"Vijana na michezo" inapokea vijana wa Afrika ili kushirikiana katika Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika ".

"Vijana na michezo" inapokea vijana wa Afrika ili kushirikiana katika Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika ".
Wizara ya vijana na michezo imepokea idadi ya vijana wa nchi za kiafrika zinazoshirikiana katika Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika ", unaotolewa kwa Wizara (Ofisi ya vijana waafrika na idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia) chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuli "Waziri Mkuu", mnamo kipindi cha tarehe ya 8 hadi 22 Juni, mwaka wa 2019,kwa ushirikiano wa Shirikisho la vijana waafrika.
Na hadi sasa mjini Kairo walifikia vijana wa nchi za Sudan, Kusini mwa Sudan, Ruwanda, Zambia, Gambia, Kenya, Algeria, Somalia, Ghana, Nigeria, Kusini mwa Afrika, Liberia, Nambia, na Uganda, na Wizara inaendelea kuwapokea vijana wanaoshiriki katika Udhamini.

Na katika Udhamini hushiriki vijana viongozi watendaji Mia moja toka nchi wanachama katika Umoja wa kiafrika, wenye maamuzi katika sekta ya kiserikali, makada watendaji kwenye sekta binafsi, vijana wa jamii ya kiraia, Marais wa mabaraza ya kitaifa kwa viajan, Maprofesa katika vyuo vikuu, watafiti katika vituo vya tafiti za kimikakati na kimawazo, wanachama wa vyama,na waandishi wa vyombo vya habari.
Na kesho matukio ya Programu yataanzisha kupitia ziara ya makumbusho na kaburi la Gamal Abd Elnasser pamoja na kufanya mkutano na Dokta El Sayd Flifel" Mkuu mkale wa kitivo cha tafiti na masomo ya kiafrika " kuhusu Gamal Abd Elnasser na Afrika.

Inatajwa kwamba Udhamini unazingatiwa chombo kimoja cha vyombo vya utendaji wa mpango wa (Million by 2021) ili kuwawezesha vijana waafrika milioni moja, uliotolewa kwa Kameshina ya Sayansi, Teknolojia, na Rasilimali za binadamu katika Umoja wa Kiafrika, na unalenga kuhamisha jaribio kale la kimisri la kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha makada vijana waafrika wa kimageuzi wenye mitazamo inayosawazisha na mielekeo ya urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika, na pia yenye imani ya kuhudumia malengo ya Umoja wa kiafrika kupitia ukamilifu, pamoja na kuunda mkusanyiko wa makada vijana waafrika wenye athari kubwa barani ; kupitia kuwafundisha, Uzoefu unaolazimishwa, na mitazamo ya kimikakati.