Udhibiti na Utawala iasaini itifaki ya Ushirikiano na Wizara ya Huduma ya Umma ya Sudan Kusini 

Udhibiti na Utawala iasaini itifaki ya Ushirikiano na Wizara ya Huduma ya Umma ya Sudan Kusini 

Dkt Saleh Al Sheikh, Mkuu wa taasisi kuu ya Udhibiti na Utawala , Bwana Bingasi Joseph Bakasoro Waziri wa Huduma ya Umma na Maendeleo ya Rasiliamali za Watu katika Jamhuri ya Sudan Kusini walitia saini itifaki ili kumarisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili , katika nyanja za utawala , Kazi za Umma na huduma ya kiraia , hivyo katika makao makuu ya Shirika hilo katika  mji mkuu wa utawala mbele ya Josef mum Balozi wa Jamhuri ya Sudan Kusini mjini Kairo.

Itifaki hiyo hujumuisha kuimarisha ushirikiano na kubadilisha uzoefu na kunufaika na jaribio wa wakala katika nyanja kadhaa, pamoja na urekabishaji wa taasisi za serekali utayarishaji wa Sheria zinazohusiana na Huduma ya kiraia na utayarishaji wa kadi za maelezo ya kazi na upangaji na nguvu kazi, viwango vya utendaji pamoja na utayarishaji wa kanuni za mwenendo na kuweka vigezo vya utawala vya uteuzi kazi za umma .

Nyanja za Ushirikiano kati ya pande hizo mbili zilijumuisha kutathmini uwezo wa wafanyakazi ya umma, vile vile uwezo wa viongozi katika vyombo vya utawala vya serekali ,huko wakitoa mafunzo kwa baadhi ya watendaji hao kada katika vituo vya mafunzo vya wakala kuu wa Udhibiti na Utawala katika Jamhuri ya kiarabu ya Misri,pamoja na maombi ya kielektroniki kuhusu maswala ya wanafanya kazi wa umma na kubadilisha uzoefu katika vigezo vya ithibati ya vituo vya mafunzo vya serekali na kibinafsi vinavyohusika na taasisi za serekali .

Ikumbukwe kuwa ziara ya ujumbe wa Jamhuri  ya Sudan Kusini nchini Misri kuanzia 7 hadi 11 Machi ilikuja kulingana na mwaliko wa wakala kuu kwa Udhibiti na Utawala , na mazungumzo yamejumuisha juhudi za kimisri katika nyanja za mageuzi ya kiutawala na wajumbe wametembelea kituo cha mashindano na kutathmini uwezo wa mamlaka ili kujionea shuguli za kituo hicho, pia walitembelea mji mkuu wa utawala ambapo alikagua Mtaa wa serikali , walitembelea Msikiti wa Al Fattah Al Alim na Kanisa kuu la " Yesu" na Chuo Kikuu cha Coventry. 

Ujumbe umesifu mafanikio yanayofanyikwa na Misri, na maendeleo inayoyashuhudia katika nyanja mbalimbali .

Hiyo ni mfano wa kuigiwa Barani Afrika, na walieleza nia yao kunufaika kwa jaribio na uzoefu ya kimisri,walisema kwamba ni jaribio la Upainia na linathibitisha uwezo wa nchi za kiafrika  kufikia Maendeleo zikitegemea uwezo wao wenyewe .