Warsha ya kazi miongoni mwa shughuli za siku ya tisa ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Matukio ya siku ya tisa ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa yalianza kwa uratibu wa warsha ya kazi kwa makundi ya vijana wanaoshiriki kwenye Udhamini kwa jina ya "ubadilishaji wa kiutamaduni na jukumu lake la kuunda Amani ulimwenguni", Ambapo walioshiriki walijadiliana kuhusu jukumu muhimu ya tamaduni mbalimbali kuunda Amani baina ya wananchi, pia waligawanyika makundi wakizungumzia changamoto ngumu zaidi zinazozuia ujenzi wa Amani ulimwenguni, Na hiyo itakuwa kupitia shughuli inayotegemea uchoraji wa mti unaowasaidia kuyafikiri mawazo kupambana na changamoto ambazo jamii zinazikumbwa, Kwa hivyo, walioshiriki wanafanya uchunguzi kwa ujumla kwa sababu kuu za changamoto zitakazoeleza katika mazungumzo yao, kuangalia nguvu na rasilimali zinazopatikana na kuanza kuumba mawazo ya kukabiliana na changamoto hizo, Warsha pia ilijumuisha mawazo mengi, maoni, mapendekezo na mipango ya vijana ambayo itaweza kufikiwa kwa ajili ya kuisaidia jamii na utu wakati wa mawasiliano na ushiriki mkubwa wa walioshiriki wa Udhamini.