Ziara ya kiutalii ya Vijana wa " Udhamini  wa Nasser " kwa Eneo la Piramidi

Ziara ya kiutalii ya Vijana wa " Udhamini  wa Nasser " kwa Eneo la Piramidi
Ziara ya kiutalii ya Vijana wa " Udhamini  wa Nasser " kwa Eneo la Piramidi
Ziara ya kiutalii ya Vijana wa " Udhamini  wa Nasser " kwa Eneo la Piramidi

Vijana waafrika wanaoshiriki katika " Udhamini  wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika " walitembelea Eneo la  Piramidi na Abul Hull , wakati ambapo waliangalia Eneo la Panorama ili kujua Ustaarabu wa kale wa Mafarao.

Hiyo ilikuwa ndani ya shughuli za siku ya sita ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika" uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya Afrika, Idara kuu ya Bunge na Elimu ya Uraia), kwa Ufadhili wa Dokta Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, na kwa Ushirikiano na Umoja wa Vijana wa Afrika, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 8 hadi 22 Juni 2019 katika Kituo cha Elimu ya kiraia huko Al Gazira.

Vijana waafrika walisikiliza maelezo ya kihistoria kuhusu Piramidi hizo na jinsi zilivyojengwa, pia mwishoni mwa ziara hiyo Vijana walipiga picha za kumbukumbu na kununua  vitu vya kale.

Shughuli za siku hiyo pia zilijumuisha kuandaa safari ya saa mbili ya Nile wakati ambapo Vijana wa Udhamini waliburudisha vivutio vya kupendeza vya Kairo, na zilijumuisha karamu ya chakula cha jioni iliyoambatana na muziki, maonyesho kadhaa ya sauti na kisanii, na Tanoura.

Safari hiyo ilijumuisha kikao cha jumla kuhusu Ustaarabu wa kale wa Misri, ambapo Dokta. Bassam Al-Shamaa, Mwanahistoria na Mtaalamu wa vitu vya kale vya Misri, alizungumzia Ukuaji na Historia ya Maendeleo ya Ustaarabu wa kale wa Misri, na ujenzi wa Piramidi, pamoja na kuzungumzia  sababu ya kuita Misri kwa Jina hilo, na majina mengine ambayo iliitwa mnamo  Historia.

Al-Shammaa aligusia Historia ya Nubia, nchi za Punt na Ustaarabu wake, Mahusiano ya kihistoria kati ya Misri na Afrika, na sifa muhimu zaidi za kawaida kati yao, pamoja na kuzungumzia Mamalik wa Misri walioitawala Afrika kutoka kusini, akisisitiza kuwa Afrika lilifundisha Dunia na kusini mwa Misri pamoja na Aswan, Uchumi, Biashara na Mahusiano ya kibiashara tangu zama za kale hadi zama za kisasa, akisema, "Misri ni Afrika, akizingatia nchi za Afrika kama Taifa moja".