Siku ya kimataifa ya kukumbuka Biashara ya Utumwa na ilivyotokomezwa

Siku ya kimataifa ya kukumbuka Biashara ya Utumwa na ilivyotokomezwa

Imetafsiriwa na/ Habiba Mohammed 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Sherehe za maadhimisho ya Biashara ya Utumwa na ilivyotokomezwa zilianzia kwenye uasi huo uliotikisa ulimwengu, ambao unawakilishwa katika uasi wa watumwa dhidi ya mfumo wa watumwa mnamo Agosti 23, 1791, katika mji wa "Santo Dominigo" huko Haiti au unaojulikana kama Jamhuri ya Dominika, na maadhimisho ya maadhimisho haya kila mwaka ni fursa ya kuzingatia sababu za kihistoria, mbinu na matokeo ya janga hili, pamoja na kuchambua mwingiliano uliosababisha kati ya mabara ya Afrika, Ulaya, Amerika na Caribbean.

Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, alisema:

"Agosti 23, tunawakumbuka wanaume na wanawake walioasi dhidi ya ukandamizaji wa utawala wa utumwa huko Santo Domingo, na kufungua njia ya kuvunja nira ya utumwa, kukomesha Utumwa na kukomesha mazoea kwa msingi wa Uharibifu wa wanadamu fulani... Tuwasalimu kwa heshima wahanga wote wa biashara ya watumwa weusi tunapowakumbuka wanamapinduzi hao leo."

UNESCO ilizindua mradi wa Utumwa: Upinzani, Uhuru na Urithi mwaka 1995 kama chombo cha kimataifa kinachoelezea matokeo na mwingiliano wa biashara ya utumwa na utambuzi wa maeneo, majengo na maeneo yaliyokuwa kitovu cha biashara hii, pamoja na kutafuta njia za kukuza uhusiano kati ya watu karibu na sheria za kawaida zinazotokana na janga hili lililowakabili watu kwenye nyakati za kale.

Kwa barua ya 29 Julai 1998 Na. 3494 kwa Mawaziri wa Utamaduni, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO aliwaalika nchi zote wanachama kuandaa matukio ya kila mwaka kwa kuadhimisha Siku ya kimataifa ya kukumbuka Biashara ya  Utumwa Nyeusi na ilivyotokomezwa mnamo 23 Agosti, na Bodi ya Utendaji ya UNESCO ilipitisha azimio 29 / 40 kwenye kikao chake cha ishirini na tisa, Siku ya kimataifa ya kukumbuka Biashara ya  Utumwa Nyeusi na ilivyotokomezwa

Mnamo Desemba 2017, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza Agosti 23 kuwa siku ya kimataifa ya kuwakumbuka wahanga wa utumwa na biashara ya utumwa wa Bahari ya Atlantiki, kwenye jaribio kubwa na kazi isiyo na kuchoka inayosababisha kutokomeza aina zote za udhalimu wa kijamii ulioachwa na historia ya utumwa, na kwenye juhudi za kupambana na aina zote za ubaguzi na ubaguzi wa rangi.

Kutambuliwa kwa UNESCO kwa eneo la akiolojia la gati ya bandari ya "Valongo" mwaka 2015 kama eneo la kumbukumbu ya biashara ya utumwa iliyoanzia mwaka 1811, ni moja ya juhudi muhimu katika kuandika jeni za suala hili, kwani Brazil ilidhibiti biashara ya utumwa kwa zaidi ya karne tatu kuanzia (1560-1850) na biashara ya utumwa ilikatazwa kabisa na sheria mwaka 1843, wakati ilikuwa nchi ya mwisho kuacha biashara ya utumwa mwaka 1888 huko Amerika, hivyo bandari ya Valongo ilihusishwa na mradi wa UNESCO unaoitwa "Slave Route:  Upinzani, Uhuru na Urithi", ulioandikwa na UNESCO kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia mnamo Julai 2017 kwa lengo la kubadilisha mawe yaliyopotea kwa muda mrefu kutoka bandari ya Case Valongo Wharf kuwa mnara.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy