Salima Mukansanga... Mwanamke wa Kwanza kuwa Refa katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika

Salima Mukansanga... Mwanamke wa Kwanza kuwa Refa katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika

 

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky

Salima Mukansanga ni Refa wa kimataifa wa mpira wa miguu, alizaliwa nchini Rwanda mwaka 1998, ambaye alikulia katika wilaya ya "Rusizi" Mkoa wa Magharibi, na kupata shahada ya kwanza katika  uuguzi na ukunga kutoka Chuo Kikuu cha "Gitwe" kilichoko katika jimbo la kusini la Ruhango, Rwanda.

 Hapo awali, alipokuwa mwanafunzi shuleni, alitamani kuwa mchezaji wa mpira wa kikapu, lakini hakuweza kufikia ndoto yake wakati huo kutokana na vikwazo katika njia yake, kama vile ukosefu wa mahitaji ya msingi ya mchezo huu, ikiwa ni pamoja na vifaa vya mpira wa kikapu.

Licha ya hayo yote, hakukata tamaa, lakini alielekeza umakini wake kwa mpira wa miguu, na mnamo mwaka wake wa mwisho katika Shule ya Upili ya St Vincent de Paul Musanze, aliongoza mechi ya mwisho ya mashindano ya shule, na hapa njia yake ya kuwa Refa wa mpira wa miguu ilianza.

 Mwaka mmoja baadaye, alikuwa amemaliza shule na kujifunza misingi ya Urefaji kupitia mafunzo yake ya mahakama na kupata cheti cha kuwa mwamuzi mwaka 2008, hivyo alianza kupanda ngazi ya mafanikio hatua kwa hatua huku akichukua daraja la pili la wanaume, na  daraja la kwanza kwa wanawake, kisha ikaibuka kidedea baada ya miaka minne, yaani mwaka 2012, alipandishwa cheo na kuwa mwamuzi mwenye leseni ya "CAF", na wakati huo mlango ukafunguliwa na kuanza kusimamia mechi zote Barani Afrika, na hii ilitokea alipochukua nafasi ya Refa msaidizi.

Pia, mnamo 2014, alipewa Refa wa kati, ambayo ilikuwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo wakati wa pambano la ubingwa wa Afrika kwa Wanawake huko "CAF" kati ya Zambia na Tanzania, Baada ya mechi ya Zambia dhidi ya Tanzania, Mukansanga alipandishwa cheo na kucheza mechi za kimataifa, Kazi yake ya kwanza ilikuwa kwenye Michezo ya Afrika mwaka 2015 iliyofanyika Brazzaville, Jamhuri ya Congo, hasa mechi ya ufunguzi kati ya Nigeria na Tanzania, na kisha kuhusika na nusu fainali kati ya Ghana na Ivory Coast.

Baada ya michuano hayo, alirejea Uganda na kuongoza  Kombe la mashindano kwa Wanawake ya CAF 2015 huko Jinja, Uganda.

Mukansanga aliendelea kupanda, na mwaka wa 2016, alikuwa miongoni mwa maafisa 47 waliosimamia Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake nchini Cameroon, akitawala fainali kati ya Cameroon na Nigeria.

Uchezaji wake nchini Cameroon ulimfanya kusimamia Kombe la Dunia la Wanawake U-17 nchini Uruguay mwaka wa 2018 na alichukua jukumu la Kundi A kati ya Uruguay na New Zealand.

Mukansanga pia alikuwa afisa katika Kombe la Dunia la Wanawake la 2019 nchini Ufaransa, na wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon mnamo 2022 aliteuliwa kuwa Refa mkuu  kama mwanamke wa kwanza Barani kushika nafasi hiyo, na Mukansanga alitumia fursa hiyo na kufanya kampeni ya uteuzi wa wanawake zaidi kwa Refa mkuu.

 Salima Mokansanga alishinda tuzo ya FORBES Woman Africa Award 2023, wakati wa Mkutano huo FORBES Women Africa Lead Women iliyofanyika Pretoria, Afrika Kusini katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8.

Salima Mokensanga sio tu mwanamke anayedhibiti katika Kombe la Mataifa ya Afrika, bali ni mfano hai wa kuwahamasisha wanawake wengine kufikia ndoto zao na kufungua milango ya azma yao.

Chanzo

Africa-women-experts