Misri na Rwanda zashirikiana katika uwanja wa mabadiliko ya kidijitali na kukuza Ujasiriamali

Misri na Rwanda zashirikiana katika uwanja wa mabadiliko ya kidijitali na kukuza Ujasiriamali

Dkt. Amr Talaat, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, alikutana na Bibi Paula ingabiri, Waziri wa Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na uvumbuzi nchini Rwanda, kutafutia kukuza Ushirikiano katika nyanja za Mawasiliano na Teknolojia ya habari, haswa zile zinazohusiana na mabadiliko ya kidijitali , uvumbuzi, Ujasiriamali na Posta. Hayo yalikuja  pembezoni mwa Ushiriki wa Dkt. Amr Talaat katika mkutano wa Dunia kwa Simu za mkononi huko Barcelona.

Mkutano huo ulijadili masuala ya Ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika nyanja za uvumbuzi, Ujasiriamali ,mafunzo ya kiufundi na kuunda makada wa Rwanda katika nyanja mbalimbali za kiufundi; Katika muktadha huo, Dkt. Amr Talaat alionesha mipango ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuandaa wenye Ufanisi wa kidijitali katika nyanja mbalimbali za Teknolojia; akieleza kuwa Chuo Kikuu cha habari cha Misri kilianzishwa ili kuunda kizazi cha wataalamu wa habari;ambapo kuangalia kikamilifu suala la kuwaalika wanafunzi wa Rwanda kusoma huko Chuo Kikuu.

Pande hizo mbili zilijadili njia za kusaidia Ushirikiano katika uwanja wa Teknolojia ya habari kwa kupeleka jumbe za kuchunguza Soko la Teknolojia ya habari na Mawasiliano la Rwanda ili kutambua nafasi zinazopatikana kwa makampuni ya Misri kuwasilisha bidhaa zao. pia Ushirikiano katika uwanja wa mabadiliko ya kidijitali na kuandaa fomu muhimu kwa ajili ya uanzishaji na uongozi wa miji bora zaidi , pia mkutano umejadili wazo la kutumia utaalamu wa Misri katika kuendeleza Posta na huduma zake mbalimbali za kuiwezesha Posta ya Rwanda kutekeleza mipango ya kisasa.