Misri na Burundi

Misri na Burundi

Tangu Rais Abdel Fattah al-Sisi ashike madaraka mnamo 2014, sera ya mambo ya nje ya Misri imeshuhudia shughuli kubwa na kufungua wigo mpya wa ushirikiano kwa mujibu wa kanuni za sera ya Misri yenye misingi ya kukuza Amani na Utulivu katika eneo la Kiarabu, kikanda na kimataifa. 

Misri na Burundi zina mahusiano imara tangu miaka 59 iliyopita, hivyo Misri ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu na Kiislamu kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja na Burundi baada ya kupata uhuru wake mwaka 1962, na miaka miwili baadaye Misri ilianzisha ubalozi wake huko, haswa mnamo Desemba 8, 1964, na mwaka wa 1962 ulikuwa mafanikio halisi ya kuwaunganisha watu wa nchi hizo mbili, hivyo  Misri iliisaidia Burundi mnamo kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 12. 

Burundi daima inasifu mwendelezo wa msaada wa Misri kwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi, vilivyodumu zaidi ya miaka 12, lakini daima kuna msisitizo juu ya haja ya kuimarisha vifungo vya ushirikiano, na kuongeza faida ya utaalamu wa Misri katika nyanja mbalimbali.

Mahusiano kati ya nchi hizo mbili hayategemei kipengele kimoja cha kisiasa au kiuchumi tu, lakini Misri na Burundi ni mfano wa kuigwa kwa pande zote. Basi kuna ziara za kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, na katika kiwango cha kiuchumi, tunaona kwamba kiasi cha kubadilishana biashara kati ya nchi hizo mbili ni takriban dola milioni moja kila mwaka. 

Mahusiano ya kuigwa kama mfano bora

Mnamo Agosti 2017 Misri ilianzisha Hospitali ya Misri na Burundi katika Mkoa wa Bururi, na serikali za nchi hizo mbili mnamo mwaka 2008 zimekubaliana kuwa Misri itaisimamia, ambapo upande wa Misri unabeba gharama za kuandaa hospitali na kutoa madaktari, wakati upande wa Burundi unachangia utoaji wa jengo la hospitali, na idadi ya madaktari wamisri katika hospitali hiyo ilifikia madaktari 20 katika taaluma mbalimbali.

Mwezi Februari 2018, Misri ilipeleka shehena ya kwanza ya msaada wa matibabu (mashine 6 za dialysis - vitengo viwili vya matibabu ya maji) kwenda Burundi; kuanzisha vituo viwili vya dialysis vya Misri vyenye thamani ya karibu Paundi za kimisri milioni 2.

Mkataba wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa Rasilimali za maji na Umwagiliaji ulisainiwa mnamo Machi 24, 2021; kutekeleza mradi wa usimamizi wa Rasilimali za maji jumuishi, unaojumuisha msaada wa kiufundi kwa ajili ya maandalizi ya utafiti wa kiufundi kwa ajili ya kuanzisha na matengenezo ya mtandao binafsi wa maji ya mvua ndani ya miji na vijiji nchini Burundi na masomo ya kiufundi kujifunza kazi ya mradi wa kupanga na kuendeleza usimamizi wa Rasilimali za maji huko Burundi. 

Chanzo:

Tovuti ya Sada Al Balad.