Bwana Ghazaly mmisri anapata lakabu la mhusika mwaafrika kwa mwaka wa 2019

Bwana Ghazaly mmisri anapata lakabu la mhusika mwaafrika kwa mwaka wa 2019
Bwana Hassan Ghazaly mmisri, mwanzishi wa Ofisi ya Vijana ya Kiafrika kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Vijana wa Afrika alishinda tuzo ya mhusika mwafrika kwa Mwaka katika hafla ya hitimisho iliyofanyika wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Vijana waafrika huko Akra, Ghana, ambapo shughuli zake hufanyika mnamo tarehe 21 hadi 23 Novemba. kwa mahudhurio ya waatalamu wa viongozi waafrika na juu yao Rais wa zamani wa Ghana, Bwana John Mahama.

Katika muktadha huu, Ghazaly alishindana taji pamoja na wagombea wengine watano, hasa Aya El Shaby wa Tunisia - mjumbe wa Umoja wa Afrika kwa vijana, na mwanariadha mchanga Kastar Seminia kutoka Afrika Kusini.
Wizara ya Vijana na Michezo ya kimisri , Waziri wa Vijana Ashraf Sobhy na sekta za vijana waafrika kutoka nchi tofauti za bara, walikuwa na sehemu kubwa katika kumuunga mkono Ghazali kupitia kupiga kura ya moja kwa moja kutoka kwa vijana wa bara hilo, wakati ambapo kulingana na shughuli za Tume ya tuzo, Ghazali alipata zaidi ya maoni 4500.
Tuzo hizo, zilizowasilishwa kwa taasisi ya Wanasiasa Vijana na Viongozi, zinalenga kutambua na kuhamasisha mafanikio ya watengenezaji wa mabadiliko barani Afrika kwa kuwapa nafasi ya kupata uzoefu muhimu na kuthaminiwa vizuri kwa matarajio yao na ubora wao wa kitaifa na kimataifa . wakati ambapo wagombea walishindana kwa tuzo kadhaa nazo ni " Msanii wa mwaka- Mjasiriamali wa mwaka- Kiongozi mtarajiwa kwa mwaka- Mwanamke mwanasiasa kwa mwaka- Mwanasiasa kwa Mwaka - Muundaji wa Sera za kisiasa kwa mwaka - na Mhusika wa mwaka".
Tuzo hizo zilitolewa kwa washindi saba - mmoja kutoka kila kikundi- ambavyo ni:
1- Mtu wa Mwaka - Hassan Ghazaly (Misri)
2. Mtu wa Siasa wa Mwaka - Bobbi Wayne (Uganda)
3. Kiongozi Mtarajiwa kwa mwaka - Elizabeth Wanjiru Wathhoti (Kenya)
4. Mwanamke wa Kisiasa wa Mwaka - Malambo Bomba (Zambia)
5. Muundaji wa sera za kisiasa kwa Mwaka - Samson Hayles Kebede (Ethuopia)
6. Mjasiriamali wa Mwaka - Gavniwi Guibert (Kamerun)
7. Msanii wa Mwaka - Davido (Nigeria)
Mkutano huo uliwakusanya vijana kutoka nchi zaidi ya 30 barani Afrika na ulihangaika kutoa maoni na masuluhisho kutoka kwa vijana bora zaidi kwenye bara hilo na kuyaweka katika mada husika zinazoweza kuunda sera ya bara hili;
ambapo mkutano huo ulijadili masuala yanayohusu viwanja kadhaa vya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kibiashara.
inatajwa kuwa Ghazali alianzisha mipango kadhaa ya vijana na shughuli zinazohusiana na Ukaribu wa Kiafrika, pamoja na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika, Shule ya Afrika 2063, Mradi wa Bezoor wa kielimu, na shughuli zingine za bara; jambo lililomfanya kustahili kupata tuzo ya Mhusika wa mwaka, na hivyo kupitia kupiga kura toka wana wenyewe wa bara wenye Utaifa tofauti wa nchi zao.