Waziri wa vijana na michezo : tunahangaika ili kuunganisha Michezo pamoja na Elimu na Afya, na kuhamisha uzoefu wetu wa kimichezo kwa nchi za Afrika.

Waziri wa vijana na michezo : tunahangaika ili kuunganisha Michezo pamoja na Elimu na Afya, na kuhamisha uzoefu wetu wa kimichezo kwa nchi za Afrika.
Leo Waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy alikutana na vijana waafrika washiriki katika Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "na hayo kupitia matukio ya Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika " uliotolewa kwa Wizara ya vijana na michezo (Ofisi ya vijana waafrika, Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia) chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuly "Waziri mkuu", mnamo kipindi cha 8 hadi 22 Juni 2019, kwa kushirikiana na Shirikisho la vijana waafrika.
Na mkutano huo ulijadili "Ufadhili wa Misri kwa Ajenda ya Afrika 2063 " ulihudhuriwa na Dokta Hala Elsaid "Waziri wa Upangaji, Marekebisho ya kiidara", Dokta Howaida Barkat"Rais wa taasisi ya maendeleo endelevu kwenye Wizara ya Upangaji " na hayo yalitokea miongoni mwa matukio ya siku ya kumi toka Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika " katika kituo cha Elimu ya kiraia kwenye Aljazira.
Pia Dokta Sobhy alifafanua umuhimu wa Michezo ikizingatiwa upande mmoja wa mapato ya kitaifa, akiashiria kwa Shime ya Wizara ya vijana na michezo kwa kuboresha Michezo ili kuiwezesha Misri kushindana kwa kiwango cha kimataifa kupitia kuunganisha Michezo na nyanja zote kama Afya, Elimu na nyingine, na kuifanya kama njia ya Uwekezaji na kazi hapa nichini Misri na katika nchi zote za kiafrika, akiashiria kwamba Wizara inatia juhudi ili kuiweka Michezo ndani ya taasisi ya kielimu, pamoja na kufunza njia ya kutoa na kuhamisha uzoefu na huduma zetu katika uwanja wa Michezo kwa nchi za kiafrika nyingine sawa na kupitia kutekleza programu za kimafunzo na kuhamisha Sayansi za kimichezo kwa maada za kielimu katika nchi zote za bara la kiafrika.
Na Dokta Ashraf Sobhy "Waziri wa vijana na michezo" alithibitisha kuzingatia toka uongozi wa kimisri kwa kuongeza juhudi za taasisi zote na vyombo vya taifa kwa Afrika, inayoelezea Imani yake kwa nguvu na uwezo wa vijana wake, akiashiria kwa Shime ya Wizara ya Vijana na michezo ili kutekleza programu kadhaa, harakati, na matukio yanayounganisha Misri na bara la kiafrika, kukitekleza yaliyotangazwa na Rais wa Jamhuri Abd Elfatah Elsisi, na Rais wa Umoja wa kiafrika kwa Aswan ni mji mkuu wa vijana waafrika.

Na Sobhy aliashiria kwamba Wizara ya vijana na michezo inaendelea katika ushirikiano wa vijana kati ya Misri na nchi zote za kiafrika, akionyesha kwamba Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika " utakuwa mwanzo wa Ushirikiano huo na maendeleo ya mikutano ya vijana wa nchi za kiafrika ili kuunda Mustakbali ya Afrika na kusonga mbele kuelekea kuhakikisha maendeleo endelevu 2063.
Waziri wa vijana na michezo alithibitisha kwamba Misri inaandaa ili kupokea Kombe la mataifa ya kiafrika, inayozingatia changamoto mkubwa zaidi kwa Misri, akiashiria kwa juhudi zinazotolewa ili kuwakilisha Misri kwa Bara la kiafrika kwa sura inayofaa katika tukio kubwa la kimataifa kama hili.
Ambapo Sobhy aliwaomba vijana waafrika kuwasiliana pamoja na kuendelea ushirikiano wao katika matukio kama haya yanayojumuisha vijana wa nchi za kiafrika kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na maoni yao pamoja .