Guevara wa Afrika Thomas Sankara

Guevara wa Afrika Thomas Sankara
Inawezekana kuwaua wapiganaji, lakini mawazo yao hapana. ”- miaka 34 baada ya mauaji ya Guevara wa Afrika.
Thomas Isidore Noel Sankara alikuwa kamanda katika jeshi la Burkini, na Rais wa Burkina Faso mnamo kipindi cha (1983-1987).
Thomas Sankara alizaliwa mnamo Disemba 1949 kwa familia ya kikatholiki na alijiunga katika shule ya jeshi, kama babake, aliyekuwa mpiganaji katika jeshi la Ufaransa wakati wa Vita vya Dunia vya pili.
Sankara alikuwa kiongozi wa mapinduzi na mpiganaji ,aliyepinga kwa muda mrefu dhidi ya Ubeberu na kuepuka misaada ya kigeni, na misimamo na mipango yake ya mapinduzi iliyoimarisha hali ya kujitegemea kwa watu wake ,ndiyo iliyomfanya awe ishara kwa masikini wa Afrika.

mfumo wake wa ndani ulifanikiwa kuifanya Jamhuri ya Burkina Faso iwe nchi ya kwanza ya Kiafrika kufikia kujitegemea na kuwa na akiba ya ziada wakati huo, wakati ambapo alihimiza viwanda vya ndani, alihangaika kuinua kiwango cha maisha kwa wakulima, kuondoa ushuru uliokuwa ukiwaudhia, na kurekebisha ardhi, kwa hivyo uzalishaji wa ngano na pamba uliongezeka maradufu, lililofanya nchi ijitegemee na hata iwe na ziada ya kuuza nje.
Sankara alijali elimu kwa kiasi kikubwa, kampeni za kuondoa Ujinga kote nchini, kukuza afya ya umma kwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa uti wa mgongo, homa ya manjano na ugonjwa wa Surua, na alijali faili ya miundombinu na kuanzisha reli ili kuunganisha vijiji na miji, na kila kijiji kiwe na kliniki na shule.
Sankara pia alijali haki za wanawake na akawachagua wanawake bora zaidi katika nyadhifa kuu za serikali nchini, naye anazingatiwa kuwa Rais wa kwanza katika historia ya Afrika kuzuia kutahiriwa na ndoa za utotoni.
Ana neno maarufu juu ya haki ya wanawake akisema: "Mapinduzi na Uhuru wa wanawake huenda pamoja, basi hatuzungumzii Uhuru wa wanawake kama kitendo cha hisani au kwa upande wa huruma ya kibinadamu, bali haki za wanawake ni hitaji la msingi kwa ushindi wa mapinduzi, wanawake ni nusu ya anga".
Alijulikana kama "Chi Guevara" kwa sababu ya kufanana kati yao katika haiba ya kibinafsi na ya kimapinduzi, upendo wao kwa maskini na kutatua kwa ajili yao na haki zao, mapambano yao dhidi ya Ubeberu na wafisadi, pamoja na kuwa wote wawili walianzisha mahakama za kimapinduzi kuhakimu wafisadi, kwa hivyo alisema katika hotuba juu ya kumbukumbu ya kifo cha "Guevara" na kabla Kuuawa kwake kwa muda mchache, "Guevara alikufa akiwa na umri wa miaka 39, nami sitaupitia".

Na hivyo ilivyokuwa, sera yake ya mapinduzi na misimamo yake dhidi ya Ubeberu zilimfanya adui wa Ufaransa, kwa hivyo walipanga kumwua, na mnamo Oktoba 15, 1987, aliuawa na kundi lenye silaha lililompigia risasi wakati alipokuwa akienda kwenye mkutano mmoja na kumzika kwenye makaburi. Hii ilikuwa kupitia rafiki yake "Compaore" aliyewasiliana na taasisi za kigeni juu ya ulazima wa kumwua "Sankara" anayetisha masilahi yao,basi yeye ndiye aliyetamka ukweli bila hofa na kulipa maisha yake kwa hivyo.