Misri na Nyumba ya Afrika kwa miaka 55 kati ya mwendelezo na mabadiliko (2)

Misri na Nyumba ya Afrika kwa miaka 55 kati ya mwendelezo na mabadiliko (2)

Imefasiriwa na / Alaa Zaki

Afrika baada ya Gamal Abdel Nasser

Baada ya Urais wa kwanza wa Misri kwa Umoja wa Afrika - uliokuwa zamani Jumuiya ya Umoja wa Afrika - katika mwaka wa 1964, sera ya mambo ya nje ya Misri iliendelea jukumu lake la kikanda kuelekea bara letu. Na uungaji mkono wa Misri kwa Umoja wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika uliendelea mnamo wa enzi ya "Rais El-Sadat", na wakati huo Misri ndiyo ilikuwa nguzo ya kuendelea mazungumzo ya kilele cha Kiarabu-Kiafrika mnamo mwaka wa 1977. 
Na diplomasia ya Misri ilifanikiwa wakati huo kuunga mkono kwa mahusiano ya Misri-Afrika na kuandaa mshikamano wa Afrika kupitia uratibu na nchi za kundi la Kiarabu-Afrika. Na ilifanya mkutano wa kwanza wa kilele wa Kiarabu-Kiafrika mnamo mwaka wa 1977, na Misri ilikaribisha nchi 65 za Kiarabu na Kiafrika nchini humo.
 Pia, tangazo la kisiasa lilitolewa kuhusu kanuni za msingi zinazotawala ushirikiano wa Kiarabu-Kiafrika, na tangazo lingine kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kifedha wa Kiafrika-Kiarabu. Vilevile, Muundo wa kitaasisi wa ushirikiano ulianzishwa ambapo ulijumuisha (Mkutano wa Kilele, Baraza la Mawaziri la Waarabu na Waafrika, kamati ya kudumu ya ushirikiano, kamati ya uratibu, na mahakama ya Kiarabu-Kiafrika ili kutumika kama chombo cha Mamlaka ya Mahakama).

Inaashiriwa kuwa mkutano wa kilele wa pili wa Kiarabu-Kiafrika ulifanyika mnamo mwezi wa Oktoba, mwaka wa 2010, huko Sirte, Libya, kwa mahudhurio ya nchi 66 za Kiarabu na Kiafrika, pamoja na kauli mbiu (kueleka ushiriki wa mkakati wa Kiarabu-Kiafrika). Kisha ilifanya mkutano wa kilele wa tatu wa Kiafrika-Kiarabu katika mwaka wa 2013 nchini Kuwait, chini ya kauli mbiu (Washirika katika maendeleo na uwekezaji), na mkutano wa kilele wa nne wa Equatorial Guinea kwa mwaka wa 2016 pamoja na kauli mbiu (Pamoja kwa ajili ya maendeleo endelevu na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Afrika na ulimwengu wa Kiarabu). Na tuko kwenye hatihati ya kufanya mkutano wa kilele wa tano wa Kiafrika-Kiarabu, uliopangwa kufanyika Riyadh, Saudi Arabia, kwa mwaka huu.

Kisha enzi ya "Rais Mubarak" ilikuja na sera tofauti iliyokuwa na sifa ya kutoegemea upande wowote katika masuala yenye changamoto, na Misri iliendelea kuunga mkono Rhodesia - sasa Zimbabwe - na Afrika Kusini katika kesi zao za kukabiliana na ubaguzi wa rangi, na inatajwa hapa kuwa "Mandla" alichagua Misri kama nchi ya kwanza ili kuitembelea baada ya kuachiliwa baada ya kukaa Takriban miaka 27 katika jela kwa tuhuma za kuchochea ghasia na kula njama pamoja na nchi za kigeni na inatajwa pia ukarimu ambao Misri na watu wake walimpokea wakati huo.

Misri ilifuata sera ya kutoegemea upande wowote  mnamo wa enzi ya "Mubarak" - ambapo wakati huo huo ilikuwa sera ilifuatiwa na Jumuiya ya Umoja wa Afrika wa ili kutatua migogoro katika wakati huo - kuelekea maswala yenye changamoto kama vile mgogoro kati ya Libya na Chad, na mgogoro wa Sudan-Ethiopia kwa sababu Sudan ilikuwa mwenyeji wa Muungano wa Ukombozi wa Eritrea, ambapo kutokana na sera ya Misri ya kutoegemea upande wowote inachoafikiana na kanuni ya Umoja wakati huo ni kwamba Misri ilitwala uongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika mara mbili: mara moja mnamo mwaka wa 1989 na tena mnamo mwaka wa 1993.