Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

Imefasiriwa na / Zeinab Abd ElMohsen Mekky

Ingawa wito wa Umoja wa Kiarabu umetolewa tangu  karne kadhaa, ila wazo la kuanzisha Shirika moja la Kiarabu linalounganisha nchi za Kiarabu halikuwa wazi hadi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia kutokana na idadi kubwa za mabadiliko ya kiarabu, ya kikanda na ya kimataifa. 

Katika ngazi ya kiarabu, inawezekana kusema kwamba ukweli wa kiarabu ulikuwa msingi wa maendeleo hayo ya kihistoria. 
Kwa upande mmoja, vita vilikuwa vinafaa vya ukuaji wa harakati za kitaifa na shughuli za upinzani dhidi ya uwepo wa ukoloni, jambo  ambalo lilionekana katika uhuru wa kuongezeka kwa idadi ya nchi za Kiarabu na liliunda hitaji la kuanzisha aina ya uwiano kati ya nguvu za kisiasa. Kwa upande mwingine, hitajio la Umoja liliimarishwa kwa ufahamu wa hatari za harakati ya Kizayuni, na wahamiaji wa kiyahudi waliingia Palestina, pamoja na jukumu la nchi iliyopewa mamlaka juu yake... "Uingereza", kutimiza ndoto ya taifa la Kiyahudi. Kwa upande wa tatu, kuongezeka kwa msuguano kati yake na nchi za Magharibi kutokana na ufadhili wa masomo ya kielimu kulisababisha uwazi kwa baadhi ya mawazo na mikondo ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea ndani yake, ambayo kimsingi ni wazo la kitaifa. Kwa upande wa nne, ilionekana kuwa kulikuwa na kiwango cha kuridhisha cha kubadilishana biashara na harakati za watu, hasa baina ya nchi za Mashariki ya Kiarabu, kwa njia ambayo ilionekana kutoa msingi wa kimaada kwa umoja pamoja na msingi wa kiroho na kiutamaduni. 

Ama katika ngazi ya kimataifa, Vita vya Pili vya Dunia vilifuatiwa na hatua ya mpito katika kuboresha  mfumo wa kimataifa. Huko Kuhusiana na Uingereza haswa, ni muhimu katika kuchambua msimamo wake kuhusu kuanzishwa kea Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, kuweka wazi ukweli kwamba jukumu lake lilikuwa ni jukumu la nyongeza au la usaidizi, na halikuwa jukumu la kuanzisha, kwa sababu hakuna nchi, haijfikii  kiwango cha utawala wake wa kisiasa mnamo kipindi fulani cha kihistoria, inayoweza kuimarisha wazo lisilopatikana kabisa.

Waziri Mkuu wa Misri Mustafa al-Nahhas alichukua hatua hiyo na kuwaalika Waziri Mkuu wa Syria, Jamil Mardam na mkuu wa umoja wa Kitaifa ya Lebanon, Bechara al-Khoury, kuangazia pamoja  mjini Kairo kuhusu wazo la "kuanzisha Jumuiya ya Nchi za Karabu ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi za Kiarabu zibazojiunga nayo." Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa wazo la Jumuiya ya Kiarabu kuibuliwa kwa uwazi huo, kisha akarejea kuthibitisha utayari wa serikali ya Misri kuchunguza maoni ya serikali za Kiarabu kuhusu suala la umoja na kufanya mkutano wa kulijadili  wazo ambalo lilisifiwa na mtawala wa Jordan wakati huo, Prince Abdullah. Kutokana na hali hiyo, mfululizo wa mashauriano baina ya nchi hizo mbili ulianza kati ya Misri kwa upande mmoja na wawakilishi wa Iraq, Syria, Lebanon, Saudi Arabia, Jordan na Yemen kwa upande mwingine. 

Wakati kamati ya maandalizi ya wawakilishi kutoka Syria, Lebanon, Jordan, Iraq, Misri na Yemen ilipokutana (kama mwangalizi) mnamo kipindi cha kuanzia Septemba 25 hadi  Oktoba 7 mnamo mwaka 1944, ilichagua mwelekeo unaotaka umoja wa mataifa huru ya Kiarabu kwa njia ambayo haiathiri uhuru na mamlaka yake, 
 
Pia iliamua kuuita muungano unaojumuisha umoja huu "Umoja wa Nchi za Kiarabu" na kuupendelea zaidi kuuita majina "Muungano" na "Umoja",  ya kwanza inaashiria mahusiano ya kawaida na ya pili inaelezea uhusiano unaolazimisha masharti  ya marejeleo yaliyokubaliwa kuibadilisha kwa Shirika Changa la Waarabu. 

Kwa kuzingatia hilo, Itifaki ya Alexandria ilifikiwa, ambayo ikawa hati ya kwanza inayohusu chuo kikuu, ambayo iliainisha kanuni zifuatazo:

•Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kutoka miongoni mwa nchi huru za Kiarabu zinazokubali kujiunga nayo, na itakuwa na baraza ambalo mataifa yanayoshiriki katika jumuiya hiyo yatawakilishwa kwa usawa. 

•Jukumu la Baraza la Jumuiya  ni: Kuzingatia utekelezaji wa mikataba iliyofanyewa  na nchi wanachama kati yao, kufanya mikutano ya mara kwa mara ili kuimarisha uhusiano kati yao, kuratibu mipango yao ya kisiasa ya kupata ushirikiano kati yao, kuhifadhi uhuru wake  na uhuru kutoka kwa wote. uchokozi kwa njia zinazowezekana za kisiasa, na kuangalia mambo ya nchi za Kiarabu kwa ujumla

•Maamuzi ya Baraza ni ya lazima kwa wale wanaoyakubali, isipokuwa kwa hali ambazo mgogoro zinatokea kati ya nchi mbili wanachama wa Jumuiya , na pande hizo mbili hukimbilia kwenye Baraza ili kutatua mgogoro kati yao. Katika hali hizo, maamuzi ya Baraza ni ya lazima na yanatekelezeka. 

•Hairuhusiwi kutumia nguvu kusuluhisha mizozo baina ya mataifa mawili ya Jumuiya hiyo, na wala hairuhusiwi kufuata sera ya kigeni inayodhuru sera ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu au nchi zake zozote.

•Inawezekana kwa nchi zote  wanachama wa Jumuiya  kufanya makubaliano maalum na nchi nyingine ya jumuiya au zingine ambazo hazipingani na maandishi na roho ya vifungu hivi. 

•Hatimaye, kutambuliwa kwa mamlaka na uhuru wa mataifa yanayoandaa jumuiya na mipaka yake halisi. Itifaki hiyo pia ilijumuisha uamuzi maalumu kuhusu umuhimu wa kuheshimiwa uhuru na mamlaka ya Lebanon, na uamuzi mwingine kuhusu Palestina kama nguzo muhimu ya nchi za Kiarabu na haki za Waarabu ndani yake ambayo haiwezi kuathiriwa bila kuathiri amani na uhuru katika nchi hiyo ulimwengu wa Kiarabu, na nchi za Kiarabu lazima ziunge mkono harakati za Waarabu wa Palestina kwa kufikia matarajio yao halali na kulinda haki zao .

•Hatimaye, itifaki ilisema kwamba (kuundwa kwa kasi kamati ndogo ya kisiasa  kutoka kwa wajumbe wa kamati ya maandalizi iliyotajwa hapo juu ili kuandaa rasimu ya mfumo wa Baraza la Jumuiya, na kuangazia masuala ya kisiasa ambayo makubaliano yanaweza kufanywa kati ya nchi za Kiarabu). 

Itifaki hii ilitiwa saini na wakuu wa wajumbe wanaoshiriki katika Kamati ya Maandalizi mnamo tarehe Oktoba 7,1944 , isipokuwa Saudi Arabia na Yemeni, ambazo zilitia saini mnamo Januari 3, 1945 , na Februari 5 ya mwaka huo huo, mtawalia, baada ya kuwasilishwa kwa Mfalme Abdulaziz Al Saud, na Imamu Yahya Hamid.

Itifaki hiyo iliwakilisha waraka kuu kwa msingi ambao Mkataba wa jumuiya ya nchi za kiarabu uliundwa.Kamati ndogo ya kisiasa, ambayo ilipendekezwa na Itifaki ya Alexandria, na wajumbe wa nchi za Kiarabu zilizotia saini Itifaki ya Alexandria walishiriki katika maandalizi yake, pamoja na mwakilishi mkuu kutoka Saudi Arabia na Yemen, na mwakilishi wa vyama vya Palestina alihudhuria kama msimamizi Baada ya kukamilika kwa rasimu ya mkataba kama matokeo ya mikutano kumi na sita iliyofanywa na vyama vilivyotajwa hapo juu katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri kati ya Februari 17 na  Machi 3 ya mwaka wa 1945 , mkataba huo ulidhinishwa katika Saffron Palace huko kairo mnamo tarehe kumi na tisa ya mwezi huo huo baada ya kufanya marekebisho kadhaa kwake.

Mkataba wa Jumuiya ulikuwa na utangulizi na vifungu ishirini, na viambatisho vitatu maalum,  kiambatisho cha  kwanza ni kinahusiana Palestina na ilijumuisha uteuzi wa baraza la jumuia kama mjumbe "yaani Palestina" ili kushiriki katika kazi yake hadi kupata uhuru. Kiambatisho cha pili kinahusiana na ushirikiano na nchi za Kiarabu ambazo haziko huru na hivyo hazishiriki katika Baraza la Jumuiya. Kuhusu kuambaticho cha tatu na ya mwisho, kinahusu kuteuliwa kwa Bw. Abdel Rahman Azzam, Waziri Plenipotentiary katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa jumuia kwa  miaka miwili. Utangulizi huo ulionesha kuwa nchi husika zilikubaliana na Mkataba huo kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kiarabu ndani ya mfumo wa kuheshimu uhuru na mamlaka kwa maslahi ya nchi zote za Kiarabu.

Mnamo  Machi 22, 1945 , mkataba wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ilitiwa saini na wawakilishi wa nchi za Kiarabu, na kikao cha kutia saini kilihudhuriwa na mwakilishi wa vyama vya Palestina, na ishirini na mbili ya Machi ya kila mwaka ikawa siku ya sherehe ya kila mwaka ya jumuiya ya nchi za kiarabu.

 Kazi za pamoja za Kiarabu ndani ya mfumo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zilishuhudia mafanikio mengi katika ngazi ya kiuchumi na ya kisiasa ambayo hayawezi kupuuzwa, ambapo katika mwanzo wake, Jumuiya hiyo ilichangia kikamilifu katika kusaidia ukombozi wa sehemu kubwa za ulimwengu wa Kiarabu na kusaidia ukombozi wa nchi nyingi za Afrika na Asia.

Jumuiya pia imeshuhudia, katika historia yake ndefu, kuanzishwa  kwa mashirikisho mengi ya Kiarabu yenye ubora, kama vile Umoja wa kiarabu kwa Mawasiliano waya na yasiyo waya, na Jumuiya za Redio za Kiarabu, kutiwa saini kwa mikataba mingi kama vile Mkataba wa Umoja wa Kitamaduni wa Kiarabu na Mkataba wa  Mwalimu Mwarabu. Mikataba ya ushirikiano wa kiarabu katika nyanja nyingi, na uanzishwaji wa Mfuko wa Kiarabu cha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii, Chuo cha Kiarabu cha Usafiri wa Baharini kutoa nguvu za watu wa Kiarabu katika nyanja za urambazaji wa baharini, Mfuko wa Kiarabu wa msaada wa kiufundi kwa nchi za kiafrika, uanzishwaji wa mabaraza ya kila Mawaziri wa Mambo ya Ndani,  Mawaziri wa Nyumba na Ujenzi na Mawaziri wa Umeme wa Kiarabu, kutolewa kwa mkataba wa Haki za Binadamu wa Kiarabu na kuanzishwa kwa Mfuko wa Jerusalem na Al-Aqsa kufuatia kuzuka  Intifadha ya Al-Aqsa
Na kupitishwa kwa Mkataba wa Kitendo cha Pamoja cha Vyombo vya Habari vya Kiarabu, na shughuli zingine kadhaa, mabaraza, misimamo na maamuzi ambayo yalichangia kuendeleza hatua za pamoja za kiarabu, na ambayo Misri ilichangia kwa ufanisi.


Misri inaunga mkono juhudi za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kama chombo kikuu cha kazi ya pamoja ya kiarabu, kwa kutoa uwezo unaohitajika wa kurekebisha miundo yake na kuiwezesha kutekeleza jukumu lake kwa ukamilifu, kuhusiana na kuendeleza miundo yake iliyopo na kuongeza  miundo mpya,  kwa namna ambayo matokeo yake ni kuimarisha kazi  ya pamoja ya kiarabu, huku pamoja na  ikiimarisha uwezo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Kudhibiti migogoro hii kabla haijaongezeka kupitia taratibu za kuzuia au kuiendesha mizozo na  kuisuluhisha kwa amani.

Misri inasisitiza umuhimu wa kusonga mbele na miradi ya ushirikiano wa kiuchumi wa kiarabu na kutekeleza taratibu na sera zinazopelekea kukomboa harakati za biashara, mitaji, watu na teknolojia miongoni mwa nchi za Kiarabu, pamoja na  kuthibitisha mchango wenye tija katika maendeleo ya uchumi wa kiarabu na kujenga miradi ya pamoja. Na kuboresha nafasi za uwekezaji wa pamoja, ambayo hatimaye itasababisha kuanzishwa kwa soko la Kiarabu na la pamoja linalotarajiwa.

Marekebisho ya mfumo wa kiarabu yanahitaji kufikia dhana ya umoja ya usalama wa pamoja wa kiarabu, asili ya vitisho vinavyoelekezwa kwake na hatua zinazohitajika za kuulinda, na kuchunguza njia za kuamsha makubaliano na mifumo ya ushirikiano wa pamoja wa kiarabu katika nyanja zote. Katika muktadha huo, Misri inatilia umuhimu mkubwa wa ushirikiano wa pamoja wa kiarabu katika nyanja za sayansi, teknolojia, elimu na utamaduni, na vile vile kuendeleza uhusiano wa nchi mbili za nchi za Kiarabu katika nyanja hizo, pamoja na ikikubali kwa taratibu na uteuzi kama njia ya kuweka michakato ya maendeleo na kurekebisha katika vitendo, kwa kuzingatia hali ya kila nchi.

Kuboresha na kuendeleza kwa uhusiano wa kiarabu pamoja na nguvu zote kuu kimataifa, kikanda, mashariki na magharibi (Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Urusi,  Uchina, Japan, India, Brazil, Afrika Kusini, Jumuiya ya ASEAN ... n.k.) husaidia kuunda kipimo cha uwiano katika kukabiliana na Changamoto zinazowekwa na hali ya sasa ya kimataifa, na kufaidika na   fursa mbalimbali za usaidizi ambazo mamlaka haya yanaweza kutoa.

Kwa kuzingatia malengo hayo, mnamo Julai 2003, Misri iliwasilisha mpango wa kuendeleza Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kuamsha hatua ya pamoja ya kiarabu, Pia iliunga mkono maamuzi ya Mkutano wa kilele cha kiarabu uliofanyika Tunis mwaka 2004 kuhusu mageuzi ya kiarabu, na ilishiriki katika juhudi zote zilizolengwa kuleta mageuzi na kuboresha kazi za pamoja za Waarabu na taasisi zake.

 Mkutano wa kilele wa kiarabu, uliofanyika katika mji mkuu wa Saudi, Riyadh, mnamo Machi 28-29, 2007, ulikaribisha katika taarifa yake ya mwisho ajenda ya kazi ya Misri ambayo iliwasilisha kwenye mkutano huo,  Inazunguka taratibu za kutekeleza dhana kuu ya usalama wa taifa la kiarabu kwa kuzingatia changamoto za sasa, jinsi ya kuamsha usalama wa taifa la kiarabu na kuilinda dhidi ya uvamizi wa nje kupitia lango la migogoro ya ndani na ya kikanda katika eneo.

 Misri ilishiriki katika mikutano mingi ya kilele ya Kiarabu iliyoshikilia kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo mnamo Machi 1945 hadi 2022.

•Mkutano wa Dharura wa Anshas "Mei 1946" ulifanyika kwa mwaliko wa Farouk, Mfalme wa Misri kwa uwepo wa nchi saba waanzilishi wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu, ambazo ni Misri, Jordan ya Mashariki, Saudi Arabia, Yemen, Iraq, Lebanon na Syria. Ilithibitisha haki za watu wa Kiarabu kupata uhuru wao na ikataka kukomesha uhamiaji wa kiyahudi kwenda Palestina.Pia iliamua kuilinda Palestina katika tukio la shambulio dhidi yake.

 •Mkutano wa dharura wa Beirut "Novemba 1956" ulifanyika kufuatia uchokozi wa pande tatu dhidi ya Misri na Ukanda wa Gaza, ambapo marais tisa wa Kiarabu walishiriki, ilitaka kusaidia Misri dhidi ya uchokozi huo, pamoja na uthibitisho wa mamlaka yake juu ya Mfereji wa Suez kwa mujibu wa mkataba wa 1888, na kanuni sita zilizoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  Oktoba 13, 1956.

•Mkutano wa Kairo "Januari 1964" ulikuwa ni mkutano wa kwanza wa kiarabu wa kawaida kwa mwaliko wa hayati Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser kujadili mradi wa Israeli wa kugeuza maji ya Mto Jordan, ulihudhuriwa na nchi zote kumi na tatu wanachama wakati huo.

• Mkutano wa kilele wa Alexandria "Septemba 1964", na ulifanyika Alexandria mbele ya viongozi 14 waarabu, mkutano huo ulitoa wito wa kuimarishwa kwa uwezo wa kiulinzi wa kiarabu, na kukaribisha kuanzishwa kwa Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina na kupitishwa kwake kama mwakilishi wa Wapalestina. watu. Pia ilitoa wito wa ushirikiano wa kiarabu katika nyanja ya utafiti wa atomiki ili kutumikia malengo ya amani, na pia katika nyanja za kiuchumi, kitamaduni na vyombo vya habari.

•Mkutano wa Casablanca "Septemba 1956" ulihudhuriwa na nchi 12 za Kiarabu pamoja na Jumuiya ya Ukombozi ya Palestina.

• Mkutano wa kilele wa Khartoum "Agosti 1967" ulifanyika baada ya kushindwa mnamo 1967 , au kile kilichojulikana kama kurudi nyuma, kutambuliwa kama Mkutano wa kilele wa "Hapana mara tatu " ambazo zilielekezwa kwa Israeli, 
hakuna upatanisho, hakuna mazungumzo, na hakuna utambuzi,  Ilihudhuriwa na nchi zote za Kiarabu isipokuwa Syria.

•Mkutano wa Rabat "Desemba 1969" ulihudhuriwa na nchi 14 za Kiarabu na kutoa wito wa kukomesha mchakato za kijeshi huko Jordan kati ya wapiganaji wa Palestina na vikosi vya jeshi la Jordan na kuunga mkono kwa mapinduzi ya Palestina. 

•Mkutano wa dharura wa Kairo "Septemba 1970" ulifanyika kufuatia mapigano ya silaha huko Jordan kati ya mashirika ya Palestina na serikali ya Jordan, ambayo yalijulikana kama matukio ya Black September, Syria, Iraq, Algeria na Morocco zilisusia mkutano huu.

Mkutano wa Algeria "Novemba 1973" ulifanyika kwa uwepo wa nchi 16 kwa mwaliko wa Syria na Misri baada ya vita vya Oktoba 1973, na kususiwa na Libya na Iraq, mkutano ulishuhudia kujiunga kwa  Mauritania kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

•Mkutano wa Rabat "Oktoba 1974" ulifanyika kwa ushiriki wa nchi zote za Kiarabu, pamoja na Somalia, ambayo ilishiriki kwa mara ya kwanza.

•Mkutano wa dharura wa Riyadh "Oktoba 1976" ulifanyika kwa mwaliko wa Saudi Arabia na Kuwait ili kujadili mgogoro wa Lebanon na njia za kuutatua, ulijumuisha Saudi Arabia, Misri, Kuwait, Syria, Lebanon na Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina. 

•Mkutano wa kairo "Oktoba 1976" ulihudhuriwa na nchi 14 kukamilisha mjadala wa mzozo wa Lebanon ulioanza katika Mkutano wa Vyama Sita huko Riyadh. 

•Mkutano wa kilele wa dharura wa Casablanca, Mei 1989, uliirejesha Misri uanachama katika Jumuiya ya kiarabu, na Lebanon haikuhudhuria, ambapo serikali mbili zilikuwa zikipigania mamlaka.

•Mkutano wa dharura wa Baghdad "Mei 1990", ambapo Lebanon na Syria hazikuwepo, ulijadili vitisho kwa usalama wa taifa la kiarabu na kuchukua hatua zinazohitajika dhidi yao, Pia ulilaani kukithiri kwa uhamiaji wa kiyahudi nchini Israel. 

•Mkutano wa dharura wa Kairo "Agosti 1990" ulifanyika kufuatia uvamizi wa Iraq katika ardhi ya Kuwait, na Tunisia haikuhudhuria.

•Mkutano wa dharura wa Kairo "Juni 1996" ni mkutano wa kipekee baada ya kufikia kwa Yamen, inayoongozwa na Benjamin Netanyahu kuingia madarakani nchini Israel na hatima ya mchakato wa amani, ulihudhuriwa na nchi zote za Kiarabu isipokuwa Iraq.

• Mkutano wa dharura wa Kairo "Oktoba 2000" ulifanyika kufuatia matukio ya vurugu yaliyozuka dhidi ya Wapalestina baada ya Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon kuingia kwenye Mtakatifu wa Yerusalemu, mkutano huo ulihudhuriwa na marais 14 wa Kiarabu, wafalme na vifalme, ujumbe wa kidiplomasia unaoiwakilisha Libya ulijiondoa siku ya pili ya mkutano huo.

•Mkutano wa Amman "Machi 2001" ulihudhuriwa na viongozi 14 wa Kiarabu na kusisitiza kuzingatiwa kwa kukata uhusiano na nchi ambazo zinahamisha balozi zao kwenda Jerusalem au kuutambua kama mji mkuu wa Israeli.

• Mkutano wa kilele wa Beirut "Machi 2002" ulikuwa mmoja wa mikutano muhimu katika historia yake, ambapo ulipitisha mpango wa Mrithi wa Kifalme wa Saudi wakati huo, Abdullah bin Abdulaziz kuhusu mzozo wa Waarabu na Israeli, na ulihudhuriwa na marais 9 wa Kiarabu.

•Mkutano wa kilele wa Sharm El-Sheikh "Machi 2003" ulioongozwa na Mfalme Hamad bin Isa Al Khalifa, Mfalme wa Ufalme wa Bahrain, na kupitisha msimamo wa umoja wa kukataa kufanyaa shambulio la Amerika huko Baghdad kwa kuhudhuria viongozi 11 wa Kiarabu na wawakilishi 11 wa serekali zilizobaki.

 •Mkutano wa kilele wa Tunis "Mei 2004" kwa uwepo wa marais 13 na wawakilishi 9 wa serikali za Kiarabu, ambapo viongozi walikubaliana kuanzisha marekebisho ya Mkataba wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Kwa mara ya kwanza tangu 1945, viongozi wa Kiarabu walifanya  kuahidi "kihistoria" kuzindua marekebisho,  walisisitiza umuhimu wa mpango wa kiarabu na ramani ya barabara iliyochorwa na Quartet kwenye Mashariki ya Kati, na kulaani ukuta wa kujitenga katika Ukingo wa Magharibi, na kusisitiza kukataa kuwapa Wapalestina makazi.

•Mkutano wa Algeria "Machi 2005" ulihudhuriwa na watawala 13 wa Kiarabu, na "Tamko la Algeria" lilitolewa, ambapo viongozi wa Kiarabu walisisitiza haja ya kuamsha mpango wa amani wa Kiarabu, ambao ulikataliwa na Israeli siku hiyo hiyo. 

•Mkutano wa kilele wa Khartoum "Machi 2006" uliohudhuriwa na viongozi 11 na kubali kuanzishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Kiarabu, ulipitisha taarifa ya kuifanya Mashariki ya Kati kuwa eneo lisilo na silaha za maangamizi makubwa na kukataa mpango wa Ehud Olmert wa kuchora mipaka na maeneo ya Palestina kutika upande mmoja. Ilielezea uungaji mkono wake kwa Sudan katika suala la Darfur na kutoa msaada wa kifedha kwa vikosi vya Umoja wa Afrika huko Darfur.

•Mkutano wa kilele wa Riyadh "Machi 2007" ulihudhuriwa na viongozi 17 wa Kiarabu, mkutano huo uliamua tena kuamsha mpango wa amani wa kiarabu miaka mitano baada ya kuzinduliwa, na kuitaka Israeli kuukubali.

• Mkutano wa kilele wa Damascus "March 2008" ulihudhuriwa na viongozi 11 na kutoa wito wa kuondokana na tofauti za kiarabu, Dkt.Mufid Shehab,Waziri wa Mambo ya Sheria na Mabaraza ya Bunge alishiriki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri.

•Mkutano wa kilele wa Doha "Machi 2009" ulihudhuriwa na viongozi 17 na kukataa uamuzi wa mahakama ya jinai iliyotoa ajenda ya kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar Al-Bashir, ambapo Dk. Mufid Shehab, Waziri wa Masuala ya Sheria na Mabaraza ya Bunge, alishiriki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri. 

•Mkutano wa Sirte "Oktoba 2010" ulifanyika kwa kushirikisha watawala 15 na kutaka mpango wa utekelezaji wa kiarabu kuokoa Jerusalem na kuhifadhi Msikiti wa Al-Aqsa, ambapo Dkt. Ahmed Nazif alishiriki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri, Rais Hosni Mubarak. 

•Mkutano wa Baghdad "Machi 2012" ulifanyika kwa uwepo wa viongozi 9 na kupitisha maono ya kina ya mageuzi katika ulimwengu wa Kiarabu, ambapo Muhammad Kamel Amr, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, alishiriki kwa niaba ya Field Marshal Muhammad Sayyid Tantawi. 

•Mkutano wa Doha "Machi 2013", ambapo marais 15 walishiriki, uliidhinisha kuanzishwa kwa Mahakama ya Kiarabu ya Haki za Kibinadamu na kuanzishwa kwa mfuko wa "Msaada kwa Jerusalem".

•Mkutano wa Kuwait "Machi 2014" ulihudhuriwa na viongozi 13 wa Kiarabu, wakiwemo wafalme, vifalme na marais, ni mkutano wa kwanza wa kilele wa Waarabu uliofanyika nchini Kuwait tangu kujitoa rasmi kwa Jumuiya ya kiarabu mnamo Julai 20, 1961.

Mkutano wa Sharm El-Sheikh  "Machi 2015", na ulifanyika kwa kushirikisha viongozi 15 wa kiarabu, na kuidhinisha kuundwa kwa jeshi la pamoja la kiarabu, mkutano wa kiarabu uliozinduliwa katika Sharm El-Sheikh mwaka 2015, ni mkutano wa kwanza uliohudhuriwa na Rais Abdel Fattah El-Sisi, mwakilishi wa Misri, ndani ya mwisho wa mkutano, Rais Abdel Fattah El-Sisi, alipitisha kanuni ya kuanzisha kikosi cha pamoja cha kijeshi cha kiarabu, ambapo timu ya kiwangu cha juu inaundwa ili kusoma nyanja zote za uanzishwaji wake.

•Mkutano wa Nouakchott "Julai 2016" ulifanyika mbele ya watawala 7, na iliamuliwa kuunganisha mkutano wa kilele wa kiuchumi na kijamii wa kiarabu na mkutano wa kawaida wa kiarabu kuwa mara moja kila baada ya miaka 4, Rais Abdel Fattah El-Sisi aliteua Sherif Esmail, Waziri mkuu wakati huo ili kuongoza ujumbe wa Misri kupitia kikao 27 cha mkutano wa kiarabu iliofanyika katika mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott.


 •Mkutano wa Amman  "Machi 2017", ambapo watawala 15 walishiriki na kuzitaka nchi za dunia kutohamishia balozi zao Jerusalem au kuutambua kuwa mji mkuu wa Israel, Rais Abdel Fattah El-Sisi alisisitiza wakati wa ushiriki wake juu ya hatari ya ugaidi ambayo inakabiliwa na taifa la Kiarabu, akisisitiza wakati wa hotuba yake katika mkutano wa kilele haja ya kufikia suluhisho la kisiasa nchini Syria Kukataa kuingilia kijeshi, kuangazia migogoro ya Syria na Libya.

•Mkutano wa kilele wa Al-Zahran Saudi Arabia "Aprili 2018", mkutano wa kilele wa kiarabu ulizinduliwa ili kujadili njia za kuimarisha njia za hatua za pamoja za kiarabu na kushughulikia changamoto na vitisho vinavyolikabili eneo la Kiarabu, ambapo Rais Abdel Fattah El-Sisi aliongoza ujumbe wa Misri katika kazi za kilele, akisisitiza kwamba usalama wa taifa wa kiarabu unakabiliwa na changamoto hzijawahi kushuhudiwa, akisisitiza kuwa tunahitaji mkakati wa kina kushughulikia vitisho vilivyopo vya usalama wa kitaifa.

•Mkutano wa kilele wa Makkah Al-Mukarramah "Mei 2019", Baraza la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu lilifanya kikao katika ngazi  ya kilele, kujadili madhara makubwa ya shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa kigaidi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kwenye vituo viwili vya kusukuma mafuta katika Ufalme wa Saudi Arabia, na shambulio walilofanya kwenye meli za kibiashara katika eneo la maji la Umoja wa Falme za Kiarabu.

•Mkutano wa kilele wa Algeria "Novemba 2022". Matukio ya mkutano wa kwanza wa viongozi wa nchi za Kiarabu zilianza katika mji mkuu wa Algeria, baada ya kusimama kiliendelea takriban miaka mitatu kutokana na janga la corona, na kufuatia makubaliano ya baadhi ya nchi kurekebisha mahusiano na Israeli. Ambayo ilifanyika chini ya kauli mbiu ya "Kuungana" kwa  siku mbili, ambapo masuala kadhaa muhimu yalijadiliwa, ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula na upatanisho wa Palestina.
Ujumbe wa Misri kwenye mkutano huo uliongozwa na Rais Al-Sisi, ambaye alisisitiza katika hotuba yake hamu ya mara kwa mara ya Misri ya kuwaunga mkono ndugu, "Ninatuma ujumbe kwa watu wetu... na nasema....amini taifa letu la kiarabu... ambapo lina historia ndefu na mchango mkubwa wa ustaarabu.... taifa hilo bado lina vitu muhimu kwa mustakabali ulio imara na wenye mafanikio, jambo la kwanza ni dhamira yenu, akili zenu, na mikono yako... amini kwamba Misri itaweka macho yake daima juu ya mshikamano wa kundi la kiarabu, uhifadhi na ulinzi wake, na itakuwepo siku zote kukuunga mkono, na milango yake itaweka wazi  kwa Waarabu wote ili kutetea maisha yao ya sasa na ya vizazi vijavyo.”

Uhusiano wa Misri na Jumuiya ya nchi za Kiarabu ni wa kihistoria, tangu kabla ya kuanzishwa kwake. "Itifaki ya Alexandria" ilijumuisha  hati ya msingi ambayo Mkataba wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ulijengwa, ambayo ilitiwa saini kwa kuzingatia mashauriano yaliyoitishwa na Mustafa Al-Nahhas Pasha, ili Mkataba wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uidhinishwe katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, mwezi Machi 1945, na Katibu Mkuu wake wa kwanza, mwanadiplomasia wa Misri Abdel Rahman Azzam Pasha, na baada yake wanadiplomasia  saba wa Misri walichukua nafasi ya katibu wa chuo kikuu kati ya  wakuu wanane wa chuo hicho, nao ni (Abdul Rahman Azzam, Muhammad Abdul Khaleq Hassouna, Mahmoud Riyad, Ahmed Esmat Abdel Majeed, Amr Musa, Nabil Al-Arabi, Ahmed Aboul Gheit).

Hamna shaka kwamba kila mmoja wa wakubwa hawa alikuwa na mchango wake ambao historia haitasahau, na nafasi yake ya utangulizi katika kuimarisha nafasi ya Jumuiya ya kiarabu na kuendeleza mifumo yake ya kazi kwa kuzingatia uzoefu wake mkubwa wa kidiplomasia, pamoja na kudumisha mifumo yake ya kazi bila usumbufu, hata katika nyakati ngumu sana ambazo eneo la Kiarabu lilipitia.
 Imani ya Misri kuhusu nafasi ya Umoja wa Nchi za Kiarabu ni thabiti na haitabadilika, kwani inaamini kwamba hali ya sasa na uingiliaji wa nje katika masuala ya Kiarabu unahitaji uratibu mkubwa zaidi kati ya wanachama wa Jumuiya, uanzishaji wa mifumo ya ushirikiano  uliopo, na hata kuundwa kwa mifumo mipya inayokabiliana na changamoto, miongoni mwa mifumo hiyo ni pamoja na kikosi cha pamoja cha kiarabu kilichopendekezwa na Misri, ambacho kinalenga kuunda mfumo madhubuti wa utendaji katika kukabiliana na changamoto za asili zinazoukabili mfumo wa Kiarabu. Waarabu ni muhimu sana kwa mfumo wa pande nyingi unaowaleta pamoja kutoka baharini hadi Ghuba, haijalishi uratibu una nguvu kiasi gani katika ngazi ya pande mbili, kama vile Jumuiya ya Kiarabu na kuamsha jukumu lake imekuwa muhimu zaidi katika hatua inayofuata ya kikomo kuingiliwa kwa nje, iwe kutoka kwa nchi jirani za kikanda au kutoka kwa nguvu zingine za nje. 

Hatimaye, Misri daima imekuwa ikithibitisha nia yake ya kuunga mkono Jumuiya ya kiarabu ili kubakia kuwa nyumba ya Waarabu ambayo ndugu hukusanyika katika nyakati za shida na taabu ili kutetea maslahi ya taifa hilo la Kiarabu mbele ya hatari zinazolitishia.

Vyanzo:-

-Tovuti ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu. 

-Blogi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri. 

-Tovuti ya Taasisi Kuu ya Taarifa.