Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa waanza shughuli za siku ya pili wakitembelea Jumuiya ya nchi za kiarabu
Shughuli za siku ya pili ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa umejumuisha ziara kwa makao makuu ya Jumuiya ya nchi za kiarabu, Washiriki wa Udhamini huo walipokelewa na ujumbe wa ngazi ya juu ya Jumuiya ya nchi za kiarabu, ukiongozwa na Balozi, katibu mkuu msaidizi, Mkuu wa sekta ya masuala ya kijamii katika Jumuiya ya nchi za kiarabu "Haifa Abu Ghazaleh" pamoja na ujumbe wa viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo.
Balozi " Haifa Abu Ghazaleh" mwanzoni mwa hotuba yake aliwakaribisha washiriki wa Udhamini huo, akiwawasilisha salamu za katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi za kiarabu
" Ahmed Abu Elgheit" kisha aliwatoa ufafanuzi mwingi kuhusu Jumuiya ya nchi za kiarabu ambayo ni kama Shirika kongwe sana katika eneo la mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika iliyoanzishwa tangu Machi,1945 na inajumuisha nchi 22 za kiarabu, na kazi yake ni kuboresha uratibu kati ya wanachama wake katika masuala ya pamoja kwa mujibu wa mfumo wa kazi yake kupitia Baraza la Jumuiya katika Wizara ya Mambo ya Nje, Baraza la Uchumi na kijamii,na mabaraza maalum ya Wizara ya kiarabu kwa kushirikiana na mashirika maalum ya kiarabu, mashirika na taasisi maalum za jamii ya kiraia ya kiarabu na kimataifa pamoja na mashirika maalum ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi katika eneo la kiarabu, sekta ya kibinafsi na taasisi za ufadhili.
Waziri, Kamishna, Mkurugenzi wa idara ya uhamiaji na Wageni
" Enas Ferjani" alizungumzia suala la uhamiaji, wakimbizi na watu walioacha makazi yao pamoja na mikakati ya Jumuiya ya nchi za kiarabu; kuimarisha ulinzi, mifumo ya kisheria na juhudi za makazi mapya. Na pia Waziri Kamishna,Mkurugenzi wa idara ya maendeleo na sera za kijamii na pia faili kadhaa za sekta ya kijamii za Jumuiya ya nchi za kiarabu; ili kuimarisha juhudi za nchi za kiarabu zenye malengo ya kutekeleza mpango wa Maendeleo Endelevu 2030,Mazungumzo hayo yalijadili mikakati na mipango ya kazi iliyowekwa kwa mkutano wa kilele wa kiarabu haswa mfumo wa mkakati wa kiarabu; ili kutokomeza umaskini wa pande nyingi, pamoja na mpango wa kazi ya kiarabu; kutokomeza sababu za kijamii zinazofanya ugaidi na mipango na programu zingine zinazozingatia maisha ya binadamu wa kiarabu pamoja na kuzingatia kuimarisha jukumu la vijana na wanawake na kusaidia makundi dhaifu katika jamii haswa watu wenye uwezo maalum, wazee na watoto na kuhimiza jukumu la familia.
Waziri Kamishna aliongeza kuwa Jumuiya ya nchi za kiarabu ina mpango ujao wa kuimarisha dhana na utamaduni wa lugha ya kiarabu kwa kimataifa na pia Jumuiya itashirika katika onyesho la shughuli za maonyesho ya Dubai "Expo" ya kimataifa huko Emirates, ambayo yametarajia kuwavutia wageni 25 Duniani kote na litaendelea kwa muda wa miezi sita katika maadhimisho ya Siku ya lugha ya kiarabu Duniani.
Afisa wa Jumuiya ya nchi za kiarabu aliwasindikiza washiriki katika Udhamini huo kwa ziara katika pande na duara mbalimbali za Jumuiya, na masuala mengi yalijadiliwa ya mifumo ya kazi ya uingiliaji kwa Jumuiya ya nchi za kiarabu; kudhibiti vikwazo vingi vinavyojilazimisha katika nchi nyingi kama kweli halisi.