Siku ya Kimataifa ya Tofauti za Utamaduni kwa ajili ya Mashauriano na Maendeleo

Siku ya Kimataifa ya Tofauti za Utamaduni kwa ajili ya Mashauriano na Maendeleo

Imefasiriwa na/ Mahmoud Ragab  
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed 

Mnamo Mwaka 2001, UNESCO ilipitisha Azimio la Ulimwengu kuhusu Tofauti za Utamaduni, na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika azimio lake la 57/249, lilitangaza Mei 21 kama Siku ya Kimataifa ya Tofauti za Utamaduni kwa ajili ya Mashauriano na Maendeleo.

Tofauti za Utamaduni ni nguvu ya maendeleo ya jamii na ni kipengele muhimu cha kupunguza umaskini na migogoro na kufikia maendeleo endelevu. Robo tatu ya migogoro mikubwa duniani ina vipimo vya kitamaduni, kwa hivyo mawasiliano ya kitamaduni ni muhimu kwa amani, utulivu na maendeleo kwa watu. Kukubalika na kutambuliwa kwa Tofauti za Utamaduni kupitia matumizi ya ubunifu, hasa ya teknolojia ya habari na habari na mawasiliano, pia huchangia mazungumzo kati ya ustaarabu na utamaduni na kuheshimiana na kuelewana.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy