Mapambano ya Bara la Afrika kuondolewa suala la Utumwa

Mapambano ya Bara la Afrika kuondolewa suala la Utumwa

Imeandikwa na| Shimaa Tarek

Tangu wakati mrefu, biashara ya watumwa bado yajadiliwa kikali na Wanahistoria wa Marekani, hilo linatokana na mwendelezo wa vita vya maadili na kisiasa vilivyozinduliwa na wapinzani wake tangu karne ya 18, licha ya ukweli wa biashara ya watumwa umetangazwa vibaya na vyombo vya habari, bali Wanahistoria wengi waatalam huko Marekani walijua masuala mengi yanahusiana biashara ya watumwa huko Pwani ya Afrika Magharibi, pamoja na hayo , mnamo 1969 Philippe Decoutan amechapisha kitabu chake cha Biashara ya Watumwa ya Atlantiki ( The Atlantic Slave Trade , A. Censure) na ndani yake ameeleza idadi ya Waafrika katika biashara hiyo tangu karne 4 haswa mnamo karne ya 16 hadi karne ya 19, vile vile Decuton ameeleza kwamba vyanzo vya ongezeko la Watumwa na mahali pa kuwanunua Barani Afrika vilibadilikwa tangu muda mrefu .(٢٠٠٩محمد أمطاط  )

Aidha, Suala la Utumwa huko Afrika Magharibi limeanza kutokeza wazi haswa nchini Mauritania kiasi kwamba Suala hilo likawa lafanyika wazi huko, pia inasemekana kuwa ndani ya baadhi ya marejeleo ukoloni wa Ufaransa ulijaribu kuondolewa suala hilo,na ilitajwa kuwa sababu ya kuliendelea huko baadhi ya watu walibaki kuhifadhi watumwa kwa sababu ya viunganishi vya kidini na kihistoria vya pamoja kati yao, pia Ukoloni wa Ufaransa umejenga miji mingi inayohusiana na watumwa wanaoasi mabwana wao, basi Jaribio la Ukoloni huo kuondoa Suala la Utumwa linaonekana wazi , lakini mnamo miongo iliyopita Mamlaka za Mauritania zilikanusha kufanya Suala hilo huko, lakini ripoti zilizotolewa na Mashariki ya kimataifa ya Haki za Binadamu zimeashiria kuwa Utumwa bado wafanyika kwa siri ndani ya maeneo mbali ya vijijini ,na imetolewa takwimu na Mashirika hayo yakiwemo Shirika la mwisho "Wawalak Firi" zaashiria kuwa Mauritania iko mbele miongoni mwa nchi ambapo Utumwa unazifanyikwa pia ziliashiria kwamba asilimia ya watumwa huko Mauritania ni kutoka 10 hadi 20% .(awast.com,2015)

Vilevile, kuhusiana na waathirika wa suala hilo ambapo idadi ya waathirika wa suala hasi huko Somalia walifikia 121,900 na Dijibouti 4,600 , takwimu hizo zote zinasisitiza hasi ya jambo hilo , pia zinasisitiza umuhimu wa kulipambana na juhudi za Mauritania ,Somalia ,Dijibouti na nchi zote za Kiafrika dhidi ya suala hilo ,hadi tulifikia awamu muhimu kuwa nchi hizo ni mfano bora zaidi katika kupambana na suala la Utumwa na ukoloni ambao unazingatiwa aina nyingine ya Utumwa .

Inaonekana kwamba tatizo la Utumwa  si jipya huko Mauritania bali Afrika zima,basi nalo linaendelea bado katika jamii zote kwa sbabu ya hali mbaya ya kiuchumi na jamii za ndani mnamo miaka kadhaa , ikijaribu kuondolewa kwa nguvu ,ambapo utamaduni ,makabila na jamii yako nyingi sana,pamoja na hayo makundi mengi yapo katika suala hilo kujaribu kuanzisha suala hilo na kuliendelea Kwa mslahi na makusudi maalum yasiyohusiana na mapambano ya jamii za kiafrika dhidi ya suala hilo .(Andrè Rütti,2017)


Vilevile, aina za Utumwa ziko nyingi sana na zinatokeza kwa mtindo tofauti tofauti wazi sana haswa Utumwa ukitegemea ndoa huko Mauritania , nayo ni aina moja ya Utumwa wa sasa, pia mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa anayejali kwa aina za Utumwa wa sasa , ameeleza kuwa watumwa huko Mauritania , haswa wanawake na watoto wanapambana Ukatilii vibaya, unyanyasaji na Ukatilii wa ngono,  wanawatendea kama vitu vya kumilikiwa,hawana maoni hata,pia aliongeza kwamba Utumwa ukitegemea tabaka ni tatizo kubwa sana, ambapo watu wenye tabaka zilizokandamizwa na za kati wanapambana kulipiza kisasi vibaya na kunyimwa kufikia huduma za msingi na tabaka zinazotawala .(News.Un,2020)


Huo ndio unaathiri kikubwa kwenye pande zote za Nchi hiyo  ndani ya nyanja zote, wakati ambapo Filip Alston mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Umaskini uliokithiri na Haki za Binadamu alisema kuwa ikiwa tajiri za Mauritania hazisambazi kwa haki kwenye watu wake, Mauritania itapambana ukosefu wa Utulivu, pia alionya kwamba kiasi 44% kutoka watu wanaishi ndani ya umaskini mzito, vilevile Suala hilo linaathiri vibaya upande wa kisiasa kikubwa huko, ambapo Kundi la Haratine na Waafrika wa Mauritania hawapa madaraka yote na hawana haki katika pande za maisha ya kiuchumi na kijamii, licha ya Makundi hayo mawili yanashikilia theluthi mbili ya watu bali hawachukui haki zao na mahitaji yao wakitosheka, pia Bw. Alston wakati wa hitimisho la ziara yake ya kwanza rasmi huko Mauritania alisisitiza lazima serikali ifanye juhudi kubwa zaidi kutatua athari za Utumwa, na kutolewa kanuni maalum inapitisha kuwa kila raia wa Mauritania ana haki kamili katika haki yake ya kimsingi kama maji, huduma ya afya, elimu na vyakula .(News.Un,2016)

Vilevile, umuhimu wa makala hiyo unatokeza ukitegemea malengo ya Maendeleo Endelevu yanayohusiana na Haki za Binadamu, uhalifu  Utumwa pia kuukatizwa , wakati ambapo Mauritania inaweka sheria inayoharamisha Utumwa na kuadhibu yeyote anaufanya huo, pia tarehe Agosti 13, 2015, Jumuiya ya kitaifa ya Mauritania mnamo Agosti 13,2015,ilipitisha sheria Na.049/15 badala ya sheria Na.13/011 iliyotolewa tarehe Januari 23,2013 hiyo inasema adhabu ya halifu za Utumwa na kutesa kwa sababu nayo halifu dhidi ya Utu, pia kanuni yenye vifungu26, ibara ya 3 kinasema kuadhibu kila uzalishaji au kazi ya kiutamaduni na kisanaa inaheshimu Utumwa kwa kufungwa miaka 6, na kuisitisha, pamoja na hayo sheria iliweka faini dhidi ya kila mtu anatesa mtu yeyote kama mtumwa, adhabu hiyo imefika miaka 10 na faini hiyo imefika Awqiyyah millioni tano ( kiasi Dola elfu14) .(Middle-east,2018)

Pia, Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Utumwa Gulnara Shahinian amepongeza serikali ya Mauritania kwa hatua zilizochukuliwa kutokomeza Utumwa nchini humo lakini akataka vitendo zaidi  na kali kwa kutekeleza sheria hiyo, na alisema: "vikundi vya kiraia vina dhima kubwa katika kutokomeza huo kwa kuhamasisha jamii na vijana kuelewa aina za Utumwa na mbinu za kuondokana nao " .(News.Un,2014) 

Jumuiya kuu ya Umoja wa Mataifa ilichangia kutatua shida hiyo,ambapo iliainisha tarehe Decemba 2 ya kila mwaka kama siku ya Kimataifa kwa Kuondolewa utumwa , pia tarehe hiyo iliashiria kwamba Jumuiya hiyo ilipitisha mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara haramu ya binadamu, na mkataba huo unazingatiwa wa kwanza kuhusu suala hilo, na ilipitishwa mnamo 1949, vilevile , siku hiyo ya kimataifa yanalengea kuondolewa Utumwa na aina zake zinazoathiri matabaka yote haswa tabaka duni, aidha siku hiyo inazingatia vizuri kuondolewa aina zote za Utumwa wa kisasa kama ndoa ya kulazimshwa , kazi za watoto na biashara huruma za binadamu na aina zake zote, pia Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusiana na dawa za kulevya na uhalifu ilieleza kuwa idadi ya waathirika zinaongezeka daima haswa biashara haramu ya binadamu, kwa mujibu wa changamoto hizo zote , Jumuiya ya kimataifa ilijaribu  kufanya juhudi kubwa ili kuzipambana kupitia protokoli ya kukomesha na kuadhibu biashara haramu ya binadamu ya mktaba wa Umoja wa Mataifa kwa kupambana na uhalifu na nchi 158 zilishiriki ndani yake , vilevile protokoli hiyo inalengea kukabiliana na masuala ya biashara haramu ya binadamu kukuza hatua za uadilifu, kulazimsha nchi zinazoshiriki kupambana na suala hilo, kusaidia waathirika na kuhamasisha ushirikiano kati ya nchi hizo .(UNODC.org,2022)


Kwa mujibu wa Jumuiya kuu ya Umoja wa Mataifa iliyotoa tangazo la Dunia kwa Haki za Binadamu kama kiwango cha pamoja kati ya watu na mataifa, kinachosema kuwa suala la Utumwa na biashara yake kwa aina zake zote haliruhusiwi, na hilo limeshatekelezwa kufuatana na mkataba ambao umetiwa saini huko Geneva mnamo  Septemba 25,1926,  unaolenga Kuondolewa Utumwa na biashara hiyo . (Ohchr.org,1956)

Hatimaye, Suala la Utumwa lazingatiwa hatari zaidi linaloshikilia hatari kubwa huko Mauritania bali Bara zima la Afrika, kwa hivyo juhudi hizo kubwa zinatokeza zikijaribu kuondoa kabisa Utumwa , na kuwepo uadilifu na usawa kati ya watu wote ,licha ya matokea mabaya yaliyotokea na suala hilo, ila hatua muhimu ilikuwa katika kupambana na Ukoloni na yoyote inayokwamisha maendeleo na kuzuia haki za binadamu , Hilo ndilo halijazuia nchi za Bara la kiafrika kutoka kwa maendeleo 
na ustwai , pia Bara hilo litabaki mfano bora zaidi katika  kupambana na Ukoloni wa aina zake na kuzindua kuelekea uhuru .

Marejeleo

1-محمد أمطاط، ستيفان هان: من أعماق أفريقيا إلى العالم الجديد :مقاربات أمريكية لتاريخ العبودية، دار رباط الكتب،٢٠٠٩.

2-awast.com/home/articl,
الساعه٢, ٢٢/٥/٢٠٢٢, تاريخ العبودية في موريتانيا .

3-André Rütti, 2017,Constructing a Human Rights Campaigni: Contemporaray Slavery in Mauritania, UC Santa Barbara .

4-https://news.Un.org/ar/news/region/africa
الساعة٩, ٢٢/٥/٢٠٢٢, موريتانيا خبير أممي يعرب عن تشجيعه بالتقدم المحرز ، لكنه يشدد على أهمية فعل المزيد للقضاء الكامل على العبودية .

5-https://news.Un.org/ar/news/region/africa
الساعة٩, ٢٣/٥/٢٠٢٢, خبير أممي يحذر من مواجهة موريتانيا عدم الاستقرار إذا لم يتم توزيع ثرواتها على نحو أفضل .
6-Middle_east.online.com
الساعة ١٠، ٢٣/٥/٢٠٢٢, العبودية في موريتانيا ظاهرة تأبى الزوال .

7-https://news.Un.org/ar/news/region/africa,saa 1,30/6/2022,Mauritania badili ahadi : kuwa vitendo ili kudhibiti Utumwa:Mtaalamu .

8-https://www.unodc.org,12 o,clock,1/7/2022, international Day for the Abolition of Slavery .

9-https://www.ohchr.org,5 o,clock, 28/6/2022,Supplementary convention on the Abolition of slavery, the slave trade,and institutions and practices similar to slavery .