Vijana wa " Udhamini wa Nasser "  wako kwenye Taasisi Kuu ya Uhamasishaji mkuu na Takwimu

Vijana wa " Udhamini wa Nasser "  wako kwenye Taasisi Kuu ya Uhamasishaji mkuu na Takwimu
Vijana wa " Udhamini wa Nasser "  wako kwenye Taasisi Kuu ya Uhamasishaji mkuu na Takwimu

Taasisi Kuu ya Uhamasishaji mkuu na Takwimu ilikaribisha Vijana waafrika wanaoshiriki katika " Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika " wakati wa shughuli za " Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika " uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya Afrika na Idara Kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia) chini ya Ufadhili wa Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu, mnamo kipindi cha 8 hadi 22 Juni 2019, kwa Ushirikiano na Umoja wa Vijana wa Afrika.

Katika ziara hiyo, ikiwa ni sehemu ya shughuli za siku ya kumi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika, Vijana walikutana na maafisa wa Shirika hilo ili kujua zaidi kuhusu wajibu na majukumu ya Taasisi Kuu ya Uhamasishaji mkuu na Takwimu na takwimu muhimu zaidi inayozitoa, pia kutambulisha jukumu la Taasisi katika kujenga na kuendeleza uwezo wa wafanyakazi.Mkutano huo ulihudhuriwa na Bi.Ghada Mustafa, Mkuu wa Sekta ya Takwimu za Uchumi na Uhamasishaji, na Bw.Ahmed Kamal.Mshauri wa Mkuu wa Taasisi pamoja na idadi ya Viongozi wa Taasisi

Kikao hicho kilishughulikia umuhimu wa Taasisi kwa kutoa  Maelezo na Takwimu  za kila aina pia kuchangia katika kuandaa mkakati wa kitaifa wa kuboresha Takwimu kwa kuzingatia kanuni na taratibu bora zilizokubaliwa kimataifa, pamoja na Washiriki wakuu wa Biashara, hiyo ndiyo inayozingatiwa hatua muhimu ya mwelekeo sahihi kufikia Mitazamo ya Misri 2030. 

Mkutano huo pia uligusia historia ya Takwimu nchini Misri, pamoja na ratiba ya machapisho ya Taasisi Kuu ya Uhamasishaji mkuu na Takwimu, mwongozo wa machapisho na huduma zinazotolewa nayo kwa sekta nyingi ndani ya jamii, ikiwa ni Mtafiti, Mfanyabiashara, Mashirika ya kimataifa, Mashirika ya ndani na vyombo vingine ili kuwasaidia kuchukua uamuzi sahihi.

Mkutano huo ulijumuisha uwasilishaji wa ufuatiliaji wa viashirio vya malengo ya Maendeleo Endelevu,pia mitazamo ya kimsingi ya malengo ya Maendeleo Endelevu, pamoja na sura tofauti za kukaribiana kati ya malengo ya Maendeleo Endelevu na mihimili ya mkakati wa Misri wa 2030, pamoja na kufafanua mifumo ya kitaifa ya Takwimu kwa Maendeleo Endelevu na jukumu la Taasisi katika ufuatiliaji wa viashirio vya kufikia Maendeleo nchini Misri, na ulihitimishwa kwa matembezi ndani ya Taasisi ili kujua zaidi kuhusu sekta zake mbalimbali na jukumu lake kwa Vijana waafrika wanaoshiriki katika  Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika".