Misri na NEPAD

Misri na NEPAD

Imefasiriwa na  / Nourhan Khaled Eid

NEPAD ni muhtasari wa tafsiri inayomaanisha " Ushirikiano mpya wa Maendeleo ya Afrika", ili kujumuisha mtazamo wa Umoja wa Afrika wa Maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Bara la Afrika. 

Au ni mojawapo ya Majaribio ya vitendo ya maendeleo ya Bara la Afrika na kukabiliana na umaskini kupitia ushirikiano na jamii ya kimataifa na kikanda kwa ngazi ya nchi, na kwa ngazi ya mikusanyiko ya kiuchumi iliyopo ndani ya Bara la Afrika.

Iliundwa na ilifadhiliwa na Wakuu wa nchi tano, nazo ni Misri, Algeria, Nigeria, Afrika Kusini na Senegal, iliwekwa na Kilele cha Jumuiya ya Nchi Huru za Afrika "inayojulikana kama Umoja wa Afrika baadaye" iliyofanyika huko Luksa  mji mkuu wa Zambia mnamo mwezi wa Julai, mwaka wa 2001, na inajumuisha nyanja za kazi za NEPAD, kilimo, usalama wa chakula, usimamizi wa rasilimali asilia,mabadiliko ya tabia tabianchi,  ufungamano wa kikanda, na miundombinu, pamoja na programu za kazi katika sekta ya maendeleo ya miundombinu , maendeleo ya Rasilimali watu, serikali ya kiuchumi na ushirikiano. 
Wakati wa kuundwa taasisi ya Umoja wa Afrika, kwa mujibu wa tangazo la Addis Ababa mnamo Mei 25, 1963, lengo lake kuu lilikuwa kukamilisha harakati za kupata uhuru kutoka udhibiti wa ukoloni, na wakati huu kuna nchi nyingi miongoni mwa nchi za Bara humo, zilikamatwa haswaaeneo la uongozi wa Uhispania, na Ureno na pia weusi kutoka kusini ya Afrika walisumbua ubaguzi wa rangi uliowekwa na wa weupe 
Tamaa ya kiliberali ilitawala kazi ya Shirika mnamo miongo miwili ya kwanza ya uhai wake, hata hivyo, kujikita kwa mataifa ya kitaifa yanayoibukia kwa wakati ulianza kufichua mipaka ya malengo ya shirika.Migogoro ya kisiasa, kijeshi na usalama iliibuka ambayo ilikuwa ya kutisha zaidi. kuwepo kwa baadhi ya nchi kuliko ukoloni, kama vile vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Kongo, Angola, na Chad

 Upungufu wa kiuchumi wa nchi nyingi za bara hilo na kuongezeka kwa deni la serikali kuliamuru kwamba Shirika linapaswa kupanga upya vipaumbele vyake ili kukabiliana na ukweli mpya. Na suala la kubadilisha mwelekeo wa jumla wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika kutoka ukombozi wa kisiasa na kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika ngazi ya bara hilo likawa ni jambo la kushughulishwa na mikutano ya kilele ya Afrika tangu mwishoni mwa miaka ya sabini ya karne ya ishirini. 

Mwakani mwa 1980, programu ya maendeleo imewekwa inajulikana kama "mswada wa Lagos kwa Kazi" inayofuatia mwakani mwa 1986, Mpango wa dharura wa mageuzi ya kiuchumi Barani Afrika. Kisha “Mfumo wa Kiafrika wa Marejeleo ya Mipango ya Marekebisho ya Miundo” mwaka 1989 , kisha “Mkataba wa Arusha wa Ushiriki na Maendeleo ya Watu” mwaka 1990 , lakini mipango yote hii ilishindikana, na juhudi za Umoja wa Afrika zikaanza kuelekeza nguvu zake katika kuweka fuwele mpya. mkakati unaofahamu kutokuwa na uwezo wa Afrika kujiendeleza kwa ufanisi na upesi kiasi, Inapendekeza ushirikiano wa pande nyingi kwa ajili ya msaada wa kimataifa. 

Na kwa hivyo NEPAD imepatikana kama tija muhimu sana ya kukaribisha na kufanya marekebisho,tena imetolewa na kizazi mpya wa viongozi waafrika, walioona kuwa mfumo wa kisiasa wa Jumuiya ya Nchi Huru za Afrika hautoshi kwa wakati ambapo maendeleo yanahitajika sana na Bara liko nyuma kabisa katika ngazi ya kimataifa.

Na miongoni mwa makubaliano ya ushirikiano wa Algia kwa ajili ya kurekebisha Afrika. Imewekwa na Rais wa zamani wa kusini ya Afrika, Tabu Mabki, aliyefichua shughuli za jukwaa ya Dafos ya kiuchumi kimataifa 2001.


Lakini kabla ya mpango wa Ambaki, Rais wa Senegal Abdallah wad alifikia mkutano wa kilele cha Frankofia nchini Cameron, mwanzoni mwa Januari mwaka wa 2001, mpango wa Omigha, unaojumuisha "maendeleo ya Kiafrika " na inaingilia makubaliano katoka mpango mpya unaoitwa mpango mpya kwa ajili ya Afrika, manufaa yake yamedhihirisha mwishoni mwa ushindi ili kuendeleza Afrika kwa NEPAD iliyokuwa kusini ya Afrika, 
Senegal, Algeria, Nigeria na Misri ndio watetezi wake muhimu zaidi, na wanasifiwa kwa kuipitisha katika Mkutano wa Wakuu wa Afrika mwaka 2001. 


Mpango huo unalengea kukabiliana na umaskini,  na kufikia maendeleo endelevu, kuachia pembe Bara la Afrika, na kuingilia uchumi wa kiafrika na uchumi wa kimataifa, na pia mpango unasisitiza miliki ya kimawazo kwa Bara hilo, na kujitegemea rasilimali,  kushirikiana na raia wa Kiafrika,  kufikia uunganishaji wa kikanda na bara, kuendelea kuhimizana nchi za Bara,  na ushiriki na nchi zilizoendelea ili kupungua kasoro kati yake na Afrika , kwa programu za kazi zilizohusika kwa kundi la vipaumbelevya sekta liliundwa na nyanja mbalimbaliza kazi za NEPAD ili kufikia malengo yanayotarajiwa, yaliyowikilishwa katika kulinda Amani na Usalama Barani humo. Kufikia udhibiti bora wa kisiasa na kiuchumi, kukuza dhana za demokrasia na kuheshimu haki za binadamu, kuongeza mazao ya kilimo na kufikia usalama wa chakula, kuongeza kiwango cha biashara ya ndani ya Afrika, kupunguza mauzo ya nje ya Afrika katika masoko ya kimataifa, kuboresha mazingira, na kuendeleza elimu na utafiti wa sayansi.

Mipango ya kazi pia inajumuisha kuongeza matumizi ya teknolojia ya habari, afya na kupambana na magonjwa yanaenezwa, hasa hasa UKIMWI na Malaria, maendeleo ya binadamu na kujenga uwezo wa Afrika, wakati wa kufanya kazi katika muktadha huu kutoa rasilimali muhimu ya kuendeleza miradi na programu za uendeshaji muhimu ili kufikia malengo haya.

NEPAD ina mipango miwili kuhusu kukusanya rasilimali zinazohitajika ili kutekeleza programu zake vitendo:

 Mpango wa Mtiririko wa Ujasiriamali

 Ilijumuisha makadirio ya rasilimali za kifedha zinazohitajika kwa ajili ya kufadhili programu za NEPAD, kama hati likikadiria kuwa karibu dola bilioni 64 kila mwaka (kwa takriban miaka 15). Hati hii ilieleza kuwa kuziba pengo hili kunahitaji ongezeko Hata hivyo, ilisisitiza kuwa “rasilimali nyingi zinazohitajika lazima zije nje ya Bara hili.” Kwa hiyo, NEPAD ilizingatia sana malengo na taratibu zinazohusiana na uhamasishaji wa nje ya bara,
 rasilimali, ikizingatia nguzo tatu kuu:

(a) Mipango mipya ya kujadiliwa kwa lengo la kuondoa deni la nje. 

(b) Marekebisho mapana (na ya kiubunifu) katika usimamizi wa misaada ya maendeleo kutoka nje na kuiunganisha na hali na ahadi za pande zote kati ya Afrika na wafadhili ili kuongeza wingi wa misaada na kuboresha ufanisi wake. 

(C) Kuhimiza mtiririko wa mitaji ya kibinafsi ya kigeni, ambayo NEPAD inazingatia umuhimu mkubwa katika kuziba pengo la rasilimali. 

 Mpango wa Ufikiaji Soko 


 NEPAD inazingatiwa kuboresha ufikiaji wa masoko ya kimataifa kwa mauzo ya nje ya Afrika kama kipengele muhimu cha uhamasishaji wa rasilimali. Mpango huu unajumuisha njia ya kufikia hili katika kanuni moja: mseto wa uzalishaji. Mseto huu unatokana na unyonyaji mzuri wa msingi wa maliasili za Afrika kupitia hatua na mageuzi katika kila sekta ya kilimo, viwanda, madini, utalii na huduma, pamoja na maendeleo ya sekta binafsi pia  kuchukua hatua za kuhimiza mauzo ya nje ya Afrika viwango vya Afrika na kimataifa, na kuondolewa kwa vikwazo visivyo vya ushuru "kodi" vinavyokabiliana navyo katika masoko ya nchi za kiwanda. 
 Kuhusu maudhui ya "ushirikiano mpya wa kimataifa" uliopendekezwa na NEPAD, inahusisha vipengele viwili: ya kwanza, kuhifadhi ubia kati ya Afrika na washirika wa maendeleo, kuhalalisha, na kuongeza matumizi yake. Pili, kujadili uhusiano mpya na nchi zilizoendelea na mashirika ya kimataifa. Mahusiano hayo mapya yanajumuisha malengo na viwango vya utendakazi vilivyokubaliwa pande zote, na majukumu na wajibu wa pande zote. NEPAD inapeana nchi zilizoendelea na mashirika ya kimataifa majukumu na wajibu katika nyanja za ushirika wake, kumi na mbili kati yao ziliorodheshwa katika hati na kujumuishwa katika aya ya (185) ya waraka. Kwa kubadilishana na majukumu haya ya ahadi, viongozi wa Afrika wanajitolea kwa upande wao kutekeleza hatua zilizotajwa katika sura ya tatu ya NEPAD (aya ya 49). 

Mbinu za utekelezaji:

Utekelezaji wa Ushirikiano mpya wa Maendeleo ya Afrika unawakilisha maudhui ya sura ya saba na ya mwisho ya waraka, ambapo ilirejelea baadhi ya misingi na kanuni zinazohusiana na utekelezaji, kama ifuatavyo:

 Kuandaa seti ya programu za dharura zitakazotekelezwa kwa
 haraka kwa ushirikiano na washirika wa maendeleo, nazo ni programu za maeneo manne yafuatayo:
 magonjwa ya kuambukiza - teknolojia ya habari na mawasiliano - kupunguza madeni - upatikanaji wa masoko.

Kupendekeza idadi kadhaa za miradi yenye umuhimu wa uhai ili kuendelea maendeleo kikamilifu kwa ngazi ya kikanda , orodha imewekwa kwa programu hii kwa msimamo wa NEPAD kwa mitandao ya intaneti.

Kuanzishwa kwa chombo cha kusimamia masuala ya NEPAD, haswa katika suala hilo, waraka huo uliweka wazi kuanzishwa kwa kamati ya utekelezaji kutoka kwa wakuu wa nchi za kiafrika yenye wakuu wa nchi kumi, ambapo mataifa mawili kwa kila kanda kutoka kanda tano Barani Afrika, pamoja na mataifa matano waanzilishi wa NEPAD: Algeria, Afrika Kusini, Nigeria, Senegal, Misri.

NEPAD inajumuisha idadi kadhaa ya vyombo vikuu na kamati husika kwake ili kuhakikisha malengo yake nazo ni:

Kamati ya Utekelezaji ya urais: 

Inajumuisha wakuu
wa majimbo matano waliochukua hatua hiyo, pamoja na wakuu wa nchi nyingine 15 zinazowakilisha jumla ya kanda tano za kijiografia za bara hilo, na nchi 4 kwa kila kanda, ambapo uchaguzi unafanyika kwa nchi za Afrika mara kwa mara kujiunga na kamati hiyo kwa kipindi cha miaka miwili, kwa kuzingatia mashauriano ya kikanda ndani ya umoja huo, kamati ina jukumu la kukuza mpango huo, kupata uungwaji mkono wa kimataifa kwa ajili yake, kuainisha sera na vipaumbele vya programu yake ya kazi na kufuatilia utekelezaji wake. utekelezaji, na kuwasilisha ripoti za mara kwa mara za kazi yake kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa AAfrika . 


Kamati ya Udhibiti:
 
Inajumuisha wawakilishi wa wakuu wa nchi wanachama wa Kamati ya Utekelezaji, huandaa mipango ya kina ya programu ya kazi na hatua ya kutekeleza mpango huo, pamoja na jukumu lake katika kusimamia mazungumzo na washirika wa maendeleo - katika ngazi ya wawakilishi binafsi. - kupata ridhaa na kuungwa mkono na Kundi la Wanane na nchi  zilizoendelea kwa juhudi.Afrika kufikia maendeleo katika Barani humo.

Utaratibu wa kudhibiti Marika wa Kiafrika:
 Inaundwa na wakuu wa nchi na serikali ambazo ni wanachama wa utaratibu huo, na Kuanzishwa kwake kunatokana na kauli ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Durban mwaka 2002, kuhusu demokrasia na utawala bora.
 Hii inamaanisha  utaratibu wa kuchagua na kutathmini utendaji wa nchi kwa nchi nyingine.Lengo la kawaida la utaratibu huo ni kusaidia nchi ambayo iko chini ya mchakato wa mapitio ili kuboresha utendaji wake wa maendeleo katika mchakato wa kufanya maamuzi na kuchagua njia bora zaidi. Na ahadi kwa viwango na kanuni zinazokubalika. Inajumuisha wakuu wa nchi na serikali ambazo ni wanachama wa utaratibu huo.Misri ilijiunga na utaratibu huo mnamo mwezi wa tatu 2004.


Sekretarieti: 
yenye makao yake mjini Pretoria, inafanya kazi kama chombo cha kiufundi ili kusaidia kamati za utekelezaji na usimamizi katika kutekeleza majukumu yao. 


Baada ya mwaka mmoja takribani,  Jumuiya ya Umoja wa kimataifa  iliunda mazungumzo ya hali ya juu kuhusu NEPAD mnamo Desemba 16, 2002, kisha mnamo Novemba mwaka huo huo, NEPAD ilipitishwa kama mfumo wa maendeleo ya Afrika, na ilitoa wito kwa vyombo vya Umoja wa Mataifa, mashirika yake maalum na washirika wengine wa maendeleo kuainisha programu zao zinazolenga kusaidia juhudi za maendeleo Barani Afrika na programu za kazi za NEPAD, na katika ufuatiliaji wa uamuzi huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatayarisha ripoti ya mara kwa mara kuhusu maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa mpango huo, kulingana na majibu anayopata kutoka kwa pande mbalimbali.

 NEPAD hufanya mikutano ya kilele ya kila mwaka kati ya wakuu wa nchi tano zilizoanzisha mpango huo, na viongozi wa nchi za kundi hilo, ulioanza tangu Mkutano wa Genoa Julai 2001, kwa lengo la kusoma njia za kuunga mkono juhudi za Afrika tekeleza mpango huo kwa vitendo.Mkutano wa Kanataskis 2002 ndio unaojulikana zaidi kati ya mikutano hii.Ulitoa kile kinachoitwa Mpango wa Utekelezaji wa Afrika kama mpango wa utekelezaji wa pamoja wa kusaidia utekelezaji wa NEPAD.

Mbali na mikutano ya mara kwa mara inayowajumuyisha pamoja wawakilishi wa wakuu wa nchi wa wajumbe watano wa Kamati ya Uongozi ya NEPAD, na wawakilishi binafsi wa viongozi wa nchi za kikundi, kujadili njia za ushirikiano ili kusaidia utekelezaji wa kazi ya mpango huo. programu na kufuatilia mapendekezo na maamuzi yaliyotolewa na mkutano huo. 

Misri inatilia maanani sana NEPAD, kwa kuunga mkono mikakati na mipango yake ya kuchangia maendeleo ya bara la Afrika, kwa kuzingatia ukweli kwamba Misri ni moja ya nchi waanzilishi wa mpango huo, pamoja na nia yake ya kuhifadhi hadithi ya mafanikio ambayo NEPAD ilianza kama alama ya tofauti katika masuala na juhudi za maendeleo ya Afrika, kupitia jukumu lake Nguzo kuu katika kuongeza ushirikiano na ushirikiano kati ya nchi za Afrika ili kukabiliana na matatizo ya bara la kuongezeka kwa umaskini na viwango vya chini vya maendeleo ndani yake, na Misri ina ufanisi na ufanisi. jukumu kuu katika kuunda programu za maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika, ambayo ilijumuishwa katika ushiriki wake katika kuzindua na kuunga mkono mpango wa NEPAD, hadi ikawa chombo kikuu cha Afrika kuwasilisha changamoto za maendeleo ya bara hilo katika viwango vya Afrika na kimataifa.


Mnamo  Mei mwaka wa 2017, mkutano wa pili wa NEPAD ulizinduliwa, uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini Misri kwa kushirikisha nchi 17 za Afrika.

 Mnamo Septemba 2018, Ushirikiano Mpya wa Maendeleo ya Afrika (NEPAD) uliiheshimu Misri ndani ya mfumo wa shughuli za Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya; kwa kushukuru juhudi za Misri katika nyanja ya mazingira barani Afrika wakati wa uongozi wa Misri wa mkutano huo kuanzia 2015 hadi 2017. 

Mnamo Februari 2023, Misri ilishika nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (NEPAD) kwa kipindi cha miaka miwili, kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame, kwa ridhaa ya wajumbe wa kamati hiyo kuunga mkono ugombea wa Misri. Hayo yamejiri wakati wa ushiriki wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, kwa njia ya video conference, katika kazi ya kikao cha 40 cha Kamati ya Uongozi ya Wakuu wa Nchi na Serikali ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (NEPAD), kilichofanyika kwa ushiriki wa Marais wa nchi na serikali za Afrika, wajumbe wa kamati hiyo. 

Vyanzo


Tovuti ya Urais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.
Tovuti ya Taasisi kuu ya Taarifa.