Dkt. Suhayr Al-Qalamawi.. Bibi wa Kitabu na mwanamke Mmisri wa kwanza apataye Uzamivu

Dkt. Suhayr Al-Qalamawi.. Bibi wa Kitabu na mwanamke Mmisri wa kwanza apataye Uzamivu

Imefasiriwa na / Osama Mostafa Mahmoud

Ikiwa wewe ni mmoja wa wageni  wa Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo, utaona bango lenye jina lake, kwa kuwa yeye ni mmoja wa waanzilishi wake... lakini je, unafahamu yeye ni nani haswa? Kila mpenzi hutafuta maelezo ya mpendwa wake; awe kielelezo kwake na mmoja wa wale wanaotembea katika njia ya mafanikio yake.. Naye ni Prof. Suhayr Al-Qalamawi, aliyependa Tiba , na alitamani kuwa daktari kama baba yake, ila hatima imfikishe mazuri zaidi na kuwa msichana wa kwanza kujiunga na Kitivo cha Sanaa, Idara ya Lugha ya Kiarabu, na ndiye pekee kati ya vijana wenzake kumi na wanne waliofanya vizuri, ndio maana Taha Hussein, Mkuu wa Fasihi ya Kiarabu na Mkuu wa Chuo Kikuu wakati huo alimzingatia sana... Si hivyo tu, ila yeye ni mwanamke mmisri wa kwanza apataye ruhusa ya uandishi wa habari nchini Misri, ili kuandika makala zake kwenye magazeti ya "Al-Latif Al- Musawara" na "Al-Arus", na wakati wa masomo yake ya chuo kikuu amepata Uzamivu katika fasihi, kwa hivyo akawa mwanamke wa kwanza kufikia hilo.

Suhayr Al-Qalamawi amezaliwa  mnamo Julai 1911, kwa baba anayefanya kazi kama daktari katika jiji la Tanta na mama wa Circassian.Alikulia katika familia iliyojivunia kuwasomesha wasichana wake, na alijiunga na Shule ya Wasichana ya Marekani. hapo. Suhayr alipenda kusoma na kusoma tangu akiwa mdogo, na baba yake alikuwa na maktaba kubwa ambapo aliweza kufaidika na kazi za fasihi katika umri mdogo.Waandishi kama vile Dkt.Taha Hussein, mwanzilishi wa shule ya kutafsiri, Rifa'a Al- Tahtawi, na Ibn Iyas walichangia pakubwa katika talanta yake ya fasihi na wakaunda sauti yake kama mwandishi, hiyo ndiyo iliyoboresha maisha yake kimaandishi baadaye.

Suhayr alitaka kusomea Tiba ya binadamu kama baba yake, lakini urasimu wa kiume wakati huo ulikataa kutimiza ndoto yake, kwa hivyo, hajapata ila Kitivo cha Sanaa katika Chuo Kikuu cha Fouad I pekee kuwa msichana wa kwanza kujiunga na Kitivo cha Sanaa, Idara ya lugha ya Kiarabu, na pekee kati ya wenzake kumi na wanne. Al-Qalamawi alishawishiwa na wanawake wa Misri walioshiriki mapinduzi ya 1919, kama vile Safia Zaghloul na Hoda Shaarawy, na hii ilikuwa mara ya kwanza kwa wanawake kushiriki katika mapinduzi, hivyo aliishi katikati ya ushawishi wa wanawake hawa ambao walichukua mijadala ya ufeministi mitaani ili kujenga vuguvugu la mbali. Nia hii iliathiri baadhi ya kanuni zake za ufeministi katika kudai haki za wanawake, kuwatetea, na kuwalinganisha na wanaume, na profesa wake, Dkt. Taha Hussein, alimsaidia kushika nafasi ya mhariri mkuu msaidizi wa Jarida la Chuo Kikuu cha Kairo mnamo 1932, kwa hivyo, Al-Qalamawi akawa mwanamke wa kwanza kufanya kazi ya uandishi wa habari nchini Misri, pamoja na kuongezeka kwa shughuli zake, alifanya kazi kama mtangazaji Kwa huduma ya utangazaji ya redio ya Misri.

Dkt. Suhayr alianza taaluma yake kama mhadhiri wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kairo mnamo 1936 , na akawa mmoja wa watu mahiri katika jamii ya kimisri, haswa baada ya kupata shahada ya uzamili ya fasihi.kisha akasafiri katika ujumbe Kuelekea Ufaransa ili kujiandaa utafiti wa Uzamivu kuhusu " Usiku Elfu Moja na Moja", na kweli akapata shahada ya Uzamivu mnamo 1941, katika tasnifu ya kwanza ya kisayansi iliyohusu. na Usiku Elfu Moja na Moja kwa kuisoma na kuiwasilisha kutoka kwa ngano hadi kazi ya fasihi, na kuwa msichana mmisri wa kwanza kuipata.

Katika mahojiano naye na waandishi wa habari, alipoulizwa kuhusu vyanzo vya kiakili ambayo Suhayr Al-Qalamawi alichomoa na kujifunza mengi kutoka kwake, alisema: "Thamani ya kwanza ninayoikumbuka kutoka kwa Taha Hussein ni ukakamavu, na kama Taha Hussein asingekuwa mwenye nia kali, hangefikia cheo alichofikia, alikuwa akisema kwa sauti yake ya kipekee, yenye mguso.” Kwa nini tutaendelea kuwa dhaifu? Nami nilikuwa nahisi kama yeye ananihimiza kuwa na ujasiri.

Al-Qalamawi akaongeza: “Taha Hussein alikuwa akisema kuwa maisha ni msimamo, mwandishi ni msimamo, na anayefanya kazi kwa fikra ni msimamo, na nilihisi ananiwekea undani wa umuhimu wa kuhisi kushika nafasi. Badala yake, fadhila muhimu zaidi, kwa sababu zinaakisi unyenyekevu pamoja na elimu, nilijifunza maana ya kuzingatia akili yangu, kwa sababu mimi ni kutoka katika kizazi ambacho kilipuuzwa na majitu kama vile Taha Hussein na Lotfy Al-Sayed, na waliamini katika kuwasomesha wasichana, na nilijifunza kutoka kwa Taha Hussein kwamba vyuo vikuu vina hadhi ya hali ya juu, na alikuwa akisema kwamba vyuo vikuu muhimu zaidi vya Ulaya ni vya Makanisa, na waanzilishi wa Misri na ulimwengu wa Kiarabu walisoma misikitini.

Kwa Dkt.Suhayr Al-Qalamawi kusoma ni mapenzi na burudani, muziki ni chakula na habari, na ladha yake ya uimbaji imejikita zaidi kwa Fayrouz na Umm Kulthum, ama kuhusu siasa ana hisia za jamii na matatizo yake rahisi ya kila siku.

Haraka alijipanga kuwa profesa wa chuo kikuu, na kazi zilizofuatana na kufaulu zilihama kutoka digrii za masomo hadi nafasi za uongozi hadi akawa profesa wa fasihi ya Kiarabu ya kisasa mnamo 1956, na akaanza kazi yake ya kisiasa alipojiunga Bunge kama mjumbe mwaka wa 1958 kwa mujibu wa ujuzi wake wa kifasihi na kisayansi miongoni mwa walioteuliwa kutoka kwa Rais Gamal Abdel Nasser, Rais wa Jamhuri wakati huo.

Pia aliwahi kuwa Mkuu wa Shirikisho la Wanawake la Misri, na mnamo mwaka wa 1959 , akawa Mkuu wa Chama cha Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Wanawake wa Kiarabu, ambapo alianzisha Taasisi ya ushirikiano kati ya Shirikisho la Misri na Shirikisho la Dunia la Vyuo vikuu.

Mnamo 1960, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake, na mnamo 1961, akakua Mkuu wa mkutano wa kwanza wa sanaa ya watu, ambapo aliunda kamati ya kusimamia Chuo Kikuu cha Wasichana wa Palestina ili kuzungumzia nia yake katika kesi la Palestina, na hiyo ilikuwa mnamo 1962.

Miongoni mwa nyadhifa alizoshikilia pia ambazo zilikuwa na athari kwa nafasi yake chanya katika jamii ni nafasi ya Mkuu wa Mamlaka Kuu ya Misri ya Sinema, Theatre na Muziki mwaka 1967, na Mkuu wa Idara ya Lugha ya Kiarabu katika Kitivo cha Sanaa, wakati huo, kisha Mkuu wa Jumuiya ya Utamaduni wa Mtoto mnamo 1968.

Dkt. Suhayr Al-Qalamawi alifikiria kuwaelimisha Wamisri kwa kusoma, kwa hivyo alikuwa na mfano wa kwanza wa kuanzisha maktaba katika ukumbi wa Azbakiya Theatre, kuuza vitabu kwa bei nafuu, ili kitabu kifikie hadhira yake wa kawaida, pia alitoa fursa kwa waandishi zaidi ya 60 kuwasilisha vitabu vyao alipotoa mfululizo wa Fasihi "Machapisho Mapya".

Alisimamia "Nyumba ya Vitabu vya Kiarabu" na kisha akasimamia taasisi ya uandishi na uchapishaji kutoka "1967 hadi 1971." Wakati wa Uongozi wake kama mkuu wa Mamlaka ya Vitabu vya Misri, alifanya kazi kupanua anuwai ya wasomaji, kuwatia moyo waandishi wachanga, na. kuendeleza tasnia ya vitabu, haswa mnamo mwaka wa 1967, aliposhiriki Dkt. Suhayr Al-Qalamawi katika kuanzisha maonesho ya kwanza ya vitabu katika Mashariki ya Kati, ambayo ni "Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo", na Rais Gamal Abdel Nasser alimkabidhi kuisimamia ili aweze kuwasilisha sayansi na fasihi kwa Wamisri wote. Alishiriki pia katika uanachama wa Baraza la Umoja wa Waandishi, na alichaguliwa kama mjumbe wa mabaraza maalumu ya Misri.

Dkt. Suhayr aliteuliwa tena kuwa mjumbe katika Bunge la Wananchi kuanzia 1979 hadi 1984, pamoja na kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi kutoka 1982 hadi 1985.

Kutokana na juhudi hizo kubwa, Dkt. Suhayr Al-Qalamawi alishinda tuzo kadhaa, kama vile Tuzo la Chuo cha Lugha ya Kiarabu mwaka wa 1954, Tuzo la Kuthamini Taifa kwa Fasihi ya Vijana, Tuzo la Kuhimizwa kwa Serikali, Tuzo la Kuithamini Serikali kwa Fasihi, Tuzo la Jimbo la Kuthamini Fasihi, na Nishani ya Jamhuri Shahada ya Kwanza, Medali ya Mafanikio, na Shahada ya heshima ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kairo, na mnamo mwaka wa 2008, Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo yalimtangaza Dkt.Suhayr Al-Qalamawi, Mhusika wa Mwaka, na hii ilirudiwa tena katika yubile ya dhahabu ya maonesho, kwa kuthamini jukumu lake kubwa katika kuanzishwa kwake, ambalo linashuhudia mamilioni ya ziara kutoka Duniani kote.

Dkt. Suhayr Al-Qalamawi alifariki Dunia baada ya safari ya mafanikio katika nyanja mbalimbali mnamo mwaka 1997, akiacha  kazi nyingi kama vile; Kitabu "Masimulizi ya Bibi yangu", ambayo ni maarufu zaidi, na historia na kazi zake bado hazijajulikana kwa vizazi wapya, kama vile kazi za "Mashetani Wacheza, Jua Likatua, Simulation katika Fasihi, na Ulimwengu katikati ya Vitabu viwili", pamoja na tafsiri nyingi, zikiwemo: "Hadithi za Kichina za Pearl Bey, na  Mpenzi wa Alwita , Ujumbe wa Abon kwa Plato", na pia alitafsiri tamthilia kumi za mwandishi wa mwingereza William Shakespeare.