Eneo la Piramidi za Giza Lakaribisha  Washiriki wa Shindano la " Mwenye mitindo bora zaidi Duniani" 

Eneo la Piramidi za Giza Lakaribisha  Washiriki wa Shindano la " Mwenye mitindo bora zaidi Duniani" 

Leo, Eneo la Piramidi za Giza lilikaribisha,  washiriki wa shindano  la " Mwenye mitindo bora zaidi Duniani" " Top model of the world", na ujumbe uliofuatana nao, ambapo shindano hilo linafanyika nchini Misri katika kipindi cha kuanzia Februari 27 mpaka Machi 14, na kuandaliwa na mmoja wa wawekezaji wa kiutalii, kwa ushiriki wa washindani 50 kutoka nchi mbalimbali za Dunia.

Bwana Ashraf Mohi Eldin,  Mkurugenzi Mkuu wa Eneo la Piramidi za Mambo ya Kale alikuwa kwenye mapokezi yao, na ambaye alifuatana nao kwenye ziara ndani ya eneo hilo, kupitia ziara hiyo walitembelea Piramidi kuu, eneo la Abu al Hull na Panorama, na walihakikisha kusajili ziara yao kwa kupiga picha kadhaa za kumbukumbu.

Na inapangwa kwamba wale washiriki wataunda filamu fupi ya utangazaji (video) kwa ajili ya kutangaza Eneo la Utalii la Misri na kuonyesha aina yake na upekee wake, ambapo, kupitia siku zilizopita walitembelea idadi ya miji ya kiutalii, miongoni mwao Hurghada, Ain Sukhna na Kairo. 

Hiyo inakuja ndani ya mfumo wa nia ya Wizara ya Utalii na mambo ya Kale kwa kuunga mkono shughuli na matukio mbalimbali ili kufaidika  kutangaza kwa Vivutio mbalimbali vya Utalii na akiolojia, na pia ilikuja katika utekelezaji wa mikakati ya vyombo vya habari kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Misri.