Mwongozaji Mwenye Akili "Shadi Abdelsalam"

Imetafsiriwa na/ Amira Roshdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Shadi Abdelsalam anasema: "tangu nilipoanza kufanya kazi, nimekuwa na imani kuwa nina kesi... kesi yangu ni historia iliyopotea au kuwa ya mtu asiyejulikana... watu ambao unawaona mitaani na nyumbani... mashambani na viwandani... wana historia... watu hawa wamekuwa matajiri wa ubinadamu... tunawezaje kuwarejesha kwenye jukumu lile lile. Tunawezaje kurudisha mchango wao wenye nguvu na chanya katika maisha. Lazima kwanza wajue ni akina nani? Na walikuwa nini? Na walitoa nini? Lazima tuunganishe kati ya mwanadamu leo na mwanadamu wa jana ili tuweze kutoa mwanadamu wa kesho... Hii ndiyo kesi yangu."
“Alikuwa mwongozaji wa filamu, mbunifu wa mapambo, mhandisi, na mbunifu wa nguo, kazi zake zilikuwa zinaakisi maono yake ya kipekee ya utamaduni wa Misri wa zamani pamoja na urithi wa Kiislamu na Kikopti. Alikuwa mwanzoni mbunifu wa mapambo, alifanya mapambo na nguo kwa filamu«Al-Nasser Salah al-Din» ya Youssef Chahine, pia alitia alama yake kwenye filamu nyingi za kitamaduni kwa kubuni nguo na mapambo yake katika filamu ambazo alishiriki, ikiwa ni pamoja na «Bayn al-Qasrayn», «Amir al-Dahaa», «Al-Khataaya», «Wa'islaamah», «Rabia al-Adawiyya», «Shafiqa al-Qubtiyya» na zingine.”
Shadi Abdelsalam alifanikiwa kupitia kazi zake kuweka sinema ya Misri kwenye ramani ya sinema ya ulimwengu. Kazi muhimu zaidi ilikuwa filamu ya "Mummy" ambayo ilipata mafanikio makubwa ulimwenguni, na ilipata tuzo nyingi, ikiwemo uteuzi wa Shirika la Kimataifa la Sinema mwaka 2009 kama moja ya filamu muhimu katika historia ya sinema ya ulimwengu, na ilionyeshwa kwenye Tamasha la "Cannes" mwaka huo huo. Mapema mwaka 1970, mwaka ambao filamu ilizalishwa, filamu ya Mummy ilipata tuzo ya "Georges Sadoul" huko Paris, na tuzo ya Tamasha la Carthage. Pia aliunda filamu ya "The sarafu ya mzawa" ambayo ilishinda tuzo ya "Leone d'Oro" huko Venice, na hivyo mkurugenzi huyo mwenye akili aliacha alama yake dhahiri kwenye sinema ya Misri na Kiarabu.
"Mzalendo mwenye vipaji vingi, Shadi Abdelsalam, alizaliwa huko Alexandria mnamo Machi 15, 1930, na alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Victoria huko Alexandria mnamo 1948, kisha akaenda London kupata mafunzo ya sanaa ya maigizo kati ya 1949-1950. Baadaye alihitimu kama mhandisi wa usanifu kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa nzuri huko Cairo kwa heshima mwaka 1955. Kutokana na shauku yake na upendo wa sinema, aliamua kwanza kufanya kazi katika tasnia hiyo, na jukumu lake la kwanza lilikuwa kurekodi muda uliotumiwa katika kila kivuli katika filamu ya "Elftewa" na mwongozaji mkubwa Salah Abu Seif, kisha akafanya kazi kama msaidizi wa Salah Abu Seif katika filamu "Alwesada Alkhalia", "Altariq Almasdud" na "Ana hora". Shadi pia alifanya kazi na mwongozaji mkubwa wa Italia, Rossellini, katika filamu ya "Alhadhara" mnamo 1966, ambaye alikuwa na athari kubwa kwa Shadi Abdelsalam kifikra na hata kiufundi kwa sababu ya kina na urahisi wa mawazo yake ya sinema. Baada ya kuteuliwa kuwa rais wa Kituo cha Filamu cha majaribio kilichokuwa chini ya Wizara ya Utamaduni mnamo 1970, katika kipindi kati ya 1970-1980, Shadi Abdul Salam aliandaa filamu nne za kumbukumbu, akizipatia kama mifano ya shughuli tofauti za kitamaduni nchini Misri."
"Shadi Abdelsalam alifariki mnamo tarehe 8 Oktoba 1986, na Maktaba ya Alexandrian inaonyesha maonyesho maalum na ya thamani ya kazi za Shadi Abdelsalam tangu mwaka 2002 ambayo iliwekwa wakfu kwa maadhimisho ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa Shadi Abdelsalam mwezi Machi 2015, ambayo ina picha nyingi na video zinazochukuliwa kutoka kwa filamu ambazo alishiriki au kutengeneza, pamoja na baadhi ya vitu vyake vya kibinafsi, kama vile vipande vya samani vya ofisi yake na maktaba yake ya kibinafsi, pamoja na ukumbi wa "Aafaq" ambapo filamu ambazo Shadi Abdelsalam alizotengeneza zinaonyeshwa kila siku, zaidi ya hayo, baadhi ya mahojiano ya televisheni ambayo msanii alifanya, na baadhi ya filamu na vipindi ambavyo vinazungumzia maisha yake na kazi zake."
“Ni vyema kufahamisha kuwa "Shadi Abdelsalam" ni moja ya nguzo muhimu na mifano halisi ambayo Mradi wa Bzoor unategemea katika kazi yake, akichukua maono yake kama njia ya kuchunguza kina cha utamaduni wetu wa kibinadamu ambao umepitia kwa binadamu wa Misri na kuweza kuufanya katika sura mpya inayomfaa, hivyo tunatafuta kuondoa pazia juu ya sanaa za Misri ya zamani na desturi za Mafaraoni ambazo hazijateketea hadi sasa na ambazo Misri ameendelea kuzifuata tangu zamani hadi wakati wetu wa sasa na jinsi zinavyounda kiungo cha karibu kwa vipengele vya taifa la Misri vilivyothibitisha utambulisho hadi sasa.”
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy