Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia nchini Qatar 

Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia nchini Qatar 

 Imeandikwa na| Mariam Islam 

Kombe la Dunia ni mojawapo ya matukio muhimu zaidi Duniani, linalofanyika baada ya miaka minne mfululizo, tangu mwaka wa 1930, lakini lilifutwa miaka ya 1942 na 1946  kwa sababu ya Vita vya pili vya Dunia. Timu 32 za kimataifa hushiriki wakishindana kupata nafasi ya kushinda kwa mwezi mzima katika nchi mwenyeji.

Mnamo  2010 Qatar ilipata heshima kubwa ya kuandaa Kombe la Dunia, ikizishinda nchi kama Marekani, Korea Kusini, Australia, na Japan, kwa hiyo hii ni mara ya kwanza kwa Qatar kuandaa Kombe la Dunia, na pia ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia lifanyike katika Ulimwengu wa kiarabu,Qatar ilitumia takriban zaidi ya dola bilioni 200 kuandaa miundombinu, miradi mikubwa, na hoteli, ikitenga dola bilioni saba kwa matayarisho ya Kombe la Dunia, pia ilitoa juhudi kubwa sana, ilitekeleza yasiyo ya kifani hata zaidi ya  yanayotarajiwa. 

Qatar imeandaa viwanja vya michezo vilivyo ni vifaa vya hali juu kuliko zaidi viwanja vingine ulimwenguni. Pia kwa sababu ya hali ya hewa ya joto kali, wameweka viyoyozi katika viti vya mashabiki, na waliweka viyoyozi mitaani mwa nchi zote, pamoja na kuandaa hoteli na makazi kwa mashabiki kwa bei zinaendana na viwango vyote, pia ilisambaza vibandiko vya hadithi za Nabii nchini kote.

Qatar imetengeneza viwanda saba kwa njia inayoiga mtindo wa kiaarabu na kiqatar kwa mfano uwanja wa Al-Bait unaoiga hema la jadi la watu wa ghuba, na uwanja wa Al-Janub ni kama mtanga ya boti za jadi za Qatar, na pia kuna uwanja wa Al-Thamama uliyo ni sawa na kilemba wa waarabu, ambapo ni sifa ya wakazi wa nchi za ghuba, pamoja na uwanja wa 974 ni idadi ya makuntena waliyatumia kujenga uwanja huo, na ndio ni uwanja wa kwanza unayoweza kuumbuliwa na itautoa kwa nchi masikini.

 Kulingana na ukaribu wa viwanja, mashabiki wanaweza kuhudhuria zaidi ya mechi moja ndani ya siku ile ile, hii ni moja wa mambo yaliyotofautisha Qatar na nchi nyingine, kwa hiyo ilitayarisha vituo bora vya kimataifa kuandaa mashindano na vikao vya michezo na nchi nyingine waliyoandaa Kombe la Dunia mnamo miaka iliyopita.

 

Qatar imeanza sherehe ya Ufunguzi wa Kombe la Dunia kwa aya za Quran tukufu, kiasi kwamba Sheikh mmoja amekaa akizungukwa na watoto wakisoma aya fulani kutoka Sura ya Al-Rahman, baadaye wamefanya maonyesho mengi kama matatu au manne takriban, na mwimbaji wa bendi ya BTS ya Korea Kusini "Jung Kook" aliyeimba wimbo wa "Dreamers" siku ya sherehe ya Ufunguzi wa Kombe la Dunia. Huko wakati muadhini alipoita, Qatar ilisitisha shughuli zote hadi mwisho wa adhana kwa dakika mbili takriban, pamoja na hao wote, Mwigizaji mashuhuri wa Marekani "Morgan Freeman" alionekana katika moja ya maonyesho, alipokuwa akiongea kwa mapenzi makubwa na balozi mdogo wa hisani mwenye ulemavu “Ghanim Al-Moftah”.

Idadi ya wageni nchini Qatar huenda kufikia takriban milioni na nusu wakati wa Kombe la Dunia, ambayo ni idadi kubwa ikilinganishwa na ukubwa wa Qatar, ambapo ukubwa wake ni takriban kilomita mraba elfu kumi na mbili.

Waarabu wote walionea fahari kwa ilivyofanywa na Qatar, waliiunga mkono kwa njia zote dhidi ya kampeni za Magharibi, kiasi kwamba Qatar haikiri haki za wapenzi wa jinsia moja, na kukataza kuvaa bendara yao ya rainbow.

Qatar imejaribu kubadilisha sura potofu ya Waarabu kwa watu wa Magharibi kupitia kutilia mkazo juu ya ukarimu wa Waarabu, kuwakaribisha wageni, na  kuheshimu tamaduni tofauti.

Kombe la Dunia nchini Qatar ndilo ni bora zaidi katika historia, kwa sababu hii ni mara ya kwanza liandaliwe katika nchi moja ya Kiarabu, ndio ni mara ya kwanza lifanyike wakati wa msimu wa baridi na katikati ya msimu wa Soka, na pia ni mara ya kwanza ya kutumia teknolojia ya nusu-otomatiki ya kubaini nafasi ya kuotea katika michuano ya Kombe la Dunia. Je, tutashuhudia nchi nyingine ya Kiarabu ikiweza kuandaa Kombe la Dunia?