Fahamu historia yako utajijue mwenyewe ili Utu ujitukuze na historia iishi

Fahamu historia yako utajijue mwenyewe ili Utu ujitukuze na historia iishi

Imefasiriwa na  /  Ali Mahmoud

Imeandikwa na / Mohamed Ashraf

Katika tukio la maadhimisho ya miaka milenia ya Kairo mnamo Mwaka wa 1969 Kiongozi Gamal Abdel Nasser, kabla ya kifo chake kwa mwaka mmoja, alizindua sherehe inayofaa maadhimisho ya kuanzishwa kwa jiji hili la kihistoria liwe ushahidi wa ukuu wake na fahari yake mwaka baada ya mwaka, na uwe uzinduzi huu kama kuimarisha kila mwaka kwa athari yake ya fasihi, kiutamaduni, kijamii na kihistoria katika ngazi za kiarabu, kikanda na kimataifa..

Kwa kweli, sherehe halisi ilikuwa ni kupita kwa miaka elfu tangu Kairo kupewa jina hili na Jawhar Al-Sicily katika Mwaka wa 969 , na umri wa Kairo hutangulia tarehe hii kwa karne kadhaa, lakini kwa majina mengine.

Abdel Nasser alitaka maadhimisho ya Milenia ya kuanzishwa kwa Kairo sambamba na uzinduzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Kairo ya Kitabu kama maonesho makubwa zaidi ya Kitabu katika Mashariki ya Kati katika Eneo la Maonesho katika mji wa Nasr, mashariki ya Kairo, ili lifanyike toleo la kwanza mnamo Mwaka wa 1969 na kuendelea kila Mwaka hadi leo.

Sasa tuko katika muongo wa tatu wa Karne ya Ishirini na Moja, na baada ya vitongoji vya Kairo kubwa, mitaa na viunga vyake vimepunguza ustaarabu mwingi wa Mashariki na Magharibi katika historia yake ndefu, maonesho ya Kitabu peke yake hayatoshi tena kuimarisha nafasi hii ya kifasihi na ya kihistoria ya Kairo, na nadhani kuwa tunapaswa kufufua historia yake katika hisia za wakaaji wake, kwanza na kisha wageni wake, jiji kama Kairo ni kama jiji linaloelea juu ya historia, lilijumuisha ndani yake utaratibu na mfululizo wa kistaarabu ambao hauna kifani ulimwenguni na bado unashuhudiwa kila mahali Kairo hadi leo, kati ya Kairo ya kifarao, ya kigiriki, ya kirumi, ya kipersia, ya kiyahudi, ya kikoptiki, ya kikatoliki, ya kiislamu, ya kiumayya, ya kiabbasi, ya kifatimi, ya kiayubia, ya ki-tuluni, ya ki-mamluki, ya ki-otoman, ya ki-alawi, ya ki-khedive, ya ki-yunani, ya ki-nasiriyah...

Je, hii haitoshi kufanya kazi ya kuunda upya historia hii katika picha rahisi kama ishara kwenye mitaa yake na viwanja vyake zikisimulia hadithi za sababu ya kuita mitaa hii, vitongoji na viwanja na matukio muhimu zaidi ambayo ilishuhudia..
Ninasikitika sana ninapomuuliza askari mpya ambaye anaishi mbele ya Msikiti wa Al-Zahir Baibars, kuhusu Al-Zahir Baibars ni nani na hajibu..

Inanisikitisha sana ninapomuuliza mkazi mwingine wa Mtaa wa Yusuf Abbas kuhusu Yusuf Abbas ni nani na yeye hajibu.
Ninasikitika sana ninapomuuliza askari anayeishi katika eneo la Bab Al-shaariya au Ain Al-Sira, au au, au

Unaona faida gani kwa muda mfupi na mrefu kwa gharama nafuu ya kuweka mabango hayo kando ya matangazo yanayoenea barabarani?

Na watu wangapi watakuwa katika Maonesho ya Kitabu wanapojua na kujifunza mali hizi kutoka kwa mabango

Na serikali itapatia faida kiasi gani leo na baadaye kwa sababu ya ujuzi wa watu kwa nafsi zao wenyewe, urithi wao Na kujishughulish nao bila kuwepo kwa mdhibiti wa kimabavu…

Fahamu historia yako, ujijue mwenyewe, ili Utu ujitukuze na historia iishi…