Chuo cha kitaifa cha Tafiti za Falaki na Jiofizikia chapokea ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Chuo cha kitaifa cha Tafiti za Falaki na Jiofizikia chapokea ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Waziri wa Elimu ya juu na Utafiti wa Sayansi Dkt, "Khaled Abd Elghaffar" alipokea ripoti kutoka Mkuu wa chuo cha kitaifa cha Tafiti za Falaki na Jiofizikia Dkt, "Gad Alqady" kuhusu mapokezi ya  ya ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaojumuisha mkurugenzi wa kituo cha uchunguzi wa Volkano cha Goma na mkuu wa sehemu ya Tetemeko la ardhi; ili kujadili hatua za kuimarisha Ushirikiano wa pamoja baina ya nchi hizo mbili, kwa mahudhurio ya wakuu na wawakilishi wa sehemu za kisayansi za Chuo.

Ripoti imeelezea kwamba ujumbe wa Congo umekuja; ili kujua uwezo wa utafiti unaopatikana na kujadili kuimarisha nafasi za ushirikiano wa pamoja kwa kuzingatia changamoto zinazokabili eneo la Goma; kama Tetemeko la ardhi na mlipuko wa mara kwa mara wa volkano mnamo mwaka jana.

Kwa upande wake Dkt, "Gad Alqady"  alikaribisha    kushirikiana na ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akisisitiza kuwa chuo kinatoa umuhimu mkubwa wa kushirikiana na nchi za kiafrika, na kutoa kila msaada kwa ushirikiano wa aina hiyo; kwa ajili ya kuendeleza viwango vya mitandao ya ufuatiliaji barani  na kufaidi kutoka uwezo mkubwa barani, akisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi; ili kutathmini nafasi zaidi ya elimu na mchango wake katika mchakato wa maendeleo endelevu.

Pembezoni mwa ziara hiyo, mkutano ulifanywa kwa ushiriki wa wenyeji, Balozi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mjini Kairo, Wizara ya mambo ya nje ya Misri, mamlaka ya ufadhili ya Ttafiti, Teknolojia na Uvumbuzi, chuo cha utafiti wa sayansi na teknolojia, sekta ya maji ya Mto Nile katika wizara ya Umwagiliaji,

Wataalamu wa taasisi hiyo, ambapo juhudi za maonesho zilionyeshwa; ili kuzuia hatari za majanga ya asili barani Afrika kupitia miradi ya utafiti na ushirikiano wa chuo cha kimataifa, na juu yake mradi wa sababu za Tetemeko la ardhi katika bonde la Nile kwa kushirikiana na washiriki wa chuo katika bonde la Nile; kwa lengo la kuanzisha mitandao ya ufuatiliaji wa mazingira katika Barani Afrika.

Mwenyekiti wa mamlaka ya ufadhili wa Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi Dkt, " Walaa" aliashiria umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiafrika, akielezea kuwa mamlaka inafadhili miradi ya kuunda uwezo katika chuo cha kitaifa cha Tafiti za Falaki na Jiofizikia, kama nyumba ya uzoefu wa kitaifa katika uwanja wa ufuatiliaji wa hatari za asili na kupunguza athari zake, na ni moja ya chuo cha utafiti wa kimataifa katika uwanja wa ufuatiliaji wa Tetemeko la  ardhi na pia mahusiano makubwa ya chuo pamoja na Uchunguzi tofauti na mashirika mengine ya utafiti katika viwango viwili vya kikanda na kimataifa. 

Makamu wa Mkuu wa Shirika la Afrika kwa Ushirikiano, Balozi " Karim Amin" alisisitiza nia ya shirika hilo kwa kuongeza fursa za ushirikiano na Congo, ilionyesha matukio ya Volkano na Tetemeko la ardhi zinazotokana na mlipuko wa Volkano vya Nyiragongo katika eneo la Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo karibu na mipaka ya Rwanda katika siku ya Mei 22 , mwaka wa 2021, Mlipuko wa volkano uliambatana na Tetemeko la ardhi; kutokana na harakati za lava kwenye volkano, na hiyo ilisabibisha ueneaji wa lava karibu na eneo la volkano,  inayosabibisha tishio kubwa kwa watu na mali katika eneo hilo. 

Balozi mdogo mjini Kairo  " Lillian" alisisitiza umuhimu wa kupata msaada wa Misri kwa ufuatiliaji wa volkano wa Goma kwa Nafasi, vifaa, kozi za mafunzo na programu za kuunda uwezo; ili kuimarisha uwezo wake wa kutekeleza mchango wake katika onyo la mapema la mlipuko wa volkano.

Maafisa wa chuo cha kitaifa cha Tafiti za Falaki na Jiofizikia walikaribisha utoaji wa msaada kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Rwanda na kuziongeza kwa vituo kadhaa vya ufuatiliaji wa Tetemeko la ardhi na sauti ya ndani na idadi ya 

wataalamu wa kiufundi; ili kufanya kazi ya kufuatilia na wenzao na kuwahimiza maafisa watendaji kwa taarifa za kiufundi.