kumbukumbu ya Siku ya wajitolea Duniani katika Maendeleo ya Kijamii- Kiuchumi

kumbukumbu ya Siku ya wajitolea Duniani katika Maendeleo ya Kijamii- Kiuchumi
kumbukumbu ya Siku ya wajitolea Duniani katika Maendeleo ya Kijamii- Kiuchumi

Imenukuliwa na Hassan Ghazaly Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana

Wakati wa kumbukumbu ya Siku ya wajitolea Duniani katika Maendeleo ya Kijamii- Kiuchumi, nakumbuka mfululizo wa  miaka ya kufanya kazi na watu wa kujitolea, Nilikutana na vikundi vingi katika nyanja mbalimbali, Nakumbuka vizuri kila mmoja wao,nahisi Shukrani kwao.. Nilikuwa nikipata  maneno ya sifa na Shukrani nilishangaa, Yeyote kati yetu anayemshukuru mwingine, nyinyi ndio msingi, mnamo miaka hiyo, nilikuwa napata nguvu zangu kutoka kwa mapenzi yao kila barabara iliponichosha. Bado ninajivunia hadithi zao za mafanikio, ambazo ninazijua vizuri na kwa karibu, najua hazikuwa rahisi, ninathamini juhudi za kila mtu aliyefanya kazi nami kwa hiari bila malipo yoyote ya kifedha,pia nina uhakika kuwa wao ndio sababu ya mafanikio ya kila mradi tuliofanikisha pamoja. shauku yao, subira, msaada, ustahimilivu, uvumilivu, na majaribio  ndiyo yaliyofanya tofauti, thamani, na kisha mafanikio, Na hiyo ilikuwa sehemu yetu kuu kuelekea mabadiliko na kuhudumia nchi zetu.

Shukrani kwa wote waotaji ndoto ulimwengu wa furaha au wanaojaribu kuunda ulimwengu huu uwe na furaha.

Na hatimaye, “anayejitolea kufanya wema, basi ni bora kwake.”

Picha ni kutoka kwa mpango mkubwa zaidi wa kujitolea unaotekelezwa na bara la Afrika kupitia Umoja wa Afrika, kwa mahudhurio ya idadi kubwa zaidi ya watu waliojitolea kutoka Afrika zima mnamo Novemba /Desemba 2019.