UTAIFA WA AFRIKA - Sehemu ya Pili

UTAIFA WA AFRIKA - Sehemu ya Pili

Utamaduni ni silaha yenye nguvu kubwa kuleta mabadiliko. Ukombozi wa Afrika utawezekana tu watakapopata Waafrika utambulisho wa pamoja.

[Waafrika] waliostaarabika, bila kujali walipo wala chanzo cha mawazo yao, wanatazama utamaduni kama chombo cha kwanza kinachomtofautisha Mwafrika na asiye Mwafrika, kukutanisha matambulisho ya kitaifa na kikabila, kwa kuangazia mambo mengi yanayohusiana na mapatano na Mzungu, kukadiria matokeo ya dini na tamaduni za kutoka nje (mwa bara la Afika) na kutafuta suluhisho la kudumu kwa matatizo ibuka ya uchumi na siasa.¹ Huu ndio msingi wa Utaifa wa Afrika, unaosimamia tamaduni historia ya Waafrika kwa pamoja.

Ukeketaji wa fahari ya utamaduni wa Mwafrika ni mpango uliofasilishwa kwa makini ili kuangamiza heshima ya nafsi na kuharibu mwelekeo wa mapendeleo yake kimawazo katika asili yake.

"...Kwa hakika utawala wa kikoloni unaratibisha unyanyasaji wa kiutamaduni na kujaribu kufutilia mbali kwa uwazi au kwa njia fiche viungo muhimu zaidi vya watu husika. Lakini watu wanaweza tu kuunda na kuendeleza vuguvugu la ukombozi kwa kuhifadhi utamaduni wao dhidi ya mpango wa kuendelezwa kwa unyanyasaji wa utamaduni wa maisha yao kwa kuendelea kuzuia, kiutamaduni, hata wakati pingamizi lao la kisiasa na jeshi linapoangamizwa. Na ni pingamizi la kiutamaduni ambalo, kwa wakati mmoja, unaweza kuchukua mwemko mpya, aghalabu, kisiasa, kiuchumi, kujihami kupigana na utawala wa ughaibuni." ~ Amilcar Cabral²

Kupata tambulisho la pamoja kwa Waafrika wote ni muhimu kwa kuliunganisha Afrika, jambo ambalo viongozi katika mwamko wa utaifa (wa Afrika) kama vile Cheikh Anta Diop wa Senegal na Frantz Fanon wa Martinique waliangazia katika miaka iliyotangulia uhuru wa nchi za Afrika, ambao kwa kuinukia mapendeleo ya miundo ya kiserikali, walitafuta kupatanisha mradi wa Jumuiya ya Kiafrika (Pan Afrikan) na ukombozi wa kimawazo kutokana na ukoloni. Fanon, aliyekuwa daktari wa magonjwa ya kiakili (au Mtaalamu wa Saikolojia), alifuatilia magonjwa ya kiakili yaliyohusishwa na utawala wa ukoloni nchini Algeria na kupatanisha mabadiliko ya afya na utimamu wa watu na ukombozi unaotokana na Jumuhia ya Kiafrika na Muungano wa Afrika.³

Kuwepo kwa mawazo ya chuki dhidi ya utamaduni wa mtu husika, humfedhehesha mtu huyo na unaweza tu kuepukwa kwa kujipenda katika muktadha wa utamaduni wa mtu husika. 

¹Nguvu ya Tamaduni za Kiafrika (2003), Toyin Falola. ukr. 3

²Utambulisho na Heshima katika Muktadha wa Pambano la Ukombozi wa Taifa (1972) katika machapisho, Ndimi Kwa Kuwa Tuko: Masomo katika Falsafa ya Kiafrika, Fred Lee Hord na Jonathan Scott Lee. ukr 85

³Ukombozi wa Afrika: Wasifa wa Nyerere (2010), Chambi Chachage na Annar Cassam. ukr 47