Ziara kwa Kituo cha Utamaduni cha kikopitiki cha kiorthodoksi huko Abasia katika matokeo ya siku 11 ya udhamini wa Nasser
Vijana waafrika wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kiafrika walitembelea Kituo cha Utamaduni cha kikopitiki cha kiorthodoksi huko Abasia , ikiwa ni sehemu ya shughuli za siku ya 11 ya Udhamini, kiasi kwamba walikutana na Baba Askofu Armia, Askofu Mkuu na Mkuu wa kituo hicho katika mkutano wa kichwa cha "ndani ya kulipenda Afrika ... thamani na ukaramu wa binadamu".
Kwa upande wake, Baba Askofu Armia, Askofu Mkuu na Mkuu wa Kituo hicho aliwakaribisha vijana waafrika wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser unaootolewa na Wizara ya Vijana na Michezo nchini Misri, akielezea furaha yake kwa uwepo wa mkutano huu wa Afrika. , kitu ambacho huonyesha kina cha mahusiano kati ya Misri na nchi zote za Afrika.
Katika hotuba yake wakati wa mkutano wake na vijana waafrika wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika, Anba Armia aliashiria kwamba anaiona Afrika kuwa chanzo cha heri na maendeleo kwa dunia nzima, na kwamba Misri mwaka huu ni kiongozi wa Umoja wa Afrika, na Rais El Sisi anajali sana nchi zote za Kiafrika ili kuhakikisha maendeleo kwa Watu wote wa bara hilo, akiashiria kwamba waliohudhuria leo wana bahati ya kuhudhuria mashindano ya Mataifa ya Afrika, ambayo itaanza Kairo kesho kutwa Ijumaa.
Anba Armia aliongeza kuwa sisi tuko hapa leo kufikiria mustakabali ya bara hilo, kwa hivyo nilichagua kuwa mada iwe "kumwandaa mwanadamu," na ni lazima tuzungumzie thamani na utu wa mwanadamu, kwani ana thamani kubwa sana kwa Mungu na mwanadamu ni taji la viumbe vyote.
Anba Armia alisema kuwa Rais El Sisi alitambua kwamba kutegemea vijana na mawazo yao ni muhimu na mtu lazima kujitayarisha na elimu na mawazo yasiyo ya kawida na ubunifu, na kwamba kupitia mawazo na jitihada za vijana watajenga daraja la mustakbali, akiashiria. kuwa kuwekeza kwenye akili ni mwanzo wa mafanikio katika jamii yoyote.
Anba Armia aliashiria kuwa kuna uhusiano kale kati ya Wamisri wote na kwamba viongozi wa serikali wanatawaliwa na maelewano, urafiki na ushirikiano, pamoja na kufanya mikutano kadhaa kwa maimamu na makasisi, na mikutano hiyo huondoa tofauti zote na sisi tunafanya kazi pamoja ili kuijenga nchi yetu Misri, na kuendelea kila mwanadamu huishi nchini Misri, na kwamba Rais El Sisi anaendesha nchi kwa uadilifu na hatofautishi kati ya mtu yeyote, na kwamba kinachotawala nchi yetu ni sheria inayolazimisha kila mtu.
Aliendelea, "ufanisi halisi katika uwanja wowote uanatokana na neno la "pamoja", na kuacha ubinafsi na utenganishi, na kwa mujibu haya tunapata manufaa ya jamii yote, tukitamani Bara la Afrika lingekuwa mahali pa furaha ya pamoja tunayojenga kwa mawazo na uhuru, na kwamba sisi sote kuwa sawa bila uhitilafu. Hivyo, tunaweza kumaliza vita katika bara, na kwamba kufanya kazi pamoja tutapata matokeo makubwa zaidi kuliko kufanya kazi peke yake. Anba Armia alifafanua kuwa hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi na kuishi peke yake, hata katika ngazi ya nchi haiwezekani , na tunapofanya kazi pamoja, lazima tuwe na ushirikiano na kukubalikana, na kwamba tunaleta wema, huruma na urafiki kwa jamii kupitia ujenzi wa kiroho, wa kijamii, pamoja na kusisitiza maadili ya kazi, ujenzi na kutia moyo, na kuwepo kwa mtazamo hufanana na wakti wake.
Anba Armia amesisitiza kwamba inapaswa kijana kufikia lengo lake na kuona jinsi ambayo ataifuata ili kuhakikisha lengo na kufanya juu chini pamoja na kutathmini hatua na uwezo wa kuirekebisha ili kufikia lengo,akieleza kuwa kazi yoyote inayofanyika lazima ikabiliane na matatizo, lakini lazima tufanye kazi bila kukata tamaa au Kujisalimisha, na lazima tutambue kwamba wakati wa sasa utaathiri maisha yetu ya wakati ijayo na ya vizazi wajao, na umuhiu wa kuwahifadhi watoto wetu katika bara la Afrika. kwa kuzingatia elimu na kuanzisha taasisi maalum za kutunza wabunifu katika nyanja zote.
Anba Aremia amezungumzia lazima ya kushikilia umoja wetu, na kwamba Mwafrika ndiye mtu mwenye nguvu zaidi ulimwenguni, lakini tunakosa baadhi ya kupanga, akibainisha kwamba Kituo cha Utamaduni cha kikopitiki cha kiorthodoksi huwakaribisha kila wakati ndugu kutoka bara la Afrika, na Bara letu la Afrika ni miongoni mwa mabara yote ya dunia, na kwamba kizazi cha sasa kina fursa ya kuunda mustakabali bora.
Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha kikopitiki cha kiorthodoksi alisema kwamba kuna sheria ambayo inasimamia kila mtu na kwamba Kanisa na Al-Azhar daima wamesisitizia wazo la kuishi pamoja kati ya wote, akielezea kwamba Wakiristo na Waislamu wanaishi pamoja katika nyumba moja huingia shule na vyuo hivyo hivyo, hujiunga na safu ya jeshi na polisi, na kuishi maisha ya kawaida ya pamoja katika kila jambo.
Aliendelea akisema kuwa historia inataja misimamo mengi ya kibinadamu inayoimarisha kina cha mahusiano kati ya Waislamu na Wakiristo, akieleza kuwa Rais Abd El Fatah El-Sisi alifungua mnamo Januari 6 iliyopita msikiti na kanisa kubwa zaidi barani Afrika na Mashariki ya Kati.na Rais El Sisi akiwa mwadilifu hivyo itaoneshwa kwa watu waote wa jamii, na kwamba Rais Sisi alithibitisha katika kusherehekea Laylat al-Qadr kwamba dini yake ilimfundisha kumpenda kila mtu na kujenga makanisa.
Aliashiria kwamba Wakiristo katika Misri wanahisi kuwa Usalama na Amani, na ni nchi ya watu wengi, na katika historia imepokea kundi kubwa la manabii, kama Ibrahim, , Yosefu na Mfalme Sulemani, ambaye alioa binti wa Farao,pia Jesus katika safari ya familia ya takatifu kwenda Misri, na nchi yetu ni sampuli ya Usalama ,kila mtu anapaswa kuhakikishia kuhusu hali ya wakiristo katika Misri, kwani wao hupenda nchi yao, na hufanya kazi na kuishi ndani yake, na daima mahusiano mazuri hujenga madaraja.
Alisisitiza kuwa, Kanisa la kikopitiki ni Kanisa la Kiafrika lililoanzia huko Aleskandaria na kuenea katika nchi za bara, na kwamba Kanisa la Orthodox linajumuisha askofu kutoka Eritrea, na kwamba Kanisa la Orthodox lina hospitali nchini Zambia na nyingine katika Kenya ambayo inatoa huduma zake kwa wananchi wote huko, akiashiria kuwa mwanzilishi wa Kanisa hilo nchini Misri ni Mkuu Markos.Mjumbe anatoka Libya, kwa hivyo ni Kanisa la kiafrika tangu kuanzishwa kwake.
Anba Aarmia alisema kuwa Kituo cha Utamaduni cha kikopitiki cha Orthodox kinajumuisha makumbushu ya mashahidi wa Kanisa na nchi ya Libya, ambao ni mashahidi 21 waliouawa na ISIS (kundi la kigaidi la Daaish) nchini Libya kwa kutumia utambulisho wa kidini.
Matukio hayo yalihitimishwa na ziara ya vijana waafrika walioshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika ndani ya Kituo cha kikopitiki cha Orthodox, ambacho kinajumuisha kikundi cha makumbusho ya urithi na pahali pa mashahidi wa vitendo vya kigaidi na mabomu ya kanisa na mashahidi wa ISIS. nchini Libya, pamoja na kutembelea Maktaba Kuu, ambayo inajumuisha mkusanyiko mkubwa wa vitabu katika nyanja mbalimbali za elimu.