"Madbuly ni mdhamini kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "

"Madbuly ni mdhamini kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "
Wizara ya vijana na michezo ilitangaza uangalifu wa bodi la mawaziri kwa uongozi wa Dokta "Mustafa Madbuly" kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika, unaotolewa kwa Wizara (Ofisi ya vijana waafrika na idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia) mnamo kipindi cha 8 hadi 22 mwezi wa Juni 2019,kwa kushirikiana na Umoja wa vijana waafrika.
Na hayo yote yanakuja kulingana na Shime na usaidizi wa taifa kwa suala la kiafrika ; kutekleza yaliyotangazwa na Rais wa Jamhuri mnamo matukio ya mkutano wa vijana wa dunia ulioshuhudia uwakilishi adhimu kwa vijana wa nchi za kiafrika, na kwa imani yake kwa mchango wa vijana waafrika na umuhimu wa kutoa njia zote za misaada, kuwezesha, na kufunza, pamoja na kuwawezesha katika vyeo vya kiutawala na kunufaika toka uwezo na mawazo yao.
Na Udhamini huu unazingatia kipengele kimoja cha vipengele vya kutekleza mpango wa (1Million by 2021) ili kuwawezesha vijana waafrika milioni moja kwa kufikia mwaka wa 2021, uliotolewa kwa Kameshina ya Sayansi, Teknolojia, na Rasilimali za binadamu katika Umoja wa kiafrika, na unalenga kwa kuhamisha jaribio kale la kimisri la kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha makada vijana waafrika wa kimageuzi wenye mitazamo inayosawazisha na mielekeo ya urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika na yenye Imani ya kuhudumia malengo ya Umoja wa kiafrika kupitia ukamilifu, pamoja na kuunda mkusanyiko wa viongozi vijana waafrika wenye athari kubwa barani; kwa mafunzo, uzoefu unaolazimishwa na mitazamo ya kimikakati.