa uhusiano kati ya Maji, Chakula na Nishati. Ili kufikia uendelevu wa miradi ya kilimo kwa kuzingatia uhaba wa Maji, na utoaji wa Chakula na Nishati, yatakayoonekana katika kuinua kiwango cha maisha ya wananchi na kukabiliana na changamoto zinazolikabili bara la Afrika.

Mpango huo wa mafunzo hayo ulijumuisha ziara kadhaa, kama vile kutembelea maabara kuu za ufuatiliaji wa mazingira katika kituo hicho, na miundo ya Hydraulics inayotekelezwa katika Taasisi ya Utafiti wa Hydraulics, na Kitengo cha Uondoaji chumvi kwenye Maji kinachotekelezwa na Kitengo cha Utafiti wa Kimkakati, Maabara za taasisi za ujenzi na mazingira katika kituo hicho, na Mifano zinazotumiwa katika taasisi ya utafiti wa mabadiliko ya hali ya hewa, na kituo cha utafiti cha kituo hicho huko Wadi El Natroun. na Uzoefu wa ukarabati wa mifereji na mifumo ya kisasa ya umwagiliaji inayotekelezwa ndani ya kituo.

Dokta Mohamed Abdel-Aty, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, na mwenzake Manawa Peter, Waziri wa Umwagiliaji wa Sudan Kusini, waliwapa wahitimu 30 vyeti vya kuhitimu kozi hiyo.

Wanafunzi waafrika: Misri ni nchi mashuhuri katika usimamizi wa Maji na sayansi za Umwagiliaji na inafanya juhudi kubwa kukabiliana na changamoto.

Wanafunzi waafrika, waliomaliza mafunzo ya "Maendeleo Endelevu.. Uhusiano kati ya Maji, Chakula na Nishati", katika Kituo cha Taifa cha Tafiti za Maji, walielezea furaha yao kwa kuwepo kwao nchini Misri, na kushiriki katika programu hiyo, na nyenzo muhimu za kisayansi zinazopatikana katika mafunzo.

Washiriki wa mafunzo hayo walisifu kituo cha mafunzo ya Hydraulics na uwezo wake wa mafunzo na Logistics, wakielezea kufurahishwa kwao na ziara za miradi ya Rasiliamali za maji.

Walisisitiza kuwa Misri ni miongoni mwa nchi mashuhuri katika uwanja wa usimamizi wa Maji na Sayansi za umwagiliaji, na inafanya juhudi kubwa kukabiliana na changamoto ya maji inayoikabili. na kuna haja ya kuboresha mchakato wa usimamizi wa Maji katika Barani Afrika.

Wanafunzi hao waafrika walieleza kuwa kozi hiyo ya mafunzo ilikuwa na nafasi katika kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa nchi za Afrika zinazoshiriki katika mafunzo hayo, na kubadilishana uzoefu na mawazo kati yao, na Wakisisitiza nia yao ya kutumia uzoefu waliopata kutokana na programu hiyo katika kusimamia Rasiliamali za Maji nchini mwao.