Kiswahili na Siku yake Duniani

Imeandikwa na / Fatma Mahmoud
Umoja wa Mataifa umeamua kuainisha tarehe 7 mwezi wa Julai ya kila mwaka ili kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyoenea katika maeneo ya pwani za Afrika Mashariki , na inazingatiwa kama lugha ya mawasiliano ya pamoja kati ya nchi za Afrika Mashariki, tena ni miongoni mwa lugha zilizoidhinishwa na Umoja wa Afrika, na nchi zinazozungumza Kiswahili ni kama (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia, Comoro, Zambia, Madagascar, Msumbiji, Malawi na Oman).
Kwa upande wa Idadi ya wazungumzaji wa Kiswahili, idadi yao inatofautiana kutoka watu milioni 50 hadi zaidi ya milioni 200, pamoja na hayo Kiswahili ilipata misamiati yake mingi kutoka kwa lugha nyingine kama Kiarabu na Sanskrit, na hiyo kutokana na kuwasiliana na wafanyabiashara Wahindi na Waarabu kwenye pwani za Kusini-mashariki mwa Afrika, tena Kiswahili iliandikwa kwa maandishi ya Kiarabu zamani, lakini sasa yaandikwa kwa herufi za Kilatini.
Lingine, Umuhimu wa kueneza zaidi lugha ya Kiswahili kati ya watu Barani Afrika unajitokeza kutokana na ukweli wa kwamba ni njia mojawapo ya kuimarisha utambulisho wa Mwafrika, na tayari juhudi za kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya Afrika zima zilianzishwa na Julius Nyerere tangu miaka ya 1960 - Rais wa kwanza wa Tanzania baada ya Uhuru- ambaye alitumia lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuwaunganisha watu wa nchi yake baada ya kupata Uhuru kutoka kwa ukoloni wa Uingereza.
Aidha , Kiswahili mnamo 2019 likawa lugha pekee ya Kiafrika inayotambuliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia pia kilitangaza hivi karibuni kwamba kitaanza kufundisha Kiswahili na bila ya kusahau mchango wa Misri katika kueneza lugha za Kiafrika, ikiwemo Kiswahili; ambapo Sehemu ya kufundisha Lugha za Kiafrika ilianzishwa tangu 1967 katika Kitivo cha Lugha na Tafsiri, Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na baada ya hapo Vyuo Vikuu vingi vya Misri vilianza kuifundisha, kama vile Chuo Kikuu cha Kairo, Ain Shams ,na Chuo Kikuu cha Aswan; Hilo ni kutokana na umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika kuimarisha utambulisho wa Mwafrika na mahusiano ya pamoja kati ya nchi za bara la Afrika .