Mapinduzi ya Julai 23.... Kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kwanza

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky
Mapinduzi ya Julai 23 ni mabadiliko makubwa katika historia ya taifa hilo kwa sababu ya mafanikio makubwa yasiyo na kifani katika nyanja nyingi (Kisiasa, kiutamaduni, kielimu, kiuchumi na kijamii) Mafanikio ya mapinduzi hayakuishia katika nyanja hizo pekee, bali pia yalipata mafanikio yasiyoweza kusahaulika katika ngazi ya kiarabu na kimataifa.
Mafanikio muhimu zaidi kati ya hayo yalikuwa ni kutangazwa kwa Jamhuri na kuteuliwa kwa Jenerali Muhammad Naguib kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Misri mnamo Juni 18, 1953.
Lakini kabla ya kuzungumzia mafanikio hayo ni muhimu kutambua asili ya mapinduzi na kushughulikia sababu za kuanzishwa kwake na kanuni zake muhimu zaidi:
Mapinduzi ya Julai ni harakati ya kijeshi iliyofanywa na viongozi wa maafisa wa jeshi ambao walijiita Taasisi ya Maafisa Huru, ili kupindua utawala wa kifalme wakati huo, kwa sababu kadhaa: hali mbaya ya kiuchumi ya nchi na kupoteza haki ya kijamii kati ya tabaka za watu kwa sababu ya mgawanyiko mbaya wa mali, na shule za bahari na kijeshi zilifungwa, pamoja na hali mbaya ya kisiasa na utawala, iliyowakilishwa na ujinga wa Mfalme na wafuasi wake kutojali haki ya wengi na kuegemea upande wa vyama vya wachache.
Sababu kuu ni kufanyikwa Vita vya Palestina bila maandalizi ya kutosha, hivyo kushindwa kukamilika na Palestina ilipotea katikati ya silaha za rushwa, Sababu hizo zilisababisha kuibuka kwa Taasisi ya Maafisa Huru katika jeshi la Misri kwa uongozi wa Gamal Abdel Nasser pamoja na Misingi sita ndiyo ilikuwa mhimili mkuu wa sera ya mapinduzi, ambayo ni kuondoa mfumo wa ukabaila, mtaji na ukoloni, ujenzi wa maisha bora ya kidemokrasia, ujenzi wa jeshi imara la taifa na uadilifu wa kijamii.
Mapinduzi yalizukwa na kusababisha mafanikio yasiyo na kifani katika nyanja nyingi, ambazo baadhi yake zinaweza kutajwa kwa ufupi.
Katika uwanja wa kisiasa, Mfereji wa Suez ulitaifishwa na makubaliano ya uhamishaji yalitiwa saini kwa uvamizi uliodumu kwa zaidi ya miaka 70. Na kuudhibiti utawala wa Misri baada ya kuanguka utawala wa kifalme na kumlazimisha Mfalme Farouk kuacha kiti cha enzi, na utawala wa kifalme ukafutwa, jambo lililopelekea kuanzishwa mfumo wa Jamhuri na kuteuliwa Muhammad Naguib kuwa Rais wa kwanza wa mfumo huo.
Katika uwanja wa elimu, mafanikio yaliwakilishwa katika uanzishaji wa vituo vya utafiti na ujenzi wa vyuo vikuu kumi badala ya vitatu tu, na kuidhinishwa kwa elimu bure ya umma na ya juu, pamoja na kuongeza maradufu bajeti ya elimu ya juu.
Upande wa kiutamaduni wakati huo pia ulipata bahati nzuri kutokana na mafanikio ya mapinduzi,Chuo kilianzishwa ambacho kilijumuisha taasisi za sinema, jukwaa , balle na muziki, na kazi ya kufadhili mambo ya kale na makumbusho, Filamu pia zilitolewa kulingana na hadithi za fasihi halisi ya Misri.
Ama kuhusu mafanikio ya kiuchumi na kijamii, mapinduzi hayo yanazingatiwa kuwa zama za dhahabu za tabaka la wafanyakazi, ambalo wakati huo liliitwa tabaka lililokandamizwa kutokana na lilivyoteseka kwa miaka mingi ya dhulma na ukosefu wa haki, Mapinduzi hayo yalisababisha mwelekeo wake wa kijamii na uondoaji wake wa mfumo wa ukabaila, kukomeshwa kwa tabaka za kijamii miongoni mwa watu wa Misri, na kuondoa ubepari na udhibiti wake juu ya uwanja wa kilimo na viwanda.
Mafanikio ya mapinduzi katika ngazi ya Kiarabu yaliwakilishwa katika umoja wa juhudi za Waarabu kuelekea harakati za ukombozi, pia ilianzisha uzoefu wa Waarabu katika Umoja kati ya Misri na Syria, mnamo Februari 1958, pamoja na kutia saini makubaliano ya pande tatu kati ya Misri, Saudi Arabia na Syria, ambapo Yemen ilijiunga. Pia ilichangia uhuru wa Kuwait na kutetea haki ya Somalia na harakati ya kujitolea kwa maamuzi na kuunga mkono uhuru wa Morocco, Somalia na Tunisia..
Miongoni mwa manufaa ya mapinduzi hayo ukilingalisha na mengine ni kuwa yalikuwa ni mapinduzi ya kizungu, yaani hayakumwaga damu, yalileta kizazi kipya cha maafisa na vijana wakiongozwa na Gamal Abdel Nasser,tena yalikuwa na sera ya kutofungamana kwa upande wowote, basi yakapata uungaji mkono mkubwa sana na wakulima na matabaka ya kawaida ya wafanyikazi, pia yalisababisha Umoja na Syria na Yemen.
Mapinduzi ya Julai hayakuwa tu mapinduzi, bali yalikuwa ni kielelezo tosha cha mshikamano wa watu na jeshi chini ya lengo moja, ambalo ni marekebisho, Lilikuwa jina la kurudisha heshima ya nchi na nchi, kudumisha maslahi ya nchi, kufikia uhuru wake, kujitawala, na mwelekeo wa kuwa bora.