Kuhitimu kundi jipya la makada wa Kiafrika katika fani ya kuzuia na kupambana na Ufisadi

Kuhitimu kundi jipya la makada wa Kiafrika katika fani ya kuzuia na kupambana na Ufisadi

Chuo cha Kitaifa cha Kupambana na Ufisadi cha Mamlaka ya Kudhibiti Utawala kiliandaa hafla ya kuhitimu kwa kundi jipya la wanafunzi 36 kutoka nchi 12 za Kiafrika, kama sehemu ya ufadhili wa Rais Abd El Fatah El-Sisi. 

Hayo yalitokea katika utekelezaji wa maagizo ya Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya kutoa ufadhili 250 wa mafunzo kwa makada wa Kiafrika wanaofanya kazi katika uwanja wa kuzuia na kupambana na Ufisadi ;kwa lengo la kujumuisha uwezo wa Bara la Afrika kukabiliana na kuzuia Ufisadi kwa aina na sura zake mbalimbali.

Mpango huo ulijumuisha mafunzo kuhusu shughuli za kuzuia na kupambana na Ufisadi na kuongeza ufahamu wa hatari na athari zake hsi kwa maendeleo endelevu barani Afrika, Kutayarisha na kutekeleza mikakati ya kupambana na Ufisadi na kudhibiti hatari za Ufisadi na mikataba inayohusiana ya kimataifa. Pamoja na uchunguzi wa kesi za kupambana na Ufisadi na kurejesha mali. 

Katika hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya kuhitimu programu ya mafunzo, Waziri Hassan Abd El Shafi Ahmed, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Utawala, aliwapongeza wahitimu kwa kupita katika programu ya mafunzo,

akieleza kuwa inakuja katika utekelezaji wa maagizo ya Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kutoa ufadhili wa masomo 250 kwa makada wa Kiafrika wanaohusika na kuzuia na kupambana na Ufisadi, ambayo ni uthibitisho wa imani ya serikali ya Misri katika uongozi wa kisiasa katika umuhimu wa mwelekeo wa kimkakati na kihistoria unaowakilishwa na bara la Afrika,  akithibitisha ukaribisho wa kudumu wa Misri kwa ndugu kutoka bara la Afrika ili kuunganisha masuala ya Ushikamano na Ushirikiano kwa ajili ya kesho bora kwa watu wa bara la Afrika.

Waziri huyo aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje kwa mchango wake wa kuratibu ushirikiano kati ya Misri na Afrika katika nyanja nyingi zinazowakilishwa na Wakala wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Misri uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri na kuwa jukwaa rasmi la kubadilishana uzoefu wa maendeleo na nchi zote za Afrika.

Na aliashiria kwamba katika uwanja wa kupambana na Ufisadi, Misri iliandaa matukio mengi, huku Kongamano la kwanza la Afrika likifanyika Kupambana na Ufisadi huko Sharm El-Sheikh kwa mwaliko wa Rais mnamo 2018, wakati wa ushiriki wake katika mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Afrika, kuwa wa kwanza wa aina yake Barani, Sambamba na uongozi wa Misri wa Umoja wa Afrika wakati huo, na kufanya  kongamano hilo kama jukwaa la mazungumzo baina ya nchi za bara hilo kwa lengo la kubadilishana uzoefu na taarifa kuhusu masuala ya Ufisadi.

Alieleza kuwa Afrika ilikuwepo kwa dhati katika shughuli za kikao cha tisa cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Ufisadi huko Sharm El-Sheikh Desemba 2021, ili kukamilishana pamoja mchakato wa kazi na hatima ya pamoja.

Mwishoni mwa hotuba yake, Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Utawala wa Kitaaluma dhidi ya Ufisadi aliagiza kuendelea kufanya kozi za mafunzo kwa ushirikiano na vyombo vya ndani, kikanda na kimataifa vinavyohusika na mapambano dhidi ya Ufisadi,

Kulingana na mpango wa kazi wa Chuo na kuhakikisha mawasiliano yanayoendelea na vifaa vingine.

Pia, Samuel Jokbani, Makamu wa Rais wa Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini Sudan Kusini, alitoa hotuba kwa niaba ya washiriki wengine wa mafunzo.

Wakati huo, aliishukuru Misri kwa msaada wake wa kudumu kwa nchi za bara la Afrika, na kushukuru Chuo cha Kitaifa cha Kupambana na Ufisadi kwa kuandaa programu ya mafunzo, iliyoboresha ujuzi wao kwa habari nyingi na uzoefu.pia aliomba kuendelea kutoa programu na kozi hizo ili kusaidia makada wa Kiafrika katika fani ya kuzuia na kupambana na Ufisadi, kutokana na uzoefu wa Misri katika uwanja huo.

Hiyo inakuja ndani ya mfumo wa jitihada za mara kwa mara za Misri kuendeleza masuala ya ushirikiano wa pamoja na bara la Afrika, kupitia mashirika na vyombo mbalimbali, ikiamini kuwa maendeleo endelevu huzaa matunda kupitia juhudi za pamoja baina ya nchi, haswa kuwa Misri inashiriki na nchi ndugu  Barani Afrika maoni sawa ya maendeleo kutokana na ukaribu wa kijiografia unaosababisha njia ya Ushirikiano wa kikanda wenye ufanisi zaidi katika nyanja mbalimbali.