Waziri Mkuu afuatilia maandalizi ya uratibu wa maonyesho na mkutano wa matibabu wa kiafrika wa kwanza

Waziri Mkuu afuatilia maandalizi ya uratibu wa maonyesho na mkutano wa matibabu wa kiafrika wa kwanza

Dokta Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu alionesha ripoti ikitolewa na Meja Jenerali Daktari, Bahaa Eldin Zidan, Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa mamlaka ya kimisri ya ununuzi wa pamoja na ugavi wa matibabu na usimamizi wa Teknolojia ya matibabu, inayohusiana na maandalizi maalum ya mamlaka kuratibu maonyesho na mkutano wa matibabu wa kiafrika wa kwanza "ExCon Health Africa".

Meja Jenerali, Bahaa Eldin Zidan, alieleza kupitia ripoti hiyo kwamba mamlaka ya kimisri ya ununuzi wa pamoja na ugavi wa matibabu na usimamizi wa teknolojia ya matibabu imeanza kuandaa uratibu wa maonyehso na mkutano wa matibabu wa kiafrika wa kwanza ambao utafanyikwa kuanzia tarehe tano hadi saba ya Juni ijayo, chini ya Uangalifu wa Rais wa Jamhuri, Abd El-Fatah El-Sisi.

Meja Jenerali, Bahaa Eldin Zidan, alisisitiza kuwa mamlaka, kupitia kufanyika kwa mkutano huo, inataka kuufanya mkutano wa kila mwaka kati ya makampuni ya kimataifa na maafisa wa sekta ya matibabu kwa upande wa kiafrika, ambapo kupitia kwake teknolojia mpya itaonyeshwa katika nyanja za matibabu na kuanzisha tovuti ya shughuli endelevu inayounganisha maafisa wa huduma ya afya, makampuni yaliyotengeneza, wawakilishi, wasambazaji na watoa huduma za afya ulimwenguni pamoja, pia kutoa nafasi kwa makampuni yote ya huduma za afya kuingiliana pamoja.

Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa mamlaka ya kimisri aliongeza kwamba maonyesho yatatoa nafasi nyingi zinazozilenga sekta mbalimbali kugundua bidhaa za matibabu na kategoria zake mbalimbali kama bidhaa na vifaa vya matibabu, vitu vya kemikali, vitendanishi vya maabara, vifaa vya matibabau, mambo yanayohusu upakuaji, bima ya matibabu, lishe ya tiba na vitamini, pamoja na mambo yanayohusiana na hospitali na maduka ya dawa, bidhaa za ngozi na vifaa vya meno, akionesha kuwa matukio yatajumuisha kufanyika kwa idadi ya mahojiano na mazungumzo ya kipekee yanayohusiana na mipango ya elimu inayoendelea ya wafanyakazi wa matibabu kwa kuzingatia masuala maarufu zaidi katika nyanja za matibabu barani Afrika.

Meja Jenerali, Bahaa Eldin Zidan, alionesha kwa kifupi, kupitia ripoti, maandalizi ya uratibu wa maonyesho wa mkutano ikiwemo Hadhira, usafirishaji, programu ya mkutano na pia matukio yatakayofanywa wakati wa mkutano.

Mwishoni mwa onyesho la ripoti, Waziri Mkuu aliweka wazi nia ya nchi kuratibu mikutano na maonyesho kama hayo, haswa ambayo yanaunga mkono kuimarisha pande za ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na nchi za Bara la Afrika, kwa mujibu wa maagizo ya Rais wa Jamhuri, Abd El-Fatah El-Sisi na pia ikisambamba na malengo ya Ajenda ya kiafrika 2063 inayojikita umuhimu wa kuongeza uwekezaji wa huduma ya afya na hivyo inaimarisha ufanisi wa sekta ya matibabu barani Afrika.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba mkutano inayopangwa kuufanyika kama shughuli na matukio,zitakuwa sawa sawa pamoja na  juhudi zifanyazo ili kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu yanayohusu upatikanaji wa bima ya afya kwa wote na kuhakikisha  huduma mpya za afya za kimsingi, pamoja na juhudi za upatikanaji wa madawa na chanjo salama zenye ufanisi na ubora wa juu za kimsingi kwa bei nafuu kwa wote, mbali na juhudi maalum ya kugeuza utengenezaji wa madawa ili yawe ya kitaifa.